Swali
Naeza kuwa mhubiri aje? Naeza kuwa mtumwa aje?
Jibu
Kuna madhehebu mingi ambayo yanahitaji mafunzo maalum na vyeti ili kuwa mhubiri. Hapa mhubiri hufanyia madhehebu hayo kazi na kupeana ripoti moja kwa moja kwao. Makanisa mengine huwa yamejitegemea na huchagua mhubiri kulingana na mawaidha ya umati ama baraza fulani la uongozi katika kanisa. Hapa kenye inahitajika huwa inaangaziwa na baraza ambalo lina jukumu la kumchagua mhubiri. Makala haya yataangazia maelezo ya Biblia na matendo ambayo yanaruhusu mmoja kuwa mhubiri, pia yanatambua kuwa makanisa fulani au madhehebu huwa na mahitaji zaidi. Makala haya pia yanaelezea kuwa yule ambaye anataka kuwa mhubiri ni mtu ambaye ako na uaminifu kwa Kristo na imani yake inakua kwa maisha ya kiroho kila siku. Kuwa mtumwa wa kila wakati si kazi ya kuchagua kulingana na masharti, malipo ama usalama wa kazi yenyewe. Kuwa mhubiri wa Biblia ama mtumwa inahitaji kumtegemea Bwana na kujali maslahi ya wengine. Ikifanywa jinsi inafaa, kuhubiri inahitaji vitu mingi na ina gharama lakini pia iko na manufaa yanayotimizwa.
Apo awali na ata sai kumekua na msisitizo kwa 'wito' yenye ina maana kuwa mtu kuwa mhubiri lazima akue na wito maalum kutoka kwa Mungu, kwa kiwango fulani hii ni ukweli. Hata hivyo, si lazima mtu akue na mafunzo maalum ili apate wito wa kuhubiri. Ikiwa mtu anataka kuwa mhubiri inafaa afuate iyo njia: "Neno hili ni kweli, kwamba mtu akitaka kuwa askofu, anatamani kazi njema"( 1Timotheo 3:1). Mwenye anataka kuwa mhubiri amehimizwa kuwa uhubiri ni kazi njema, na atapata usaidizi kutoka kwa wale ambao atakua anahubiria, na ikiwa Mungu ako ndani atafungua milango kwa shirika ilo. Hata hivyo, bidii ya mtu kuchagua kazi hii inafaa ikue ni utukufu wa Mungu na mema ya watu wengine. Mtu yeyote anayechagua utumwa kwa ajili ya pesa, uongozi,ushawishi ama ufahari/starehe ni vitu za uovu.
Hizi ni baadhi ya hatua za matendo unafaa kufuata ili kuwa mhubiri ama mtumwa:
1. Tumia manufaa ya shirika penye uko: Neno mhubiri lina mizizi yake kwa wazo kuwa ni kazi ya kuchunga kondoo wa Mungu, ambayo inahusisha kuwalisha chakula ya kiroho na kulinda imani yao jinsi mchungaji hulinda na kuwalisha kondoo wake. Neno 'mtumwa/waziri' lina mizizi yake kwa wazo la kuwahudumia ama kushughulikia mahitaji ya waumini. Kwa jumla, kila muumini anfaa kuwa mhubiri ama mtumwa wa wengine nyumbani, shuleni, kazini, na kanisani. Kuhudumia wale wanaotukosea kila siku kwenye maisha yetu ya kawaida ni mafunzo bora ya kuwa mtumwa mkamilifu. Kila mtumwa ama mhubiri anafaa kutumia fursa ama manufaa ya shirika ambalo anatumikia kabla ya kutamani manufaa mengine.
2. Jihusishe kikamilifu na maisha kulingana na Biblia ya kanisa: Kanisa mingi huwa na mahitaji mingi ambazo zinafaa kufanywa na watu wengi ambao hawajatimiza mahitaji hayo. Kujitolea kwa kanisa ni njia bora ya mtu kugundua ama kujua kenye anafanya kwa ubora,na talanta yake, na kile anafurahia kufanya. Pia inamsaidia mhubiri anayetarajiwa fursa mingi za mafunzo akiwa kazini. Yeyote anayetaka kuwa mhubiri wa kila wakati anafaa akue na historia ya kujitolea ama kufanya kazi kwenye kanisa wakati wa mapumziko. Uzoefu na uwajibikaji ambao huletwa na huduma hii haina thamani.
3. Kuwa mwanafunzi wa neno la Mungu: Kila Mkristo anafaa awe mwanafunzi wa neno la Mungu, lakini kama mhubiri , kufunza na kuhubiri neno la Mungu ( ata ikiwa ni kwa umati mkubwa, darasa la wanafunzi wachache ama kwa mafunzo ya kusoma Biblia ama kati ya mtu mmoja) ni kipaumbele cha kwanza (soma 2Timotheo 4:2). Kwa hivyo lazima mhubiri awe na ujuzi wa neno la Mungu.
Daktari wa ubongo wa binadamu lazima aelewe ubongo na awe na ujuzi wake nje na ndani. Wakiri lazima asome kwa miaka mingi na apite mtihani kabla ya kuruhusiwa kushiriki kwenye sheria. Fundi wa umeme lazima apate mafunzo kutoka kwa fundi mkuu wa umeme kwa muda mrefu kabla ya kuruhusiwa kufanya kazi peke yake. Kwa hizi tajriba zote, maisha, usalama na uhuru wa mtu uko taabani. Mhuburi anashughulikia kitu ambacho ni muhimu zaidi kuliko fani hizi- yani roho takatifu milele! Mhubiri lazima ajue na kuelewa yaliyomo kwenye Biblia. Anafaa akue na uwezo wa kutumia mafunzo ya Biblia na kupeana ujumbe wa ukweli kuhusu Mungu kwa njia inayofaa.
Katika mataifa mengi, wale ambao hutaka kuwa wahubiri hawananga fursa ya kupata elimu ya kawaida. Hata hivyo, kwa mataifa mengine shule za kibiblia na seminari ni tele, zinazopeana mafunzo ya kibiblia na jinsi ya kuwa mchungaji na yeyote anayetaka kuwa mtumwa anafaa kuingia kwa masomo kama hayo. Matayarisho yanafaa kuwa kusoma Biblia na kufanya uchunguzi wake pamoja na kujifunza vipengele vya utendaji kama uongozi katika kanisa .
Mara nyingi roho hupewa kipaumbele kuliko elimu ya kawaida, na hii ni makosa. Kuna mhubiri maarufu alisema kwamba ukisoma neno la Mungu sana, roho itaendelea kufanya kazi kwa shirika lako maradufu. Elimu haifai kupewa kipaumbele kushinda roho, na roho haifai kupewa kipaumbele kuliko elimu. Zote kwa umoja ni muhimu.
Mwanafunzi anaposhughulika na kujiandaa kwa ajili ya huduma,hafai kusahau hatua za 1 na 2 apo juu.
4. Timiza mahitaji ya kibiblia: Timotheo ya kwanza 3:1-7 na Tito 1:5-8 zinaelezea mahitaji ya kikiblia ambayo mhubiri anafaa kuwa nayo ( pia wanaitwa wazee ama askofu ). Mahitaji haya yanasisitiza juu ya ukomavu wa kiroho na jinsi hekima inashughulikia watu kwa kudhibiti tabia ya mtu. Mahitaji moja kuu ni kuwa wahubiri/wazee/askofu lazima wawe wanaume na si wanawake. Ingawa kuna huduma mingi ambazo wanawake wana fursa ya kuongoza kama vile huduma ya watoto na ile ya wanawake, pia kuna nafasi zingine muhimu wanawake wanaeza ongoza katika huduma zingine za kikristo.
Ikiwa mtu ambaye anatamani kuwa mhubiri ama mtumwa anajitayarisha kwa kusoma neno kwa bidii, basi kibiblia amefaulu na kukua kiroho na anachukua fursa zote ambazo ziko kupitia kanisa basi manufaa itakuja katika huduma yake. Kwa mfano manufaa haya yanaeza tokea kwa njia ya kupata kazi kanisani ili kujaza nafasi iliyo bure na itapelekea kupewa majuku maalum katika huduma.
English
Naeza kuwa mhubiri aje? Naeza kuwa mtumwa aje?