Swali
Je kulewa ni dhambi?
Jibu
Kulewa kwa pombe kumekatazwa wazi katika Biblia (Mithali 20:1; 23:20; 29-32; Isaya 5:22; Waefeso 5:18). Kunazo amri nyingi katika Maandiko kuhusu tabia za kuepukwa, kama vile ulevi, usherati (1 Wakorintho 6:18), na uongo (Mithali 6:16-17). Lakini Biblia ni zaidi ya orodha huhusan ya “dhambi.” Tunapoiangalia kwa mtazamo huo, tunakosa kuelewa wazo nzima. Mungu hataki tuondoe orodha na kuzingatia kila kitu kingine kuwa kinakubalika. Mafarisayo walifanya hivyo, na Yesu hakupendezwa nao (Luka 11:42; Mathayo 23:23). Mungu anatamani utiifu unaotokana na moyo wa upendo ambao unatamani kuwa kama Yeye (1 Petro 1:15).
Ulevi ni dhambi, lakini je, unywaji pombe wa kiwango? Kunywa pombe kumekuwa mada ya mjadala ndani ya kanisa kwa karne nyingi. Miaka mingi iliyopita Wakristo wengi walichukulia kunywa pombe kwa kiasi chochote kuwa dhambi. Leo hii kuna makubaliano zaidi kwa unywaji wa wastani wa pombe kati ya Wakristo. Katika nyakati za Biblia, mtu yeyote aliyetengwa kwa ajili ya Mungu alipaswa kujiepusha kabisa na matunda yoyote ya mzabibu wakati wa kuwekwa wakfu kwake (Waamuzi 13:4; Walawi 10:9; Hesababu 6:3; Luka 1:15). Mvinyo wakati mwingine ulikuwa ishara ya uchafuzi wa ulimwengu (Ufunuo 18:3), na wale walioitwa katika huduma ya kikuhani walipaswa kujiepusha nayo wakati wa kuhudumu katika hema la kukutania (Walawi 10:9). Maonyo kama hayo yamewaongoza wafuasi wengi wa Kristo kuacha pombe kabisa, wakiona matumizi yake kuwa si ya hekima. Ingawa kunywa kwa kiasi hakulaaniwei katika Maandiko, kushindwa kujizuia kumekataliwa, na kuna maonyo mengi kuhusu tabia ya uharibufu ya pombe (Mithali 20:1; 31:4).
Waefeso 5:18 inasema, “Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho.” Vitu viwili vinalinganishwa hapa: mvinyo na Roho Mtakatifu. Kila mmoja ana nguvu za kudhibiti akili na tabia ya mtu- kwa matokeo tofauti kabisa. Kulewa husababisha kupoteza kujizuia; kujazwa na Roho husababisha kujizuia zaidi(Wagalatia 5:22-23). Hatuwezi kutawaliwa na roho za kileo na Roho Mtakatifu kwa wakati mmoja. Tunapochagua kumeza vitu vinavyobadilisha akili, tunachagua kwa ufanisi kujitoa kwenye udhibiti wa kitu kingine isipokuwa Roho Mtakatifu. Kitu chochote kinachodhibiti akili, mapenzi, na hisia zetu ni mungu wa uongo. Bwana yeyote tunayemtii isipokuwa Bwana ni sanamu, na kuabudu sanamu ni dhambi (1 Wakorintho 10:14).
Kulewa ni dhambi. Iwe ni pombe, dawa za kulevya, au tabia nyingine ya uraibu, Yesu alisema, “Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili” (Mathayo 6:24). Wakati tunalewa kwa pombe au dawa za kulevya, tunamtumikia bwana mwingine badala ya Bwana. Kuchagua kumfuata Yesu kunamaanisha kuchagua dhidi ya mifumo na maisha yetu ya zamani ya dhambi. Hatuwezi kumfuata Yesu na pia kufuata ulevi, usherati, au mawazo ya kilimwengu (Wagalatia 2:20; Warumi 6:1-6). Zote zinaenda pande tofauti. Andiko la 1 Wakorintho 6:10 linaorodhesha walevi kati ya wale ambao “hawataurithi ufalme wa Mungu.” Wakati tunachagua kutambuliwa kwa dhambi, hatuwezi pia kuwa wafuasi wa Kristo (Wagalatia 5:19-21). Tunapochagua ulevi licha ya amri ya Mungu dhidi yake, tunachagua kutotii na hatuwezi, katika hali hiyo, kuwa katika ushirika na Mungu mtakatifu anayeihukumu (Luka 14:26-27; Mathayo 10:37-38).
English
Je kulewa ni dhambi?