settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kurudia katika sala?

Jibu


Yesu alisema katika Mahubiri ya Mlimani, " Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi." (Mathayo 6: 7). Neno 'bure' maana yake ni "tupu" au "haina maana"; hivyo Yesu anatuonya kwamba kurudia maneno yasiyo na maana katika sala zetu haitasaidia kusikilizwa na Mungu. Baba yetu wa mbinguni hahusiwi na idadi ya maneno, maneno ya mashairi , au maneno ya kurudiwarudiwa; Anapendezwa na "ukweli ulio moyoni" (Zaburi 51: 6).

Yesu anasema kuwa matumizi ya maneno ya kurudiarudia au maneno ya kanuni fulani ni "kipagani" na haipaswi kuwa sehemu ya sala ya Kikristo. Sala zetu zinapaswa kuwa kama vile sala rahisi na fupi ya Eliya kwenye Mlima. Karmeli na sio maombi ya muda mrefu na ya kurudia kama vile sala ya manabii wa Baali (ona 1 Wafalme 18: 25-39).

Tunapoomba, tunazungumza na Mungu na kumuabudu. Ni kama mazungumzo, kutoka kwa moyo. Dini nyingi-ikiwa ni pamoja na baadhi ya vitengo vya Kikristo-zina sala nyingi ambazo zinawashauri kurudia mara kwa mara. Makanisa mengine hata huenda kuwataka wanachama wao kusoma sala fulani idadi maalum ya nyakati ili kusamehewa dhambi. Hii ni upagani na ushirikina; sala hiyo ya mpangilio fulani ni "kurudia bure" ambazo hazina mahali kanisani. Yesu tayari ametakasa dhambi zetu mara moja na kwa wote (Waebrania 10:10), na tunaweza kujongea kiti cha enzi kwa ujasiri kwa sababu ya dhabihu ya Kristo (Waebrania 4: 15-16), sio kwa sababu ya "maneno mengi" yetu (Mathayo 6: 7).

Ni rahisi kujishughulisha kwa kurudia bure, kurudia maneno sawa katika sala zetu badala ya kufikiria juu ya maneno yetu au kuacha maneno hayo kutoka moyoni. Tunapaswa kuzingatia Mungu kwa sala na kumheshimu katika mioyo yetu. Katika Isaya 29:13, Mungu anasema, "Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali miyo yao iko mbali nam. ... "

Onyo la Yesu dhidi ya kurudiarudia ina maana ya kuwa tunapaswa kuepuka maneno yasiyo na maana au ya kurudia katika sala zetu. Mambo ya kurudia hupoteza muda, lakini sio thibitisho ya kujitolea kwetu na pia haitupi nafasi bora ya kusikika na Mungu. Tunapaswa kuwafundisha watoto wetu katika umri mdogo kuomba kwa namna ya asili, mazungumzo, kwa heshima kwa Yule wanaozungumzia.

Kujitahidi katika sala si sawa na kurudia maneno mara kwa mara. Hakuna chochote kibaya kwa kuomba kitu kimoja mara nyingi(ona 2 Wakorintho 12: 8). Baada ya yote, Yesu alitufundisha kwamba tunapaswa 'kuomba daima na kutoacha' (Luka 18: 1). Lakini inaeleweka kuwa sala zetu zinatoka moyoni, kwa hiari, na kumheshimu Mungu, sio kurudia maneno yaliyoandikwa na mtu mwingine.

Biblia inatufundisha kuomba kwa imani (Yakobo 1: 6), tukizungumza na Mungu moja kwa moja (Mathayo 6: 9), na kwa jina la Yesu (Yohana 14:13). Tunapaswa kutoa sala zetu kwa heshima na unyenyekevu (Luka 18:13), kwa uvumilivu (Luka 18: 1), na kwa utiifu wa mapenzi ya Mungu (Mathayo 6:10). Biblia inatufundisha kuepuka maombi ambayo ni ya unafiki, yanayolenga kusikilizwa tu na wanadamu (Mathayo 6: 5), au kutegemea kurudia bure (Mathayo 6: 7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kurudia katika sala?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries