Swali
Je! Kanuni ya kifo cha mbadala ni gani?
Jibu
Mbadala ni mojawapo ya mada kuu katika Biblia. Mungu alianzisha kanuni ya mbadala katika bustani mwa Edeni wakati Adamu na Hawa walitenda dhambi. Kwa kumuua mnyama ili afunike uchi wao (Mwanzo 3:21), Mungu alianza kuchora taswira jinsi itakavyo mgharimu kumrejesha mwanadamu katika uhusiano mwema Naye. Aliendeleza mada hiyo na watu wake wateule Israeli. Kwa kuwapa Sheria, Mungu aliwaonyesha utakatifu Wake na akaonyesha jinsi wao wenyewe hawangeweza kufikia utakatifu huo. Kisha Mungu akawajalia mbadala wa kulipa gharama ya dhambi zao, kwa namna ya dhabihu za damu (Kutoka 29: 41-42; 34:19; Hesabu 29: 2). Kwa kumtoa mnyama asiye na hatia kulingana na maagizo ya Mungu, wanadamu waliweza kusamehewa dhambi zao na kuingia mbele za Mungu. Mnyama alikufa kwa niaipa ya mwenye dhambi, na hivyo kumruhusu mwenye dhambi kuenda huru na kuthibitishwa. Mambo ya Walawi 16 inatusimulia juu ya mbuzi wa kubebeshwa dhambi, ambaye wazee wa Israeli wangemwekelea mikono yao, kwa ishara ya kuhamisha dhambi za watu hadi kwa mbuzi. Kisha huyo mbuzi angeachiliwa huru kwenda jangwani, akiwa amebeba dhambi za watu kwenda mbali.
Mada ya kifo cha mbadala inapatikana katika Agano la Kale nzima kama ubashirifu wa kukuja kwa Yesu Kristo. Sherehe ya Pasaka vile vile iliangazia ubadala. Katika Kutoka 12 Mungu anapeana maagizo kwa watu wake kujitayarisha kwa kuja kwa Malaika wa Bwana ambaye atawaua vitinda mimba wanaume wa kila familia kama ishara ya hukumu kwa wa Misri. Njia pekee ya wangeepuka pigo hili ilikuwa ni kuchukua kondoo wa kiume mkamilifu, na kumua, na kupaka damu yake katika milingo ya milango ya nyumba zao. Mungu aliwaambia, "Damu itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonyesha nyumba ambazo mtakuwamo; nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri" (Kutoka 12:13). Kondoo wa Pasaka alikuwa mbadala kwa kila mwanaume mzaliwa wa kwanza ambaye angekubali.
Mungu aliendeleza mada hiyo ya mbadala hadi katika Agano Jipya kwa kukuja kwa Yesu. Mungu alikuwa ameandaa njia ili mwanadamu aweze kuelewa has ani nini Yesu alikuja kufanya. Wakorintho wa Pili 5:21 yasema, "Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye." Mwanakondoo wa Mungu mkamilifu alizichukua dhambi za dunia, akayatoa maisha Yake, na kufa kwa niapa yetu (Yohana 1:29; 1 Petro 3:18). Dhabihu pekee iliyokubalika ya dhambi ni sadaka kamilifu. Ikiwa tutakufia dhambi zetu wenyewe, basi haitatosha kulipia. Sisi sio wakamilifu. Ni Yesu pekee Mungu-Mwanadamu ambaye ni mkamilifu, anatimiza mahitaji yote, na aliyatoa maisha Yake kwa ajili kwa hiari (Yohana 10:18). Hakuna kitu tungefanya ili kujiokoa, kwa hivyo Mungu alifanya kwa niapa yetu. Unabii wa Masiha wa Isaya 53 unaifanya wazi kifo cha mbadala cha Kristo: "Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona" (aya ya 5).
Ubadala wa Yesu kwa niapa yetu ulikuwa kamilifu, kuliko dhabihu ya wanyama ya Agano la Kale. Waebrania 10:4 inasema, "kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi." Mtu mwingine anaweza sema, "Wamaanisha zile dhabihu zote za Wayahudi zilizofanywa zilikuwa za bure?" Mwandishi anabainisha kwamba damu ya mnyama pekee haikuwa na dhamana. Ilikuwa ni kile hiyo damu iliashiria kilifanya tofauti. Dhamini ya dhabihu za kale ikuwa kuwa mnyama alitumika kwa niapa ya dhambi za watu na hiyo iliashiria kwa dhabihu ya mwisho ya Christo (Waebrania 9:22).
Watu wengine hufanya makosa ya kufikiria kuwa, kwa vile Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, kila mtu ataenda mbinguni. Hii sio sahihi. Kifo kibadala cha Kristo zalime kitumiwe kibinafsi kw akila moyo, kwa njia ile ile ambayo damu ya Pasaka ililazimika kutumika kibinafsi kwa mlango (Yohana 1:12; 3:16-18; Matendo 2:38). Bala tuweze kuwa wenye "haki ya Mungu katika Yeye," lazima tubadilishane utu wetu wa kale wa dhambi na ule takatifu. Mungu anatoa njia mbadala, lakini ni lazima tuipokee kibadala hicho kibinafsi kwa kumkubali Krisot kwa imani (Waefeso 2:8-9).
English
Je! Kanuni ya kifo cha mbadala ni gani?