Swali
Ni nini maana ya kuhuzunisha / kumzimisha Roho Mtakatifu?
Jibu
Wakati neno "kuizima" limetumika katika maandiko, yanazungumzia moto wa kukandamiza. Wakati waumini wanavaa ngao ya imani, kama sehemu ya silaha yao ya Mungu (Waefeso 6:16), wao huzima nguvu ya mishale ya moto kutoka kwa Shetani. Kristo ilivyoeleza kuzimu kama mahali ambapo pa moto ambao "hauzimiki" (Marko 9:44, 46, 48). Vile vile, Roho Mtakatifu ni moto ambao umeweka makao katika kila ndani ya muumini. Yeye anataka kujionyesha Mwenyewe katika matendo na mitazamo yetu. Wakati waumini hawaruhusu Roho kuonekana katika matendo yetu, wakati sisi hufanya chenye tunajua ni mbaya, sisi hukandamiza au kumzimisha Roho. Hatuwezi kuruhusu Roho kujidhihirisha yeye mwenyewe kwa njia atakavyo.
Kuelewa ni nini maana ya kumhuzunisha Roho, ni lazima kwanza kuelewa kwamba hii inaonyesha Roho ana utu. Ni mtu tu anaweza kuhuzuni, kwa hiyo, Roho ni lazima awe ni mtu wa uungu ili aweze kuwa na hisia hii. Pindi tunapoelewa hili, tunaweza kuelewa vizuri jinsi Yeye anahuzunishwa, hasa kwa sababu sisi pia tunahuzunishwa. Waefeso 4:30 inatuambia kwamba tusimhuzunishe yule Roho. Sisi uhuzunisha Roho kwa kuishi kama wakafiri ( 4:17-19), kwa uongo ( 4:25), kwa kuwa na hasira (4:26-27), na kuiba (4:28), na kulaani (4:29), kwa kuwa na uchungu ( 4:31), kwa kuwa wa kutosamehehe ( 4:32), na kwa kuwa wazinzi ( 5:3-5). Kumhuzunisha yule Roho ni kuigiza njia ya dhambi, hata kama ni katika mawazo tu au katika yote mawazo na matendo.
Zote kuuzima na kuhuzunisha Roho ni sawa katika madhara yake. Zote huzuia maisha ya kiungu. Zote hutokea wakati muumini anasini dhidi ya Mungu na ifuatavyo tamaa yake mwenyewe ya kidunia. Barabara pekee sahihi ya kufuata ni barabara imwelekezayo muumini karibu na Mungu na usafi, na mbali zaidi kutoka kwa dunia na dhambi. Kama vile sisi hatupendi kuhuzunishwa, na vile sisi hatutafuti kuyazima yaliyo mema -hivyo tunapaswa tusimhuzunishe au kumzimisha Roho Mtakatifu kwa kukataa kufuata uongozi wake.
English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili
Ni nini maana ya kuhuzunisha / kumzimisha Roho Mtakatifu?