Swali
Kumjua Yesu dhidi ya kujua juu ya Yesu-tofauti iko wapi?
Jibu
Mitandao ya burudani na majarida hutusaidia kujibu swali hili. Wapennzi wa kanda, runinga, muziki au riadha hutumia pesa na wakati mwingi ili kupata habari, picha, na burudani kuhusu nyota wanaowashabikia. Baada ya kusoma jarida kama hizo, mashabiki hujihizi kuwa wanafahamu mashujaa wao vyema. Lakini, je! wanawajua? Wanaweza kujua ukweli Fulani juu ya shujaa wao. Wanaweza kutaja tarehe ya kuzaliwa kwao, rangi waipendayo, na vitu walivyovipenda wakiwa Watoto, lakini, ikiwa walikuwa wakutane na huyo shujaa ana kwa ana, shujaa atasema nini? Je huyo shabiki anamjua shujaa vyema?
Yesu alijibu swali hili katika Mathayo 7:21-23: "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu." Kulikuwa na watu katika nyakati za Yesu waliofikiria kuwa walikuwa marafikize kwa sababu waliifahamu sheria, walitengeza masharti kali kwa ajili yao wenyewe (na kwa wengine), na walisikiza mafundisho yake. Walimfuata, walipongeza miujiza yake, na kupenda baadhi ya kile alisema. Lakini Yesu anawaita "watenda maovu" na kusema "sikuwajua nyinyi."
Leo hii kunao maelfu ya watu wanaojua habari ya Yesu-hiyo ni kusema, wanajua kweli Fulani kumhusu, wanaweza kariri aya fulani za Biblia, na pengine wanahudhuria kanisa. Lakini hawajawai ruhusu kweli hizo kuwa kweli yao ya kibinafsi. Wao wanashikilia ufahamu vichwani mwao bila kuruhusu ukweli kupenya nyoyo zao. Yesu alielezea shida hii: "Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu" (Mathayo 15:8-9; Marko 7:6).
Inaweza kuwa rahisi kubadilisha dini kwa uhusiano halisi na Kristo. Kila mara twafikiria kwamba, ikiwa tunafanya "matendo ya dini," hiyo ndiyo inahitajika. Tunaweza shukuru kweli kwamba kifo cha Yesu na ufufuo wake, lakini hadi tumfanye Bwana wetu, ukweli huo hauwezi tufanyia chochote (Yohana 3:16-18; Matendo 10:43; Warumi 10:9). Kunayo tofauti kati ya elemu ya juu na imani inayookoa. Kumjua Yesu inamaanisha tumekubali dhabihu yake kwa niapa yetu (2 Wakorintho 5:21). Tumuuliza awe Mwokozi wa maisha yetu (Yohana 1:12; Matendo 2:21). Tunashirikiana nay eye katika kifo chake and kuhesabu nafsi zetu za kale kufa pamoja naye (Wakolosai 3:3 Warumi 6:2, 5; Wagalatia 6:14; 2:20). Tunakubali msamaha wake utakazo kutoka dhambini na kutafuta kumjua zaidi katika ushirika kupitia Roho Mtakatifu (Yohana 17:3; Wafilipi 3:10; 1Yohana 2:27).
Wakati tunatubu dhambi zetu na kutoa maisha yetu kwake, Yesu anatupa Roho Mtakatifu (Matendo 2:38; Yohana 14:26; 16:13). Roho Mtakatifu huja na kukaa ndani yetu, na kutubadilisha milele (1 Wakorintho 6:19; 1 Yohana 3:9). Kweli tunajua kuhusu Yesu huwa hai tunapoendelea kumjua kibinafsi. Hebu na tuseme umesoma kwamba shujaa wa kanda umpendayo ana macho ya kijani kibichi na kifinyo katika mashavu yake. Dalili hizo ni kweli tu katika maelezo hadi ukutane nay eye ana kwa ana. Ghafla bini ghafla macho hayo ya kijani kibichi yanakuangalia na kifinyo katika mashavu yake kujitokeza kwenye mashavu yake wakati anapotabasamu. Anakuelezea jinsi siku yake ilikuwa, hofu yake, na mawazo yake ya ndani. Unaweza kumbuka kwamba ulikwisha sikia kweli hizo mbeleni, lakini sasa unazishuhudia. Ulikuwa unajua kumhusu, lakini sasa umemtambua. Chenye ulikuwa unajua kinageuka na kuwa kweli. Dilili ilifikiria unajua zinaanza kuwa na maana unapoingia katika uhusiano.
Yesu ni nafsi. Kumjua ni kuingia katika uhusiano. Amri kuu ni "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote" Mathayo 22:37; Marko 12:30; Luka 10:27). ni vigumu kumpenda mtu ambaye humjui. Kumpenda Yesu huanza na kunyenyekea kwa mpango wake juu ya maisha yako. Hiyo ndiyo inamaanisha kumfanya Bwan (Mathayo 6:33; Warumi 10:9-10; Zaburi 16:8). asili ya Mungu ni kuu na ngumu kiasi kwamba hakuna mwanadamu ambaye anaweza kufahamu kikamilifu kila kitu kinafaa kujulikana juu yake. Lakini maisha ni kuendelea kumtafuta, kujifunza mengi juu yake, na kufurahia ushirika wake (Yeremia 29:13; Wafilipi 3:8).
English
Kumjua Yesu dhidi ya kujua juu ya Yesu-tofauti iko wapi?