Swali
Biblia inasema nini kuhusu kushinda majonzi?
Jibu
Majonzi ni hisia ya kawaida katika maisha ya binadamu, na tunashuhudia mchakato wa majonzi katika biblia. Wahusika wengi wa Biblia walipata kushuhudia majonzi kubwa, ikiwa ni pamoja na Ayubu, Naomi, Hana, na Daudi. Hata Yesu aliomboleza (Yohana 11:35; Mathayo 23: 37-39). Baada ya Lazaro kufa, Yesu alikwenda kijijini cha Bethania, ambako Lazaro alizikwa. Yesu alipomwona Martha na wengine waliomboleza wakalia, pia alilia. Aliguzwa na majonzi yao na pia kifo cha Lazaro. Jambo la kushangaza ni kwamba, ingawa Yesu alijua kwamba angemfufua Lazaro kutoka kwa wafu, alichagua kushiriki katika majonzi ya hali hiyo. Kwa kweli Yesu ni kuhani mkuu ambaye anaweza "kuhurumia kwa udhaifu wetu" (Waebrania 4:15).
Hatua moja katika kushinda majonzi ni kuwa na mtazamo sahihi juu yake. Kwanza, tunatambua kuwa majonzi ni jibu la kawaida kwa maumivu na kupoteza. Hakuna kitu kibaya katika kuomboleza. Pili, tunajua kwamba nyakati za majonzi zinatimiza kusudi fulani. Mhubiri 7: 2 inasema, " Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake." Aya hii ina maana kwamba majonzi inaweza kuwa nzuri kwa sababu inaweza kupanua mtazamo wetu juu ya maisha. Tatu, tunakumbuka kuwa hisia za majonzi ni za muda mfupi. "Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha." (Zaburi 30: 5). Kuna mwisho wa kuomboleza. Maumivu ina madhumuni yake, lakini pia ina kikomo chake.
Katika yote, Mungu ni mwaminifu. Kuna maandiko mengi ambayo yanatukumbusha uaminifu wa Mungu wakati wa kuomboleza. Yeye yu pamoja nasi hata katika bonde la kivuli cha kifo (Zaburi 23: 4). Daudi alipokuwa na majonzi, aliomba hili katika Zaburi ya 56: 8: "Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)." Tunapofikiria jinsi Mungu anayafuta machozi yetu ni picha yenye maana. Anaona majonzi yetu na hayadharau. Kama Yesu alipoingia katika majonzi ya waombozi huko Bethania, Mungu huingia katika majonzi zetu. Wakati huo huo, Yeye hutuhakikishia kuwa yote hayajapotea. Zaburi 46:10 inatukumbusha "tulia" na kupumzika katika ujuzi kwamba Yeye ni Mungu. Yeye ni kimbilio yetu (Zaburi 91: 1-2).Katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. (Warumi 8:28).
Sehemu muhimu ya kushinda majonzi ni kuionyesha kwa Mungu. Zaburi zina mifano mingi ya kupeana moyo wako kwa Mungu. Kwa kushangaza, mtunga-zaburi hakumalizia ambapo alianza. Anaweza kuanza zaburi kwa maneno ya majonzi, lakini, karibu kabisa, yeye atamalizia kwa sifa (Zaburi 13, Zaburi 23: 4, Zaburi 30: 11-12; Zaburi 56). Mungu anatuelewa (Zaburi 139: 2). Tunaposhirikiana naye, tunaweza kufungua akili zetu kwa ukweli kwamba Yeye anatupenda, kwamba Yeye ni mwaminifu, kwamba Yeye ana udhibiti, na kwamba anajua jinsi atakavyofanya kazi kwa ajili yetu.
Hatua nyingine muhimu katika kushinda majonzi ni kushirikiana na wengine. Mwili wa Kristo (kanisa) ipo ili kupunguza mzigo wa wajumbe wake binafsi (Wagalatia 6: 2), na waamini wenzake wana uwezo wa "kuomboleza pamoja na wale wanaomboleza" (Warumi 12:15). Mara nyingi, majonzi huwazuia wengine, na kuongeza hisia za kutengwa na majonzi. Ni vizuri kutafuta ushauri, na mipangilio ya kikundi inaweza kuwa yenye thamani. Makundi huchangia kusikiliza na kuhimiza kwa manufaa, uchangamano, na uongozi katika kuondoa majonzi. Tunaposhiriki hadithi zetu na Mungu na wengine, majonzi zetu hupunguzwa.
Kwa kusikitisha, majonzi ni sehemu ya maisha ya binadamu. Kupoteza ni sehemu ya maisha, na majonzi ni jibu la asili kwa kupoteza. Lakini tuna tumaini la Kristo, na tunajua kwamba Yeye ni mwenye nguvu ya kutosha kubeba mizigo yetu (Mathayo 11:30). Tunaweza kuwasilisha uchungu wetu kwake kwa sababu Yeye hutujali (1 Petro 5: 7). Tunaweza kupata faraja kwa Roho Mtakatifu, Msaidizi wetu (Yohana 14:16). Kwa majonzi, tunatupa mizigo yetu kwake, tutegemee jumuiya ya kanisa, tupate ukweli katika Neno, na hatimaye kupata tumaini (Waebrania 6: 19-20).
English
Biblia inasema nini kuhusu kushinda majonzi?