settings icon
share icon
Swali

Kwa nini napaswa kumwamini Mungu?

Jibu


Imani katika Mungu ni msingi wa mambo yote ya kibinadamu. Kumshukuru Muumba ni msingi wa kujifunza zaidi kuhusu Muumba mweyewe. Bila kumwamini Mungu, haiwezekani kumpendeza au hata kuja kwake (Waebrania 11: 6). Watu wamezungukwa na ushahidi wa kuwepo kwa Mungu, na ni kwa njia ya ugumu wa dhambi ambayo hufanya wanadamu kukataa uthibitisho huo (Warumi 1: 18-23). Ni upumbavu kukataa kumwamini Mungu (Zaburi 14: 1).

Kuna chaguo mbili katika maisha. Kwanza, tuna chaguo la kuamini fikra ndogo za mwanadamu. Kanuni za mwanadamu zimetoa falsafa mbalimbali, dini nyingi duniani na "fomu," ibada tofauti, na mawazo mengine na maoni kuhusu ulimwengu. Hoja za mwanadamu kwa kawaida hazidumu. Pia zina upungufu,kufuatia akili za mtu amabazo zina mwisho; sisi sio wenye busara kama tunavyofikiri (1 Wakorintho 1:20). Fikra ya mwanadamu huanza na yeye mwenyewe na kuishia kwake mwenyewe. Mtu huishi katika sanduku la wakati bila na kwa hivyo hawezi toka. Mtu anazaliwa, hukua hadi kukomaa, hufanya athari yake duniani, na hatimaye hufa. Hiyo tu ndiyo Maisha yake kwa kawaida. Chaguo la kuishi kutegemea kanuni za bidanamu juacha mtu kwa njia panda. Ikiwa mtu anafikiria kwa njia ya maisha kama hiyo, inapaswa kumfanya azingatie chaguo la pili.

Chaguo la pili tunayo ni kukubali ufunuo wa Mungu katika Biblia. Ili "... usitegemee akili zako mwenyewe" (Methali 3: 5). Bila shaka, kukubali kwamba Biblia ni kutoka kwa Mungu, mtu lazima akiri Mungu. Imani katika Mungu wa Biblia haimaanishi kuacha kutumia akili; badala yake, ni wakati tunamtafuta Mungu kwamba Anufungua macho yetu (Zaburi 119: 18), huangaza njia zetu (Waefeso 1:18), na kutupa hekima (Mithali 8).

Imani katika Mungu imethibitishwa na ushahidi wa uwepo wa Mungu ambao unapatikana kwa urahisi. Viumbe vyote vinatoa ushahidi juu ya ukweli wa Muumba (Zaburi 19: 1-4). Kitabu cha Mungu, Biblia, kinaweka uhalali wake mwenyewe na usahihi wa kihistoria. Kwa mfano, fikiria unabii wa Agano la Kale kuhusu kuja kwa Kristo kwa kwanza. Mika 5: 2 inasema kwamba Kristo angezaliwa Bethlehemu ya Yudea. Mika alitoa unabii wake karibu 700 BC. Kristo alizaliwa wapi karne saba baadaye? Alizaliwa Bethlehemu ya Yudea, kama Mika alivyotabiri (Luka 2: 1-20; Mathayo 2: 1-12).

Peter Stoner, katika kitabu Science Speaks (uk. 100-107), ameonyesha kuwa jambo la nasibu katika Maandiko ya unabii haiwezekani katika sayansi ya uwezekano. Kwa kutumia sheria za uwezekano katika kutaja unabii nane kuhusu Kristo, Stoner aligundua kuwa nafasi ya mtu yeyote ya kutimiza unabii wote nane ni 1 kati ya 10 hadi mara 17. Hiyo itakuwa nafasi 1 katika 100,000,000,000,000,000. Na hiyo inazingatia tu unabii nane; Yesu alitimiza zaidi ya hayo. Hakuna shaka kwamba usahihi na uaminifu wa Biblia huthibitishwa na unabii.

Tunaposoma Biblia, tunaona kwamba Mungu ni wa milele, mtakatifu, binafsi, mwenye neema, na upendo. Mungu amefungua wazi sanduku la wakati kwa njia ya kufanyika mtu halisi kwa Mwanawe, Bwana Yesu Kristo. Hatua ya upendo ya Mungu haiadhiri akili za mwanadamu lakini hutoa mwanga kwa akili za mwanadamu ili aweze kuanza kuelewa kwamba anahitaji msamaha na uzima wa milele kupitia Mwana wa Mungu.

Hakika, mtu anaweza kumkataa Mungu wa Biblia, na wengi hufanya hivyo. Mwanadamu anaweza kukataa kile Yesu Kristo amemfanyia. Kumkataa Kristo ni kukataa Mungu (Yohana 10:30). Je, itakuwaje kwako? Je! Utaishi kwa kutegema akili pungufu za binadamu? Au utakubali Muumba wako na kukubali ufunuo wa Mungu katika Biblia? " Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. "(Mithali 3: 7-8).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini napaswa kumwamini Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries