settings icon
share icon
Swali

Wokovu ni nini? Mafundisho ya kikristo ya wokovu ni yapi?

Jibu


Wokovu ni ukombozi kutokana na hatari au mateso. Kuokoa ni kukomboa au kulinda. Neno hubeba wazo la ushindi, afya, au kuhifadhi. Wakati mwingine, Biblia inatumia maneno kuokolewa au wokovu kwa kutaja muda, ukombozi wa kimwili, kama vile ukombozi waPaulo kutoka gerezani (Wafilipi 1:19).

Mara nyingi zaidi, neno "wokovu" husungumzia umilele wa, ukombozi wa kiroho. Wakati Paulo alimwaambia Mfilipi mfungwa kile lazima akifanye ili aokolewe, alikuwa akimaanisha hatima ya milele ya askari (Matendo 16:30-31). Yesu alilinganisha kuokolewa na kuingia ufalme wa Mungu (Mathayo 19:24-25).

Sisi tumeookolewa kutoka kwa? Katika mafundisho ya kikristo ya wokovu, sisi tumeokolewa kutoka kwa "ghadhabu," yaani, hukumu ya Mungu kwa dhambi (Warumi 5:9, 1 Wathesalonike 5:9). Dhambi yetu imetutenganisha na Mungu, na matokeo ya dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Wokovu wa kibiblia wahusu ukombozi wetu kutokana na matokeo ya dhambi na kwa hiyo unahusisha kuondolewa kwa dhambi.

Nani anaokoa? Mungu tu ndiye anaweza kuondoa dhambi na atuokoe na adhabu ya dhambi (2 Timotheo 1:9, Tito 3:5).

Ni namna gani Mungu anaokoa? Katika mafundisho ya kikristo ya wokovu, Mungu ametuokoa kwa njia ya Kristo (Yohana 3:17). Hasa, ni kifo cha Yesu msalabani na kilichofuatwa na kufufuka kwake ndio kilifikia mafanikio ya wokovu wetu (Warumi 5:10, Waefeso 1:7). Maandiko yako wazi kwamba wokovu ni neema, zawadi tusiyostahili kutoka kwa Mungu (Waefeso 2:5, 8) na unapatikana tu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo (Matendo 4:12).

Je, sisi hupokea wokovu namna gani? Sisi tumeokolewa kwa imani. Kwanza, ni lazima tuisikie injili- habari njema ya kifo cha Yesu na ufufuo wake (Waefeso 1:13). Basi, ni lazima tumwamini -kikamilifu Bwana Yesu (Warumi 1:16). Hii inahusisha toba, mabadiliko ya akili juu ya dhambi na Kristo (Matendo 3:19), na kulitia jina la Bwana (Warumi 10:9-10, 13).

Ufafanuzi wa kikristo wa mafundisho ya wokovu itakuwa "ukombozi, kwa neema ya Mungu, kutokana na adhabu ya milele ya dhambi ambayo ni nafasi kwa wale ambao hukubali kwa imani masharti ya Mungu ya toba na imani katika Bwana Yesu." Ukombozi unapatikana katika Yesu peke yake (Yohana 14:6; Matendo 4:12) na Mungu anategemewa kuutoa, uhakikisho na usalama.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wokovu ni nini? Mafundisho ya kikristo ya wokovu ni yapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries