settings icon
share icon
Swali

Kwenda mbingu- Ninawezaje kuwa na uhakika wa hatima ya maisha yangu ya milele?

Jibu


Kabiliana nalo. Ile siku ambayo kila mmoja wetu ataingia uzima wa milele inaweza kuwa hivi karibuni kinyume na matarajio yetu. Kwa kujitayarisha kwa ajili ya wakati huo, tunahitaji kuujua ukweli huu-sio kila mtu anaenda mbinguni. Tunawezaje kujua kwa akika kwamba tuko katika kile kikundi cha wale watakao kaa mbinguni milele yote? Miaka 2,000 iliyopita, mtume Petero na Yohana walikuwa wakihubiri injili ya Yesu Kristo kwa umati mkubwa Yerusalem. Ulikuwa wakati huo Petero aliitoa habari ambayo inaweza kutumika hata inaweza kutumika ulimwengu baada yetu: “Wala hakuna wokovu katika jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo ya Mitume 4:12).

Kama vile ilivyo kuwa wakati huo, pia hii leo “njia zote zaelekeza mbinguni” hali ya anga huu sio ujumbe wa kisiasa ulio kweli. Kunao wengi wanaodhani wanaweza kuingia mbinguni bila kumpokea Yesu. Wanata ahadi nzuri ya utukufu, lakini hawataki kushughulika na msalaba, na hata yule aliyeangikwa kwa ajili ya dhambi za wale wote wamwaminio. Wengi hawataki kumkubali Bwana Yesu kama njia pekee na wametia bidii kutafuta njia mpadala. Lakini Yesu mwenyewe anatuonya ya kuwa hakuna njia nyingine na madhara ya kutokubali hii njia ya kweli ni jahannam ya milele. Ametueleza wazi wazi kuwa “ Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima,bali ghadhabu ya Mungu inamkalia” (Yohana 3:36)

Wengine watapinga kuwa Mungu alikuwa na mawazo finyu kwa kutoa njia moja pekee ya kwenda mbinguni. Lakini kwa ukweli, kwa mtazamo wa uazi wa mwanadamu wa kumkataa Mungu, kuna upana wa mawazo wa Mungu kupeana njia nyingine ya kwelekea mbinguni. Tunastahili hukumu, badala yake anatupa njia ya kuepuka kwa kumtuma Mwanawe wa pekee kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Hata kama mtu ataiona dhana hii kuwa finyu au pana, huu ndio ukweli na Wakristo wanastahili kuifanya njia iwe wazi, ujumbe usiobadilishwa ya kuwa njia pekee ya kwenda mbinguni ni kupitia Yesu Kristo.

Watu wengi siku hizi wameamini injili iliyotiliwa chumvi ambayo yatupilia mbali ujumbe wa toba wa dhambi zao. Wanataka kumwamini Mungu mwenye upendo lakini haukumu ambaye haitaji toba na hakuna ubadilisho katika nama wanavyoishi. Wanaweza sema vitu kama, “Ninaamini katika Kristo Yesu, lakini Mungu wangu si wa hukumu. Mungu wangu kamwe hawezi kumtuma mtu jahannam.” Lakini hatuwezi kuwa na njia zote mbili. Kama tunadai sisi ni Wakristo, lazima tumtambue vile alivyo and vile alivyo sema ako- njia pekee ya kwenda mbingu. Kukataa hili ni kumkataa Yesu mwenyewe, kwa maana ni yeye alisema, “Mimi ndimi njia, nakweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mini” (Yohana 14:6).

Swali bado labaki: Ni nani kwa kweli ataingia katika ufalme wa Mungu? Ninawezaje kuwa na uhakika kuhusu hatima yangu ya milele? Jibu kwa maswali haya linaweza tolewa katika elezo la tafauti kati ya wale wako na uzima wa milele na wale hawana. “Yeye aliye na Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima” (1Yohana 5:12). Wale wamwaminio Kristo, wenye wamekubali dhabihu yake kwa kulipa fidia ya dhambi, na wanye wanamfuata katiak kutii watakaa milele naye Mbinguni. Wale watakao mkataa kamwe hawatarithi uzima. “Amwaminiye hahukumiwe; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana Pekee wa Mungu” (Yohana 3:18).

Vile mbingu itakuwa ya ajabu kwa wale wote watakao mchagua Yesu Kristo kama mwokozi, jahannam itakuwa ya kustaajabisha kwa wale wote waliomkataa Yeye. Ujumbe wetu kwa wapoteao utawazilishwa kwa uepesi kama tutaelewa ni nini utukufu na utakatifu Mungu utawafanyia wale wote ambao wameasi msamaha uliopeanwa katika Mwanawe, Yesu Kristo. Mtu hawezi kuisoma Biblia tena na tena kwa bidii bila kuona hiyo – mustari umewekwa. Biblia iko peupe kuwa kuna njia moja pekee ya kwenda mbinguni- kupitia kwa Yesu Kristo. Ametupa onyo hili: “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao walonalo ni wachache” (Mathayo 7:13-14).

Kuna njia moja iendayo mbinguni na wale waifuatayo wameakikishiwa kufika huko. Lakini sio kila mtu anaifuata hiyo njia. Je! Waifuata?

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwenda mbingu- Ninawezaje kuwa na uhakika wa hatima ya maisha yangu ya milele?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries