settings icon
share icon
Swali

Siri ni gani ya kutumia Biblia katika maisha yangu?

Jibu


Kuitumia Biblia ni wajibu wa Wakristo wote. Ikiwa hatutumii, Biblia haitakuwa kitu kingine zaidi kuliko kuwa kitabu cha kawaida, mkusanyiko usiowezekana wa maandishi ya kale. Ndiyo sababu Paulo anasema, "Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutok kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia Amani atakuwa pamoja nanyi" (Wafilipi 4: 9). Tunapoitumia Biblia, Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nasi.

Hatua ya kwanza ya kutumia Neno la Mungu katika maisha yetu ni kulisoma neno. Lengo letu la kusoma ni kumjua Mungu, kujifunza njia zake, na kuelewa kusudi lake kwa ulimwengu huu na pia lengo lake kwetu. Katika kusoma Biblia, tunajifunza juu ya ushirikiano wa Mungu na ubinadamu katika historia, mpango wake wa ukombozi, ahadi zake, na tabia yake. Tunaona ni namna gani maisha ya Kikristo inaonekana. Ujuzi wa Mungu tunaokusanya kutoka kwenye Maandiko hutumika kama msingi muhimu sana wa kutumia kanuni za Biblia maishani.

Lengo letu linalofuata ni kile ambacho mtunga-zaburi anasema kama "kujificha" Neno la Mungu ndani ya mioyo yetu: "Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea" (Zaburi 119: 11). Njia tunayo "ficha "Neno la Mungu ndani ya mioyo yetu ni kwa kusoma, kukariri, na kutafakari juu ya kile tulichosoma kwanza. Hatua hizi nne-kusoma, kujifunza, kukariri, na kutafakari-huifanya kuwezekana kuyatumia Maandiko kwa ufanisi katika maisha yetu.

Kujifunza: Wakati kujifunza inahusisha kusoma, kusoma si sawa na kujifunza. Kujifunza Neno la Mungu inamaanisha kuwa tunajitolea katika maombi na mawazo yetu ili kupata kuendelea katika ujuzi wa juu juu ya mtu fulani, somo, mandhari, kifungu au kitabu cha Biblia. Mengi ya rasilimali za utafiti zinapatikana, ikiwa ni pamoja na maoni ya kibiblia na masomo ya Biblia iliyochapishwa ambayo inaweza kutuwezesha kula "nyama" ya Neno la Mungu (Waebrania 5: 12-14). Tunaweza kujitambulisha na rasilimali hizi, kisha kuchagua mada, kifungu, au kitabu ambacho kinachuguza maslahi yetu na kukizingatia.

Kariri: Haiwezekani kutumia kile ambacho hatuwezi kukumbuka. Ikiwa tunataka "kuficha" Neno ndani ya mioyo yetu, tunapaswa kulipata kwanza kwa njia ya kukariri. Kukumbuka Maandiko hutoa ndani yetu kisima ambacho tunaweza kuendelea kunywa, hasa wakati ambapo hatuwezi kusoma Biblia zetu. Kwa njia ile ile tunayoweka fedha na vitu vingine vya kidunia kwa matumizi ya baadaye, tunapaswa "Yawekeni maneno yangu haya mioyoni mwenu na rohoni mwenu" (Kumbukumbu la Torati 11:18, KJV). Unda mpango wa mistari ya Maandiko ungependa kukariri kila wiki.

Waza: Mwandishi na mwanafalsafa Edmund Burke wakati moja alisema, "Kusoma bila kutafakari ni kama kula bila kuchimba." Hatuwezi kumudu "kulila" Neno la Mungu bila "kulichimbua" neno hilo. Katika mfano wa dongo nne (Mathayo 13: 3-9, tazama 18-23), Yesu anasema juu ya mkulima ambaye alienda kupanda mbegu katika shamba lake,na kupata kwambwa baadhi ya mbegu — Neno la Mungu (Mathayo 13:19) — zilikuwa zimeanguka juu ya "penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina. Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka" (13: 5-6). Hii, Yesu anasema, ni mtu ambaye Neno hupandwa lakini hachukui mizizi (13: 20-21).

Zaburi 1: 2 inasema kwamba mtu anayetafakari juu ya Neno la Mungu amebarikiwa. Donald S. Whitney, katika kitabu chake cha Mafundisho ya kiroho kwa ajili ya Maisha ya Kikristo, anaandika, "Mti wa maisha yako ya kiroho hufurahia sana kutafakari kwa sababu inakusaidia kunyonya maji ya Neno la Mungu (Waefeso 5:26). Kwa kusikia tu au kusoma Biblia, kwa mfano, inaweza kuwa kama mvua ndogo juu ya udongo mgumu. Bila kujali kiasi au ukubwa wa mvua, wengi hutoraka ile hali wachache wanazama ndani. Kutafakari hufungua udongo wa nafsi na kuruhusu maji ya Neno la Mungu kupenya undani. Matokeo yake ni matunda ya ajabu na mafanikio ya kiroho" (kurasa, 49-50).

Ikiwa tunatamani Neno lichukue "mizizi" katika maisha yetu ili tuweze kuzalisha mavuno yanayompendeza Mungu (Mathayo 13:23), tunapaswa kuangaziaa, kujimulika, na kutafakari juu ya kile tunachosoma na kujifunza katika Biblia. Tunapotafakari, tunaweza kujiuliza maswali fulani:
1. Kifungu hiki kinanifundisha nini kuhusu Mungu?
2. Kifungu hiki kinafundisha nini kuhusu kanisa?
3. Kifungu hiki kinanifundisha nini kuhusu ulimwengu?
4. Kifungu hiki kinanifundisha nini kunihusu? Kuhusu tamaa zangu na nia zangu?
5. Je, fungu hili linahitaji kwamba nifanye hatua? Ikiwa ndivyo, ni lazima nichukue hatua gani?
6. Ni nini ninahitaji kukiri na / au kutubu?
7. Nimejifunza nini kutoka kwenye kifungu hiki ambacho kitanisaidia kuzingatia Mungu na kujitahidi kufikia utukufu wake?

Kutenda: Kiwango tunachojifunza, kukariri, na kutafakari juu ya Neno la Mungu ni kiwango ambacho sisi tunaelewa jinsi kinavyotumika kwa maisha yetu. Lakini kuelewa jinsi Neno linavyotumika haitoshi; lazima tuliweke katakia matendo (Yakobo 1:22). "Kuliweka katika matendo" inamaanisha hatua, na hatua ya utii ndio hatua ya mwisho ya kusababisha Neno la Mungu liwe hai katika maisha yetu. Matumizi ya Maandiko yanasisitiza zaidi na huongeza mwanga wetu, na pia inatusaidia kuimarisha ufahamu wetu, hutusaidia kuelewa vizuri kati ya mema na mabaya (Waebrania 5:14).

Kama neno la mwisho, ni muhimu kutambua kwamba hatujaribu pekee kuelewa na kulitumia Neno la Mungu katika maisha yetu. Mungu ametujaza na Roho Wake (Yohana 14: 16-17) ambaye anaongea na sisi, akiongoza na kutuongoza katika ukweli wote (Yohana 16:13). Kwa sababu hii, Paulo anawaonya waumini "kutembea katika Roho" (Wagalatia 5:16), kwa kuwa Yeye ni Msaada wetu wakati wa mahitaji (Zaburi 46: 1)! Roho atatuongoza kwa uaminifu katika mapenzi ya Mungu, daima hutufanya kufanya haki (Ezekieli 36: 26-28; Wafilipi 2:13). Ni nani aliye bora kutufundisha jinsi ya kuishi kulingana na yote yaliyoandikwa katika Biblia kuliko Yule ambaye aliongoza uandishi wa Biblia, kwa kwanzia — Roho Mtakatifu mwenyewe? Kwa hiyo, hebu tufanye sehemu yetu kwa kuliweka Neno ndani ya mioyo yetu na kumtii Roho Mtakatifu anavyo lidhihirisha Neno hilo kutoka ndani mwetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Siri ni gani ya kutumia Biblia katika maisha yangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries