settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inafundisha maadili ya hali?

Jibu


Maadili ya hali ni mtazamo fulani wa maadili ambayo inasisitiza kwamba maadili ya kitendo hutegemea na muktadha wake. Maadili ya hali inasema kwamba ikiwa kuna jambo zuri au mbaya, inategemea matokeo yaliyohitajika ya hali hiyo. Maadili ya hali inatofauti na kanuni kwamba busara, kweli na utamaduni haziwezi ishi bila desturi/tamaduni (ile hali ya kubadilika) kwamba maadiliya ya uhusianaji inasema kwamba hakuna jambo la haki au mbaya. Maadili ya hali ya mazingira inaleta kanuni za maadili ambayo kukidhi mahitaji ya kila hali huamua kile kilicho sawa au kibaya.

Kutoka mwanzo wa Biblia hadi mwisho wake, Biblia unaangazia ukweli nani thabiti, na inaweza kutumika. Je, Biblia inafundisha, kuonya, au hata kuimarisha kuelezea maadili ya hali? Jibu fupi ni "hapana." Hebu tuzingalie kanuni tatu: 1) Mungu ndiye muumbaji na mwenye kuendeleza. 2) Neno la Mungu lote ni kweli. Hata sehemu ambazo hatupendi au hatuelewi. 3) Jambo la haki na lisilo la haki linatambuliwa na hufafanuliwa kulingana na kuelewa haswa Mungu ni nani.

1. Mungu ni Muumba na Msaidizi. Maadili ya hali ya mazingira inasema kwamba maadili hutegemea mazingira au matukio Fulani . Neno la Mungu linasema maadili hutegemea uhuru wa Mungu, kama Yeye ndiye mwumbaji na msaidizi. Na sio suala la kimantiki (semantics) bali ni kweli. Hata kama Mungu angeweza kutoa amri kwa kikundi kimoja cha watu na kukataza kikundi kingine, uamuzi wa kama ni sahihi au usio sahihi, haitegemei hali ilivyo, bali inategemea ile amri ya Mungu. Mungu ana mamlaka ya kutawala haki na mbaya. Warumi 3: 4 inasema, "Mungu na awe wa kweli na kila mtu ni mwongo."

2. Neno la Mungu lote ni kweli. Kuashiria kwamba Biblia inasisitiza maadili ya hali itakuwa ya kuashiria kuwa kuna makosa yaliyomo ndani yake. Hiyo haiwezekani. Haiwezekani kwa sababu kwanza Mungu ni muumbaji na msaidizi.

3. Haki na lisilo la haki hufafanuliwa kwa kuangazia haswa Mungu ni nani. Upendo ni asili ya Mungu. Anafafanua haswa upendo ni nini na sio kwa kile anachofanya, bali tu kwa yeye mwenyewe. Biblia inasema, "Mungu ni upendo" (1 Yohana 4:16). Upendo haujijali na kuwa na wasiwasi wa wengine, haujitafutii utukufu wake mwenyewe au radhi (1 Wakorintho 13). Kwa hiyo, kwa sababu ya ukuu Mungu , Biblia, kutolewa na Mungu na kuwa kweli, hawezi kuwa na mfumo wa maadili ambayo yenyewe hutetea asili ya Mungu. Maadili ya hali hupata haki na mabaya kufurahisha wengi au mtu mmoja kutokana na kujipenda. Upendo ni kinyume chake. Upendo unatafuta kuhimiza na kujenga wengine.

Matatizo mawili ya msingi na maadili ya hali ni kubaini ule ukweli kamili na dhana ya upendo halisi. Biblia inafundisha ukweli kamili, ambayo inaisitiza kuwa haki na maovu huteuliwa na Mungu Mtakatifu. Upendo wa Mungu kama vile anvyouelezea hauna ule ubaya au hitilafu wala ubinafsi. kama mtu angeweza kusema kuwa hali hiyo inahitaji kujitegemea, bado ni uamuzi wa binadamu na sio wa Mungu. Sababu za kibinadamu za kuamua ni bora zaidi, bila upendo wa kweli ni msingi wa ubinafsi.

Nini kinachotokea wakati vitu vinavyoonekana vizuri lakini Mungu anasema kwamba vina makosa? Ni lazima tumaini ukuu wa Mungu na tuwe na tumaini "kwamba vitu vyote Mungu hufanya kwa wema wa wale wanaompenda, ambao wameitwa kwa mujibu wa kusudi lake" (Waroma 8:28). Ikiwa sisi ni wa Kristo, Mungu ametupa roho wake mtakatifu (Yohana 16), na kupitia kwake au kuwa ndani yake tuna ufahamu wa kile kilicho sahihi na kibaya. Kupitia kwake sisi tuna hakika, tunahimizwa, na tunaongozwa kuwa wenye haki. Ikiwa mtu ana nia ya kujua ukweli wa suala, pamoja na kumtafuta Mungu, yeye atazawadiwa kwa jibu la Mungu. "Heri walio na njaa na kiu cha haki, kwani watajazwa" (Mathayo 5: 6).

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inafundisha maadili ya hali?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries