Swali
Je! Mkristo ambaye ni bikira anaweza kuolewa na mtu ambaye sio bikira?
Jibu
Ndoa bora ya Kikristo ni kweli, wakati wote wawili ni bikira, baada ya kuelewa kuwa ndoa ndiyo pahali pekee panmahusiano ya ngono mbele ya macho ya Mungu. Lakini hatuishi katika ulimwengu bora. Mara nyingi, mtu aliyelelewa katika Ukristo na kuokolewa kutoka utoto hupenda kuoa mtu aliyeokolewa katika miaka yake ya 20 au 30 na ambaye huleta kwenye ndoa ile maisha yake ya zamani aloiishi kulingana na viwango vya kidunia. Wakati Mungu anaweka dhambi zetu mbali na sisi kama jinsi mashariki ilivyo kutoka magharibi tunapokuja kwake kwa kutubu na imani katika Kristo (Zaburi 103: 12), watu wana kumbukumbu nyingi, na kusahau maisha ya zamani ya mtu inaweza kuwa jambo ngumu. Ukosefu wa kusamehe na kusahau makosa ya zamani ya mmoja wa washirika wa ndoa kwa hakika inathiri ndoa vibaya.
Kabla ya kufunga ndoa na mtua ambaye alijihusisha kwa ngona katika maisha yake ya zamani, ni muhimu kuelewa kwamba wokovu na msamaha wa dhambi tupatiwa kwa neema. "Kwa maana mmeokolewa neema, kwa njia ya imani; ambayo hio hailutokana na nafsi zenu, ni zawadi ya Mungu, wala sio kwa matendo, mtu yeyote asjije akajisifu" (Waefeso 2: 8-9). Tunapoanza kuelewa nini maana ya kusamehewa kweli, tunaanza kuona kupitia macho ya Mungu na jinsi anavyotupenda, na hio hutusaidia kusamehe wengine. Kusamehe ni kuyatupilia mabli m na kumwona akosa aliyefanya mtu fulani na kumuona kama kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17). Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi yake, na mchumba huyu sasa anahitaji kuamua ikiwa kumbukumbu ya dhambi hiyo anaweza kuishi nayo. Hapa ndipo ambapo fundisho linatoka kuwa maandishi tu kugeuzwa vitendo.
Katika masuala ya msamaha, daima husaidia kutazama maisha yetu ya kale kwa kupitia mtazamo wa Mungu. Dhambi ya ngono ni mbaya sana kwa Mungu, lakini vilevile uongo, kudanganya, mawazo mabaya, kunywa / kunywa sigara sana, kutokuvumilia, kiburi, na kutosamehe. Nani kati yetu hana dhambi na anaweza "kutupa jiwe la kwanza"? Kabla ya kuja kwa Kristo, kila mmoja wetu "amekufa katika makosa na dhambi" na hufanywa hai tu kwa neema ya Mungu (Waefeso 2: 1-5). Swali ni tunaweza kuwasamehe wengine kama Kristo alivyotusamehe? Kuwa na uwezo wa kufanya hivyo ni alama ya Mkristo wa kweli. Yesu alisema ikiwa hatusamehe, wala Mungu hatatusamehe (Mathayo 6: 14-15). Hakuwa anamaanisha kwamba kusamehe wengine ni njia ya kupata msamaha wa Mungu, ambayo tunajua ni kwa neema pekee, lakini kwamba moyo wa kusamehe ni ishara ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu ndani ya moyo wa mwamini wa kweli. Kuendelea kutosamehe ni ishara ya moyo mgumu, usio sawa.
Kabla ya kuingia katika ndoa na asiye bikira, mawazo mengi, sala, na kujitazama kwa undani ni muhimu. Yakobo 1: 5 inatuambia kwamba ikiwa mmja wenu amepungukiwa na hekima hekima, na aombe dua kwa Mungu awapaye wote, kwa ukarimu wala hakemei, naye atapewa. Kuzungumza na mchungaji wa wa Mungu na kushiriki katika kanisa la kufundisha Biblia litasaidia katika mchakato wa kufanya maamuzi. Makanisa mengine yana madarasa mazuri ya kabla ya ndoa. Pia, kuzungumza kwa wachumba kwa uhuru na kwa uwazi kuhusu mambo haya kunaweza kufunua mambo ambayo yanahitaji kushughulikiwa na kusamehewa.
Ndoa ina changamoto hata katika mazingira bora na inachukua kazi nyingi ili kuifanikisha. Washirika wote wanahitaji, na wanastahili, kupendwa bila kuwekewa vikwazo. Waefeso 5 inaelezea majukumu ya mume na mke katika ndoa, lakini kifungu hiki huanza na kanuni inayozidi kwa yote: ''mwe mnanyenyekeana katika kumheshimu Kristo" (Waefeso 5:21). Kutoa dhabihu na nguvu ya kuchagua kuwa mtumishi wa uboreshaji wa ndoa ni alama za mwanamume na mwanamke mzima wa kiroho wanaomheshimu Mungu. Kwa busara, kuchagua mke au mume kulingana na misingi za kibiblia ni muhimu, lakini cha muhimu vilevile ni ukuaji wetu wa kiroho na kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Mwanamume ambaye anajitahidi kuwa mtu Mungu anataka awe naye ataweza kumsaidia mkewe kuwa mwanamke Mungu anataka awe naye pia, licha ya maisha ya kale yao, wataweza kujenga ndoa yao kuwa ndoa inayomuheshimu Mungu ambayo, watakayoifurahia.
English
Je! Mkristo ambaye ni bikira anaweza kuolewa na mtu ambaye sio bikira?