settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inatufundisha kusamehe na kusahau?

Jibu


Maneno "kusamehe na kusahau" haipatikani katika Biblia. Hata hivyo, kuna mistari nyingi inayotuagiza "kusameheana" (k.m., Mathayo 6:14 na Waefeso 4:32). Mkristo ambaye hayuko tayari kusamehe wengine atapata kizuizi katika ushirika wake na Mungu (Mathayo 6:15) na anaweza kuwa uchungu na kupoteza tuzo (Waebrania 12: 14-15; 2 Yohana 1: 8).

Msamaha ni uamuzi wa kupenda. Kwa kuwa Mungu ametuamuru kusamehe, tunapaswa kufanya uchaguzi wa busara kumtii Mungu na kusamehe. Mkosaji anaweza asitamani msamaha na huenda asibadilike, lakini hilo halipingi matakwa ya Mungu kwamba tuwe na roho ya kusamehe (Mathayo 5:44). Kwa hakika, mkosaji atatafuta upatanisho, lakini, ikiwa hatafanya hivyo, mtu aliyekosewa anaweza kufanya uamuzi wa kusamehe.

Bila shaka, haiwezekani kusahau dhambi ambazo zimefanyika dhidi yetu. Hatuwezi "kufuta" matukio kutoka kwenye kumbukumbu yetu. Biblia inasema kwamba Mungu "hakumbuki" uovu wetu (Waebrania 8:12). Lakini Mungu bado anajua yote. Mungu anakumbuka kwamba "tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Lakini, baada ya kusamehewa, sisi tumefanywa wenye haki. Mbinguni ni yetu, haijalishi kuwa dhambi yetu imewahi kufanyika. Ikiwa sisi ni wake kupitia imani katika Kristo, Mungu hatatuhukumu kwa dhambi zetu (Warumi 8: 1). Kwa maana hiyo Mungu "husamehe na kusahau."

Ikiwa kwa "kusamehe na kusahau" mtu anamaanisha, "Mimi nachagua kumsamehe mkosaji kwa ajili ya Kristo na kuendelea na maisha yangu," basi hii ni njia ya busara na ya kiungu. Kwa kadiri iwezekanavyo, tunapaswa kusahau kilichotendeka hapo nyuma na kujitahidi kuelekea mbele (Wafilipi 3:13). Tunapaswa kusameheana "kama vile katika Kristo Mungu alitusamehe" (Waefeso 4:32). Hatupaswi kuruhusu mizizi ya uchungu kuongezeka ndani ya mioyo yetu (Waebrania 12:15).

Hata hivyo, ikiwa "kusamehe na kusahau" ina maana, "nitajifanya kuwa dhambi haijawahi kutokea na kuishi kama sikumbuki," basi kunaweza kuwa na tatizo. Kwa mfano, mwathirikaji wa ubakaji anaweza kumsamehe mkosaji, lakini hiyo haimaanishi kwamba anapaswa kujifanya kama dhambi hiyo haijawahi kutokea. Kukaa na mkosaji kwa mda hasa ikiwa hajatubu, haiambatani na mafundisho ya Maandiko. Kusamehe kunahusisha kutoshikilia dhambi dhidi ya mtu tena, lakini msamaha ni tofauti na imani. Ni busara kuchukua tahadhari, na wakati mwingine mambo vipengele katika uhusiano zitabadilika. "Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia" (Mithali 22: 3). Yesu aliwaambia wafuasi wake "kuwa wenye busara kama nyoka na wasio na hatia kama njiwa" (Mathayo 10:16).Tunapokuwa na ushirika na wenye dhambi wasiotubu, lazima tuwe "bila hatia" wakati huo huo "wenye busara" (kuwa waangalifu).

Lengo ni kusamehe na kusahau. Upendo hauhesabu mabaya(1 Wakorintho 13: 5) na hufunika uingi wa dhambi (1 Petro 4: 8). Hata hivyo, kubadilisha mioyo ni kazi ya Mungu, na, mpaka mkosaji ana kweli, mabadiliko ya moyo ya kweli, itakuwa busara tu kupunguza kiwango cha uaminifu kwa mtu huyo. Kuwa waangalifu haimaanishi sisi hatujasameha. Ina maana ya kwamba sisi sio Mungu na hatuwezi kuona moyo wa mtu huyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inatufundisha kusamehe na kusahau?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries