Swali
Ninawezaje kushiriki ushahidi wangu wa Kikristo?
Jibu
Ushuhuda unaofaa ni ni ule unaonyesha uzoefu wako mwenyewe na Injili ya Kristo ili mtu mwingine awe na habari kuhusu mchakato wa wokovu. (1) Anza kwa kuandika maelezo ya jinsi ulivyomtumainia Kristo kukuokoa. Kujibu maswali yafuatayo kutakusaidia: a) Ni nani aliniambia kuhusu Kristo? b) Ni matukio gani ambayo yalisababisha kumtegemea au kumwamini Kristo? c) Nilimtegemea wakati gani Kristo? d) Nilikuwa wapi wakati nilipoamini kwanza? e) Ni jinsi gani imani katika Kristo imekuwa baraka kwangu?
Kwa mfano, huu. ni ushahuda wangu wa jinsi nilivyokuja kumtegemea Kristo kama Mwokozi wangu.
(2) Baadaye, andika mambo haya, kuifanya kuwa hadithi. Ifanye iwe kuwa rahisi kama iwezekanavyo. Kama lengo, jaribu kufanya urefu wa ushuhuda wako ili uweze kushiriki kwa ufanisi kwa dakika tatu au chini.
(3) Hakikisha umenukuu Maandiko sahihi katika ushuhuda wako. Kumbuka kwamba Maandiko ambayo yana mamlaka kwa sababu ni Neno la Mungu. Kwa mfano, ushuhuda wako unapaswa kuwa na ujuzi wako kwamba ulikuwa umetenganishwa na Mungu kwa sababu ya dhambi yako (Warumi 3:23), kutambua kwamba ungekaa milele mbali na Mungu ikiwa haungepokea msamaha (Warumi 6:23), ufahamu kwamba Mungu alimtuma Mwanawe pekee Yesu kufa na kulipa dhambi yako (Warumi 5: 8), na hatimaye kupokea msamaha kwa kuamini kuwa Kristo peke yake aligharamia dhambi (Matendo 16:31).
Ingawa kama mtoto na kijana nilizungumza na mchungaji mara tatu au nne kuhusu jinsi nitakavyoweza kwenda mbinguni wakati nitakapokufa, sijawahi kuelewa kweli Injili ya Kristo mpaka nilipokuwa na umri wa miaka 20. Nilianza kusoma Biblia kwa miaka michache, kusikiliza walimu wa Biblia wenye kihafidhina kwenye televisheni, na kujadili yale niliyoyasikia na Wakristo kazini. Kwa njia hii, niligundua kwamba nilikuwa mwenye dhambi aliyejitenga na Mungu na nilistahili utengano huo milele. Hii ilikuwa msingi wa Waroma 3:23 "Wote wamefanya dhambi na wamepungukiwa na utukufu wa Mungu" na Warumi 6:23 "mshahara wa dhambi ni mauti." Nilikuja kuelewa kwamba Mungu anipenda sana hata alimtuma Wake Mwana Yesu, na Yesu alikuja duniani hasa kwa ajili ya kufa kwa ajili ya dhambi zangu (na dhambi za ulimwengu wote) ili nipate kusamehewa (Warumi 5: 8; Yohana 3:16).
Hatimaye, nilifahamu kwamba hakuna njia ambayo ningeweza kuwa mzuri au kufanya nzuri ndiposa nistahili mbinguni. Warumi 3:10 inasema hakuna yeyote anayefanya mema na Waefeso 2: 8-10 inasema kuwa wokovu ni zawadi ya Mungu, sio kitu ambacho mtu hufanyia kazi, na inapokewa tu kwa imani, ambayo ni kuamini tu au kutegemea kabisa kifo, kuzikwa, na ufufuo wa Kristo kama malipo ya dhambi yangu. Baada ya kuelewa ukweli huu kutoka kwa Maandiko, nilikuwa na hisia ya uhakika kwamba kwa sababu sikuweza kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu, siwezi kuupoteza kwa sababu ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Kulikuwa na hisia kubwa ya msamaha kwa kujua kwamba nimewasamehewa na kwamba Mungu alikuwa upande wangu na bado anataka kile ambacho ni bora kwangu. Tangu mwanzo wa maisha yangu na Kristo, Yeye, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu ambaye anaishi moyoni mwangu, anaendelea kunitakasa kupitia Neno Lake na Kazi yake katika maisha yangu. Huu msamaha na usalama ambayo ninao kutoka kwa Mungu inaweza kuwa yako pia ikiwa utamwamini Kristo pekee kwa msamaha wa dhambi zako.
English
Ninawezaje kushiriki ushahidi wangu wa Kikristo?