settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu kesi kotini?

Jibu


Mtume Paulo aliwaonya Wakristo wa Korintho kuwa wasipelekane mbele ya koti wao kwa wao (1 Wakorintho 6:1-8). Kwa Wakristo wasiposameheana wao wenyewe na kupatana kwa tofauti zao ni kuonyesha kushindwa kiroho. Ni kwa nini mtu athamani kuwa Mkristo ikiwa Wakristo wenyewe wako na shida nyingi na hawana uwezo wa kuzitatua hizo shida zinazowakabili? Ingawa, kuna matukio mengi ambayo koti itakuwa ya muimu kutatua tofauti kati ya Wakristo. Ikiwa mtindo wa Kibiibilia wa upatanisho utafuatwa (Mathayo 18: 15-17) na mwenye makosa bado angali na makosa, katika nyakati zingine koti inaweza kukubaliwa hapa. Hii tu itafanyika baada ya maombi mengi ili tupate hekima (Yakobo 1:5) na kushauriana na uongozi wa kiroho.

Mukhtadha wote wa 1 Wakorintho 6:1-6 wahusika na tafauti katika Kanisa, lakini Paulo anarejelea mfumo wa koti wakati anaponena juu ya hukumu kuhusu mambo yanahusiana na maisha haya. Paulo anamaanisha mfumo wa koti upo kwa mambo ya maisha haya ambayo yako nche ya Kanisa. Shida za kanisa. Matatizo ya Kanisa yasichukuliwe mbele ya mfumo wa koti, bali yatatuliwe ndani ya Kanisa.

Matendo Ya Mitume mlango wa 21-22 wazungumzia kuhusu Paulo akiwa ameshikwa na kuwekelewa makosa ambayo hajayafanya. Warumi walimtia mbaloni na “amri jeshi mkuu akamuingiza Paulo ndani na kuamuru achabwe fimbo ili wamfanye akubali makosa yake, Paulo akamwambia afisa aliyesimama hapo, ‘Je! Ni sheria wewe kumwadhibu kwa kiboko Mrumi ambaye hajaribiwa kisimbani?’” Paulo aliitumia sheria ya Rumi na urahia wake kujikinga. Hakuna makosa yo yote kwa kutumia mfumo wa kotini bora ufanywe kwa nia njema na roho takatifu.

Paulo zaidi anasema, “Basi imekuwa upunguvu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afahdali kudhulumiwa? Maana si afahdli kunyangánywa mali zenu?” (1 Wakorintho 6:7). Mambo ambayo Paulo yanamsumbua Paulo hapa ni ushuhuda wa Wakristo. Itakuwa vyema zaidi kwetu kudhulumiwa, au kutusiwa, badala yetu kumsukuma mtu mbali na Kristo kwa kumchukua kotini. Ni lipi la muimu sana- vita vya sheria au vya kupigania nafsi ya mtu kwa uzima wa milele?

Kwa ufupi, je! Wakristo wanastahili kuwapeleka Wakristo wengine kotini kwa mambo yanayohusiana na Kanisa? Kwame la! Je! Wakristo wanastahili kupelekana kotini kwa kesi ya kibianafsi? Ikiwa itaweza kwa njia yo yote ile itaweza kuepukwa, la. Wakristo wanastahili kuwapeleka wasio Wakristo kotini makosa wamewafanyia? Pia ikiwa itaweza kuepukika, la. Ingawa katika hali zingine, kama vile kulinda haki zetu (ndio mfano wa Mtume Paulo), inaweza kuwa sawa kwa kutafuta suluhisho kisheria.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu kesi kotini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries