settings icon
share icon
Swali

Je! Lusifa ni Shetani? Je, kuanguka kwa Ibilisi kunamwelezea Shetani?

Jibu


Hakuna mstari katika Biblia ambayo unasema, "Lusifa ni Shetani," lakini uchunguzi wa vifungu kadhaa unaonyesha kuwa Lusifa hawezi kuwa mwingine isipokuwa Shetani. Kuanguka kwa Lusifa ilivyoelezwa katika Isaya 14:12 kuna uwezekano sawa na ule Yesu aliyomtaja katika Luka 10:18: " Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme." Kuanguka sawia kunaonyeshwa katika Ezekieli 28.

Isaya 14: 12-18 inaelezea kuanguka kutoka mbinguni kwa mmoja aitwaye "Lusifa," jina linamaanisha "nyota ya asubuhi," "mwana wa asubuhi," "Nyota ya Siku," au "nyota inayoangaza". inajulikana inaonyesha kwamba inaweza kuwa hakuna mwingine isipokuwa Shetani. Tunajua kutoka kwa maneno ya Yesu mwenyewe katika Luka 10 kwamba Shetani alianguka kutoka mbinguni. Kwa hiyo, Isaya akielezea Lusifa (Kwa Kiebrania, helel) akatupwa duniani (Isaya 14:12), hawezi kuwa mwingine isipokuwa Shetani. Sababu ya kuanguka kwake inapatikana katika mstari wa 13 na 14: "Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.'" Hii imekuwa daima tamaa ya Shetani-kuwa Mungu-na ndilo jaribio alilitumia katika bustani mwa Edeni ili kumfanya Hawa amwasi Mungu: "Mtafanana na Mungu" ( Mwanzo 3: 5).

Ezekieli 28 ni kifungu kingine kinachofikiriwa kuelezea Lusifa / Shetani. Ingawa huanza na Ezekieli akiagizwa na Mungu " umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro" (mstari wa 12), mfalme mwovu na mwabudu sanamu, punde ikawa dhahiri kuwa kifungu hiki kinamaanisha pia nguvu ya mfalme huyo- Shetani. Mstari wa 13 unasema alikuwa "katika Edeni, bustani ya Mungu." Kwa wazi, mfalme wa Tiro hakuwahi ishi huko Edeni. Mstari wa 14 unasema, "Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye." Inaonekana, Lusifa / Shetani alikuwa na nafasi ya upawabu mbinguni "miongoni mwa mawe ya moto," yaliyofikiriwa kuwa vyombo vya thamani vinavyoonekana katika maelezo mengine ya mbinguni (Kutoka 24:10; Ufunuo 21: 18-21). Kwa kuwa mfalme wa Tiro hakuwapo mbinguni, ama, hii inaweza tu kuelezea Lusifa. Sehemu zote zinaelezea sababu kutupwa nje kutoka mbinguni. Kwa sababu ya uzuri wake, moyo wake ukajivunia na hekima yake iliharibiwa (Ezekieli 28:17). Uburi katika ukamilifu wake, hekima, na uzuri (mstari wa 12) ulikuwa chanzo cha kuanguka kwake, na Mungu akamtupa duniani (mstari wa 17). Hii ilishuhudiwa na Bwana Yesu mbinguni kabla ya ubadilisho wake (Luka 10:18).

Kwa muhtasari, Lusifa alitupwa mbinguni kwa ajili ya dhambi yake ya kiburi na hamu yake ya kutaka kuwa Mungu. Yesu alitaja kumwona Shetani akitupwa mbinguni. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba Lusifa na Shetani ni kutu kimoja.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Lusifa ni Shetani? Je, kuanguka kwa Ibilisi kunamwelezea Shetani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries