settings icon
share icon
Swali

Kutazama karama za kiroho-ni karama gani za kiroho ambazo Biblia inataja?

Jibu


Kabla kuchunguza karama za kiroho, tutaangalia maneno mawili ya Kiyunani yanayotumika kuelezea karama za Roho: pneumatika inahusu chanzo, Roho Mtakatifu (pneuma) wa Mungu; na charismata linahusu ukweli kwamba karama zinapeanwa kama kitendo cha neema ya Mungu (charis).Karama za Roho hupeanwa kwa neema na sio kulingana na uthamini wetu au uwezo wa kibinafsi; zinapeanwa kulingana na chaguo kuu la Mungu. Karama zinapeanwa na Roho wa Mungu; kwa hivyo karama ni sehemu ya maisha mapya ambayo tumepewa katika Kristo na yanaweza kuwa tofauti kabisa na uwezo au tamaa zetu za kabla ya wokovu. Wakorintho wa kwanza 12:4-7 inaeleza, "Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana." Waumini watatofautiana katika karama zao za kiroho, lakini karama zote za kiroho zinakusudiwa kutumika kwa kukuza mwili wa Kristo na kwa utukufu wa Mungu.

Kuchunguza kwa ufupi kwa maandishi kuu tatu (Warumi 12:6-8; 1 Wakorintho 12:4-11; 1 Petro 4:10-11) kutasaidia kuona muundo wa Mungu kuhusu karama zake.

Mojawapo ya mambo ya kwanza ambayo ni wazi katika vifungu hivi ni utofauti wa karama. Uchunguzi wa Paulo wa karama za kiroho katika Warumi 12 inajumuisha karama tofauti kuliko ambazo zinapatikana katika 1 Wakorintho 12. Na wakati Petro alizungumza juu ya karama za kiroho katika 1 Petro 4:10-11, yeye hakuzipambanua bali aliorodhesha aina pana za karama ambazo Mungu hupeana. Kati ya karama ambazo zimeorodheshwa katika Bibllia ni unabii, utumishi, hekima, neno la maarifa, imani, kuponya, kufundisha, kushauri, kutoa, kutawala, kuonyesha rehema, kunena kwa lugha, na kutafsiri lugha. Kila karama inashikamana na zingine na zote zinafanya kazi pamoja kama sehemu za mwili ili kutekeleza kazi kamili (Warumi 12:5).

Katika uchunguzi kamili wa karama za kiroho, mtu lazima ajaribu kukadiria na kufafanua karama hizo. Warumi 12 inaorodhesha angalau karama saba, na 1 Wakorintho 12 inaorodhesha tisa. Kuna mwingiliano katika orodha hizi na hakika inaonekana kwamba kuna karama nyingi kuliko ilivyoorodheshwa.

Hapa kuna uchunguzi mfupi wa karama za kiroho kutoka kwa Dk. Larry Gilbert (Uliyorekebishwa kutoka "How Many Spiritual Gifts Are There?"/" Kuna karama ngapi za kiroho"):

1. Karama za kimiujiza
• Utume (1Wokorintho 12:28; Waefeso 4:11)
• Kunena kwa lugha (1 Wakorintho 12:10, 28,30)
• Kutafsiri (1 Wakorintho 12:10,30)
• Miujiza (1 Wakorintho 12:10,28
• Kuponya (1 Wakorintho 12:9,28)

2. Karama za kuwezesha
• Imani (1 Wakorintho 12:9)
• Kubainisha karama (1 Wakorintho 12:10)
• Hekima (1 Wakorintho 12:8)
• Neno la maarifa (1 Wakorintho12:8)

3. Karama za Timu

• Uinjilisti: Kuwaongoza wengine kwa ufahamu wa kuokoa wa kristo (Waefeso 4:11)
• Unabii: Kutangaza ukweli wa Mungu kwa ujasiri, bila kuogopa (Warumi 12:6; Waefeso 4:11; 1 Wakorintho 12:10,28)
• Kufundisha: Kuweka wazi ukweli wa Mungu kwa unyenyekevu na usahihi (Warumi12:7;1 Wakorintho 12:28)
• Kushauri: Kuwahamasisha wengine kupiga hatua, matumizi na kusudi (Warumi 12:8)
• Uchungaji: Kusimamia,kufunza, kulisha, kufundisha/kuongoza (Waefeso 4:11)
• Kutumikia: Kutoa msaada wa kimwili na kiroho ( Warumi 12:7; 1 Wakorintho 12:28)
• Kufariji: kutambua na kufariji wanaohitaji (Warumi 12:8)
• Kutoa: Kutoa rasilimali kwa kuendeleza kazi ya Kanisa (Warumi 12:8)
• Utawala:kuandaa, kusimamia, kukuza na kuongoza (Warumi 12:8; 1 Wakorintho 12:28)

Katika 1 Petro 4:9-11, Petro anatupa vikundi viwili vya karama za Timu

1.Karama za "kuzungumza." Wale walio na vipaji vya kuzungumza ni Wainjilisti, Manabii, Waalimu, Washauri na Wachungaji.

2. Karama za kuhudumia au karama ya kusaidia. Watu ambao wana karama hizi huiga Kristo kwa kuwa hakuja kutumikiwa lakini kutumikia (Marko 10:45). Wamebarikiwa kwa kujisahau hivi kwamba wanazingatia mahitaji ya wengine. Karama za kuhudumia zinajumuisha Wachungaji, Wanaofariji, Watumishi, Wanaotoa na Watawala.

Biblia inasema kwamba tumepewa karama za kiroho kwa kusudi fulani. Katika Warumi 12:8 tunaambiwa tutumie karama mbalimbali kulingana na tabia na mapenzi ya Mungu yaliyowekwa wazi "kwa ukarimu…kwa bidi… kwa furaha." Katika 1 Wakorintho 12:24-25 tunaambiwa kwamba "Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe." Katika 1 Petro 4:11 kusudi la karama ni "ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kutazama karama za kiroho-ni karama gani za kiroho ambazo Biblia inataja?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries