Swali
Je! Bibilia inasema nini kuhusu kushikwa na mapepo? je! Hii yawezekana hii leo? Kama ni hivyo, dalili zake ni zipi?
Jibu
Bibilia inapatiana baadhi ya mifano ya watu waliopagagwa na mapepo au kuadhirika na mapepo. Kutokana na mifano hii tunaweza kupata dalili za kupagagwa na mapepo na kupata kujua vile mapepo yanaweza kumshika mtu. Hapa kuana baadhi ya aya za Bibilia: Mathayo 9:32-33; 12:22; 17:18; Mariko 5:1-20; 7:26-30; Luka 4:33-36; Luka 22:3; Matendo Ya Mitume 16:16-18. Ndani ya hizi kurasa, kupagagwa na mapepo kunaleta magonjwa ya mwili kama, kuwa kisiwi, dalili ya kifafa, kipofu na kadhalika. Katika sehemu zingine yanamfanya mtu kufanya maovu, Yudasi akiwa mfano mkuu. Katika Matendo Ya Mitume 16:16-18, roho wa pepo ulimpa msichana mtumwa uwezo wa kujua mambo yanozidi elimu yake. Mtu wa Gadarenesi aliyepagagwa na mapepo, alipagagwa na kikundi cha mapepo, alikua na nguvu zinazozidi za mwanadamu alikaa uchi katika makaburi. Mfalme Saulo, baada ya kuasi Mungu, alisumbuliwa na roho (1 Samweli 16:14-15; 18:10-11; 19:9-10) hali ya mawazo ikaingia papo hapo na nia ya kumwua Daudi ikaongezeka.
Kwa hivyo kuna wingi wa dalili za kupagagwa na mapepo , kama vile magonjwa ya kimwili ambayo hayawezi kuambatanishwa na shida za kimwili, hasira ya kutaka kumudhulu mwingine, kubadilika kwa hali kama vile, mawazo, nguvu sizizo za kawaida, tabia isiyo ya kawaida, hali ya kutokua na uhusiano na watu, vilevile uwezo wa kushiriki habari ambayo mtu hana uwezo wa kawaida wa kuujua. Ni muhimu kutilia maanani kuwa, Karibu zote, kama si zote za hizi tabia zaweza kuwa na maelezo mengine, kwa hivyo ni muimu kumtaja mtu aliyepagagwa na mapepo, kifafa sawa na Yule amepagagwa na mapepo. Kwa upande mwingine, tamaduni za magharibi huwa hazijukui ushirikisho wa kishetani katika maisha ya watu.
Kwa kuongezea hizi dalili za kuonekana au hisia, mtu anaweza kuangalia hali ya kiroho ambayo inaweza kuonyesha jinsi anaweza kushawishika na mapepo. Hii yaweza huzisha, kukataa kusamehe (2 Wakorintho 2: 10-11) na imani katika mafunzo ya uongo ambayo yamenee, hasa kuhusu Yesu Kristo na kazi ya yake ya utakazo (2 Wakorintho 11:3-4).
Kuhusu kuwepo kwa mapepo katika maisha ya Mkristo, mtume Petero ni kielelezo cha dhana kwamba muumini anaweza kushawishika na shetani (Mathayo 16:23). Wengine huwahuzisha wakristo walio chini ya nguvu za mapepo kuwa “wamepagagwa” lakini hakuna mfano wowote katika maandiko wa mkristo katika Kristo amepagagwa na mapepo. Wanathiologia/wachanganusi wa Bibilia wengi wanaamini kuwa mkristo hawezi kushikwa na mapepo kwa sababu ako na Roho Mtakatifu ambaye anakaa nao (2 Wakorintho 1:22; 5:5; 1 Wakorintho 6:19), na roho wa Mungu hawezi kamwe kukaa pamoja na mapepo.
Hatuambiwi kamili vile mtu anaweza kujiachilia kwa mapepo. Kama kesi ya Yudasi kinawakilisha, basi mtu anaufungua moyo wake kwa maovu kwa kesi kwa uchoyo (Yohana 12:6). Ili iwe rahisi kwamba ikiwa mtu atahurusu moyo wake kutawalwa na dhambi zingine za Kusini, inakua rahisi kwa pepo kuingia. Kutoka kwa wamisonari, usoefu, kupagagwa na mapepo kumehusiana na kuabudu miungu ya kujichongea na kupagagwa huku ni kwa mashetani. Maandiko kwa yarudia kuhuzisha kuabudu miungu sawa na kuabudu mapepo (Mambo Ya Nyakati 17:7; Kumbukumbu La Torati 32:17; Zaburi 106:37; 1 Wakorintho 10:20), kwa hivyo kisiwe kitu cha kushangaza kuwa kuwepo kwa kuabudu miungu waweza kuelekeza kupagagwa na mapepo.
Kulingana na kurasa za Bibilia hapo juu na baadhi ya usoefu wa wamisonari, tunaweza kumalizia kuwa watu wengi wanayafungua maisha yao kwa mapepo kupitia kwa kukumbatia dhambi au kujiuzisha kwa dini za kishetani (ama kwa kujua au kutojua). Mifano inaweza kuhuzisha, usherati, vivinyo ambavyo vinabadilisha hali ya akili, kuasi, hasira, na kuwaza yasiyostahili.
Kuna teteo zaidi. Shetani na uwekaji wake maovu, hawawezi kufanya chochote ambacho Mungu hajawaruhusu kufanya (Ayubu 1-2). Hii kuwa hali, shetani, akifikiria anafanikisha mapenzi yake, bali anakamilisha mapenzi ya Mungu, vile ilivyokua katika kesi ya Yudasi akimsaliti Yesu. Watu wengine wanaanza kuwa na mawazo yasiyo mema na dini mbaya na matendo ya kishetani. Hili si jambo la hekima na la kibibilia. Ikiwa tutamtafuta Mungu, na tukijivika silaha na tukitegemea uweza wake (Waefeso 6:10-18), hatuna chochote cha kuogopa kutoka kwa shetani, maana Mungu ako juu ya vyote.
English
Je! Bibilia inasema nini kuhusu kushikwa na mapepo? je! Hii yawezekana hii leo? Kama ni hivyo, dalili zake ni zipi?