settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kutafuta uso wa Mungu?

Jibu


Mara nyingi katika Maandiko, watu wa Mungu wanahimizwa kutafuta uso wa Mungu. Mstari unaofahamika unasema, "Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao" (2 Mambo ya Nyakati 7:14). Ikiwa hatuwezi kuona uso wa Mungu, tunatafutaje uso wa Mungu?

Neno la Kiebrania "uso" katika Agano la Kale mara nyingi limetafsiriwa kumaanisha "uwepo." Tunapotafuta uso wa Mungu, tunatafuta uwepo wake. Wito wa kutafuta uso wa Mungu ulitolewa kwa watu wake kwa sababu walikuwa wamemwacha Mungu na walihitaji kurudi kwake.

Uso wa mtu hudhihirisha mengi kuhusu tabia na nafsi yake. Tunapata kuona hisia za ndani za mtu kupitia uso wake. Tunatambua mtu kwa kutazama uso wake. Uso wa mtu unawakilisha mtu mzima. Kwa waandishi wa Biblia, uso wa mtu unaweza kuwakilisha mtu mzima.

Katika Zaburi 105:4, waaminifu wa Mungu walihimizwa "kutafuta uso wa Mungu daima." Hata kama hatujamwacha Mungu, kuna wakati ambapo tunapuuza kumtafuta. Uso wa Mungu, tabia Yake Takatifu mara nyingi inadunishwa na hali yetu ya kibinadamu na tamaa za mwili. Ndiyo sababu Bwana anatuhimiza tutafute uso wake daima. Bwana anatamani kuwa rafiki yetu maishani. Yeye anataka sisi tumjue kabisa. Ikiwa tutamkaribia, Mungu pia atatukaribia: "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili" (Yakobo 4:8).

Tunapomwendea Mungu katika maombi, tunatafuta uso wake: "Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo" 24:3-6).

Hali ya kweli ya ibada ni kumtafuta Mungu. Maisha ya Mkristo ni maisha ya kujitolea kutafuta uwepo wa Mungu na kibali chake. Bwana anataka tutafute uso wake kwa unyenyekevu na uaminifu katika maombi na wakati wetu katika Neno lake. Kutafuta uso wa mtu fulani inahitaji uhusiano wa karibu. Kutafuta uso wa Bwana ni sawa na kukuza uhusiano wa karibu naye: "E Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu!" (Zaburi 63:1-3).

Kupata tabasamu kutoka kwa uso wa Mungu ni ishara ya baraka, upendo na kibali: "Mwenyezi Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani" (Hesabu 6:25; Tazama pia Zaburi 80:3, 7, 19).

Tunapomkaribia Mungu, tunabarikiwa na neema yake inayoangaza. Hatumtafuti tu ili kumpa mahitaji yetu kwa sababu tunajua kwamba yeye tayari anajua tunachohitaji (Mathayo 6:7-8, 32-33). Tunaamini kwamba atatutunza.

Kutafuta uso wa Mungu ina maanisha kutamani kujua tabia yake na kumtaka Yeye- uwepo wake- kuliko kitu chochote anachoweza kutupatia.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kutafuta uso wa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries