Swali
Kwa nini tuombe? Kuna haja gani ya kuomba wakati Mungu anajua kesho na bado ni yeye anatawala. Ikiwa hatutaweza badilisha mawazo ya Mungu kwa nini tuombe?
Jibu
Kwa Mkristo, maombi ni kama kupumua. Ni rahisi kufanya kuliko kutofanya. Tunaomba kwa ajili ya sababu mbalimbali. Kwa sababu moja maombi ni njia ya kumtumikia Mungu (Luka 2:36-38) na kumtii. Tunaomba kwa sababu Mungu anatuamuru kuomba (Wafilipi 4:6-7). Maombi yamedhihirishwa kwetu na Yesu pamoja na kanisa la kwanza (Mariko 1:35; Matendo Ya Mitume 1: 14; 3:1; 4: 23-31; 6:4; 13:1-3). Kama Yesu aliehesabu kuwa maombi ni kitu cha maana, pia nasi lazima. Kama aliitajika kuomba ili asalie katika mapenzi ya Baba yake, je tunahitajika kuomba kiazi gani?
Sababu nyingine ya kuomba ni kuwa Mungu anataka maombi yawe njia kupata suluhisho lake kwa hali zetu. Tunaomba tukijiandaa kufanya maamuzi muimu (Luka 6:12-13); ilitushinde vizuizi vya shetani (Mathayo 17:14-21); kukusanya wafanyi kazi kwa sababu ya mavuno ya kiroho (Luka 10: 2); kupata nguvu ili tuyashinde majaribu (Mathayo 26:41); na kupata njia ya kuwatia wengine nguvu kiroho (Waefeso 6:18-19).
Tunakuja kwa Mungu katika mahitaji yetu kamili, na tuko na ahadi ya Mungu kwamba maombi yetu si ya bure, hata kama hatupati chenye tunauliza (Mathayo 6:6; Warumi 8:26-27). Ameahidi kuwa tunapouliza vitu ambavyo viko katika mapenzi yake, atatupa chochote tuitizacho (1 Yohana 5: 14-15). Wakati mwingine anakawisha majibu yake kulingana na hekima yake kwa manufaa yetu. Katika hali hii tunastahili kuwa makini na kudumu katika maombi (Mathayo 7:7; Luka 18:1-8). Maombi yasionekane kama njia zetu za kumfanya Mungu kutenda mapenzi yetu duniani, bali iwe ni njia ya Mungu kutenda mapenzi yake duniani. Hekima ya Mungu inapita hekima yetu.
Kwa hali ambazo hatuwezi jua mapenzi ya Mungu kamili, maombi ni njia ya kutambua mapenzi yake. Ikiwa mwanamke Myunani aliyekuwa na binti aliyepagagwa na mapepo angeponywa (Mariko 7:26-30). Ikiwa kibofu nche ya Yeriko angemwita Kristo kwa sauti, angebaki kibofu (Luka 18: 35-43). Mungu amesema kuwa kila mara tunaenda bila kwa sababu hatuulizi (Yakobo 4:2). Kwa njia nyingine maombi ni kama kushiriki injili na watu. Hatujui ni nani ataitikia ujumbe wa injili hadi pale tunapoishiriki. Kwa njia hiyo hiyo, hatuwezi kuyaona matunda ya maombi yakijibiwa hadi tuombe.
Ukusefu wa maombi yaonyesha ukosefu wa imani na ukosefu wa imani katika neno la Mungu. Tunaomba ili tuonyeshe imani yetu kwa Mungu, kuwa atatenda vile ameahidi katika neno lake na kubariki maisha yetu utele zaidi ya vile tumeuliza na kutumainia (Waefeso 3:20). Maombi ni njia ya kuona kazi ya Mungu katika maisha ya wengine. Kwa sababu ni njia yetu ya “kujitupa ndani” ya nguvu za Mungu, ni njia yetu ya kumshinda shetani na jeshi lake ambalo hatuna nguvu za kulishinda sisi wenyewe. Kwa hivyo Mungu anatupata kila mara mbele ya kiti chake cha enzi, kwa vile tuko nakuani mkuu mbinguni anayeweza jua yote amboyo tunayapitia (Waebrania 4:15-16). Tuko na ahadi yake kuwa maombi ya mwenye haki yatatenda mengi (Yakobo 5:16-18). Na Mungu atukuze jina lake katika maisha yetu tunapomwamini na kukuja kwake kila mara katika maombi.
English
Kwa nini tuombe? Kuna haja gani ya kuomba wakati Mungu anajua kesho na bado ni yeye anatawala. Ikiwa hatutaweza badilisha mawazo ya Mungu kwa nini tuombe?