settings icon
share icon
Swali

Nini madhumuni ya ndoa?

Jibu


Je, ni muhimu kwa Mkristo kuolewa? Ni nini kusudi la ndoa? Biblia ina mengi ya kusema juu ya mada hii. Kwa kuwa ndoa ya kwanza ilikuwa kati ya mwanamume wa kwanza na mwanamke wa kwanza, inaonekana kuwa ndoa ni mapenzi ya Mungu kwa watu wengi. Ilianzishwa katika hali isoyo ya hatia na hivyo ni shirika takatifu. Sababu ya kwanza ambayo Biblia inatoa kwa kuwepo kwa ndoa ni rahisi: Adamu alikuwa peke yake na alihitaji msaidizi (Mwanzo 2:18). Hii ni kusudi la msingi la ushirikiano wa ndoa, ushirika, na usaidizi na faraja.

Lengo moja la ndoa ni kujenga nyumba imara ambayo watoto wanaweza kukua na kustawi. Ndoa bora ni kati ya waumini wawili (2 Wakorintho 6:14) ambao wanaweza kuzaa watoto wenye kumcha Mungu (Malaki 2: 13-15). Katika Malaki, Mungu anawaambia Waisraeli kuwa hatakubali sadaka zao kwa sababu wamekuwa wasio waaminifu kwa wake wa ujana wao. Hii inaonyesha jinsi Mungu anavyojali juu ya ndoa kudumishwa. Sio hilo tu, lakini anawaambia Yeye alikuwa akitafuta "uzao wa kiungu." Hiki ni kifungu cha kushangaza, na kimetafsiriwa kumaanisha a) kwamba uzao wa wenye kumcha mungu ni kusudi la ndoa; b) kwamba ndoa nzuri kati ya watu wawili wa Mungu itamaanisha kuwa watoto wowote wanao watakuwa wa wenyekumcha Mungu pia; c) Mungu alitaka Waisraeli kuwa waaminifu kwa wake zao badala ya kuwaacha na kuwaoa wanawake wa kigeni ambao watawazalisha watoto wao wasiomcha Mungu kwa sababu ya ibada ya sanamu ya mataifa hayo; na d) kwamba Mungu Mwenyewe alikuwa akitafuta watoto Wake mwenyewe (watu) kuonyesha uungu kwa uaminifu wao. Katika tafsiri yoyote hii, tunaona mada ya kawaida: watoto wa watu waaminifu watakuwa waaminifu, pia.

Ndoa sio kufundisha watoto jinsi ya kuwa mwaminifu tu, na kuwapa mazingira imara ambayo kujifunza na kukua, ina athari ya kutakasa pia kwa washirika wote wa ndoa wanapojiwasilisha kwa sheria ya Mungu (Waefeso 5). Kila ndoa ina wakati mgumu au mienendo ngumu. Wakati watu wawili wenye dhambi wanajaribu kuunda maisha pamoja, wanapaswa kuwasilisha kwa amri ya Mungu ya kupendana kama vile Mungu ametupenda-bila ubinafsi (1 Yohana 3:16). Jitihada zetu za kufuata amri za Mungu kwa nguvu zetu wenyewe huishia kushindwa, na kushindwa huko hufanya mwamini kujua kumtegenea Mungu na zaidi kukubali kazi ya Roho ndani yake, ambayo husababisha kumcha Mungu. Na utakatifu hutusaidia kufuata amri za Mungu. Hivyo, ndoa husaidia sana kwa mtu anayejaribu kuishi maisha ya kimungu; husaidia kuweka moyo safi, bila ubinafsi na uchafu mwingine.

Ndoa pia inalinda watu kutoka kwenye uasherati(1 Wakorintho 7: 2). Dunia tunayoishi imejaa picha za ngono na majaribu. Hata kama mtu hafuati dhambi ya ngono, inamvuta, na ni vigumu sana kuiepuka. Ndoa hutoa nafasi nzuri ya kuonyesha maapenzi, bila kujihatarisha kihisia na mara nyingi kuepuka uharibifu wa kimwili, uharibifu unaosababishwa na mahusiano ya kiholela ya ngono. Ni wazi kwamba Mungu aliumba ndoa kwa manufaa yetu (Methali 18:22), kutufanya kuwa wenye furaha, kukuza jamii bora, na kuzalisha utakatifu katika maisha yetu.

Hatimaye, ndoa ni picha nzuri ya uhusiano kati ya Kristo na kanisa lake. Mwili wa waumini ambao huunda Kanisa na kuitwa bibi wa Kristo. Kama Bwana-arusi, Yesu alitoa maisha yake kwa Bibi arusi wake, "kumfanya awe mtakatifu, kumtakasa kwa kuosha kwa maji katika neno" (Waefeso 5: 25-26), na kitendo chake cha kujidhabihu kinatoa mfano kwa waume wote. Kuja kwa pili kwa Kristo, kanisa litaungana na Bwana arusi, "sherehe ya arusi" rasmi itafanyika, na kwa hivyo umoja wa milele wa Kristo na bibi yake itafanyika (Ufunuo 19: 7-9; 21: 1-2).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini madhumuni ya ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries