settings icon
share icon
Swali

Wakati tunaungama dhambi zetu kwa Mungu, tunahitaji kuwa na maelezo ya kina kiasi gani?

Jibu


Kuungama dhambi kwa Mungu kumeamrishwa katika Maandiko na ni sehemu ya kuishi maisha ya Kikristo (Yakobo 5:16; 1 John 1:9). Lakini tunapoungama dhambi zetu, tunahitaji kupata maelezo mahususi vipi? Je! tayari Mungu hayajui maelezo hayo yote?

Ni kweli kwamba Mungu anajua maelezo yote ya dhambi zetu. “Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana” (Zaburi 139:3-4). Kwa hakika Mungu anajua mambo yote kutuhusu, ikiwa ni pamoja na kina cha dhambi zetu na yale yote tumetenda. Kwa hivyo wakati tunaungama dhambi zetu Kwake, hatumwambii chochote ambacho Yeye tayari hakijui.

Hata kutokana na uwezo wa Mungu wa kujua mambo yote, ungamo la kina la dhambi kwa Mungu linafaa. Hatutaki kuwa kama Adamu, tukijificha kati ya miti ya bustani, tukitumaini kuwa hatuwezi tambulika (Mwanzo 3:8). Afadhali tuwe kama Daudi aliposema, “Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nilisema, “Nitaungama makosa yangu kwa Bwana.” Ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu” (Zaburi 32:5).

Wakati Mungu alipozungumza na wenzi hao wawili wenye hatia katika Edeni, alimuuliza Adamu, “Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?” (Mwanzo 3:11), na akamuuliza Hawa, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” (aya ya 13). Maswali yote mawili yalihitaji jibu maalum. Ujumla haungetosha. Wala kurahisisha kupita kiasi au mambo ya jumla yanayojitokeza hayapaswi kutosha katika maombi yetu ya kuungama.

Wakati wowote tunapozungumza na Mungu pekee katika sala ya faragha, mawasiliano yanapswa kuwa ya kina nay a ndani. Tunashiriki wenyewe na Mtu ambaye anatujali zaidi kuliko mtu mwingine yeyote anayejali. Tunapoungama dhambi zetu, kwa undani, tunakubali uthamini wetu kwa upana wa msamaha wake. Tunazungumza na Mtu pekee ambaye sio kwamba anajua mapambano yetu tu ya maisha, kushindwa na nia, bali ambaye ana uwezo wa kiungu wa kutubadalisha kuwa zaidi kama Yeye.

Tunapokiri undani wa dhambi zetu kwa Mungu, tunamwonyesha kwamba hatuna cha kuficha. Tunakubali kwa unyenyekevu kwamba “Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu” (Waebrania 4:13). Katika maungamo yetu tunamtazama Yeye pekee aliye na uwezo wa kutusamehe kabisa dhambi zetu na kutufanya kuwa wakamilifu wenye kukubalika mbele zake.

Tunahitaji kuogopa hukumu ya Mungu. Tunapoungama dhambi zetu, tunajua kwamba Kristo tayari amelipa kwa ukamilifu. Anaahidi msamaha Wake na uwezo wa kuvunja udhibiti wa dhambi juu yetu. Kukiri ukina wa dhambi zetu kwa Mungu ni sehemu ya tuweke “kando kila kitu kinachotuzuia na ile dhambi inayotuzinga kwa urahisi” ili tuweze, “kupiga mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa kwa ajili yetu” (Waebrania 12:1).

Katika kikao cha ushauri, mshauri atatarajia mshauriwa wake kuwa wazi na mwaminifu iwezekanavyo ili kuwezesha mchakato wa uponyaji. Ukosefu wa uaminifu utazuia mchakato. Yesu Mshari wa Ajabu (Isaya 9:6), anastahili uaminifu na uwazi. Amesimama tayari kusikiliza na kuongoza. Fauka ya yote Bwana wtu alifanyika “afanane na ndugu zake kwa kila hali, ili apate kuwa Kuhani Mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika kumtumikia Mungu, ili pia apate kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu. Kwa kuwa yeye mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wale wanaojaribiwa” (Waebrania 2:17-18).

Badala ya kusali kikawaida, tukisema mambo kama vile, “Ikiwa lilifanya dhambi leo, tafadhali nisamehe,” tunapaswa kujihusisha na kutaftufa nafsi ya kweli na kufahamu yale ambayo tumefanya. Maombi ya mtu binafsi hayatoki katika ungamo la dhambi la kina. Moyo wenye kujuta, wenye toba hautaogopa kifichua dhambi yake kwa Mungu: “Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau” (Zaburi 51:17). Na tunakumbuka kwamba “Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho” (Zaburi 34:18).

Tunaweza kumwendea Mungu tukiwa na kila kitu ambacho kiko akilini mwetu, tukiungama dhambi zetu kwa uaminifu, na kisha kujua uwezo wa kuweka huru wa wa msamaha Wake. Baada ya kupatana na Mungu, tutapata pumziko kutokana na hisia ya hatia na kuimarisha mwendo wetu kama waumini katika Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wakati tunaungama dhambi zetu kwa Mungu, tunahitaji kuwa na maelezo ya kina kiasi gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries