Swali
Kwa nini majaribu ya ngono ni tatizo kubwa kwa wanaume kuliko kwa wanawake?
Jibu
Ingawa wanawake pia hupata majaribu ya ngono , kwa kawaida, wanaume wanakabiliana na majaribio hayo kwa kiwango kikubwa zaidi. Wanaume zaidi wanafanya uzinzi kuliko wanawake. Katika mahusiano kabla ya ndoa, kuna uwezekano wa juu kwa wanamume kutaka ngono kutoka kwa wapenzi wao kuliko wanawake.
Kwa nini iwe hivyo? Kwa nini majaribu ya ngono ni tatizo kubwa kwa wanaume kuliko kwa wanawake? Biblia haina jibu la swali hili. Badala yake, Biblia inaweka wazi kuwa usherati ni dhambi daima (Matendo 15:20, 1 Wakorintho 5: 1, 6:13, 18; 10: 8; 2 Wakorintho 12:21; Wagalatia 5:19; Waefeso 5 : 3; Wakolosai 3: 5; 1 Wathesalonike 4: 3; Yuda 7). Ukweli kwamba kushinda majaribu ya ngono mara nyingi ni vigumu sana kwa wanaume sio udhuru. "Ni ngumu kupinga" sio maelezo ambayo Mungu atakubali kutoka kwa mwanamume, au kutoka kwa mwanamke kwa jambo hilo. Tena, uasherati daima ni dhambi. Kwa hivyo, majaribu ya ngono ni ya kushindwa (1 Wakorintho 6:18), haijalishi jaribu hio ni kali au kidogo, au kama mtu anayejaribiwa ni mwanamume au mwanamke.
Kwa kuwa Biblia haitoi jibu mahsusi kwa nini majaribu ya ngono ni tatizo kubwa kwa wanaume kuliko wanawake, tunaweza kuangalia biolojia /saikolojia kwa ufahamu. Kwa kiasi kikubwa, wanaume wana hisia zaidi za ngono zaidi kuliko wanawake. Wanaume kwa kawaida wanafikiria kuhusu ngono mara nyingi na tamaa ya ngono mara nyingi zaidi kuliko wanawake. Hasa wakati kujamiiana hakujafanyika hivi karibuni, mwili wa kiume una hamu kubwa ya ngono. Hii inajumuishwa na ukweli kwamba wanaume wanavutiwa sana kwa kuona zaidi kuliko wanawake (ambayo pia inaeleza kwa nini wanaume huenda kukabiliana na kuangalia picha za ponografia). Kuona tu mwanamke mwenye kuvutia wakati mwingine yatosha kusababisha tamaa za kimwili. Ikiwa mtu hatokabiliani na mawazo ya ngono (kwa usaidizi wa Mungu), majaribu ya ngono huenda yakaongezeka na kuwa vigumu sana kupinga.
Tena, basi tunaweza kusema hamu ya ngono ya kiume ni ukweli, sio udhuru. Ikiwa mtu anaingia katika majaribio ya ngono, hamna mtu mwenye kulaumu lakini yeye mwenyewe. Wakorintho wa kwanza 10:13 husema, "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili." Kama hatutumia faida ya" mlango wa kutokea,'' "hatuna udhuru. Majaribu ya ngono yanaweza kuwa na nguvu, na dhambi ya ngono ni kati ya maovu zaidi (1 Wakorintho 6:18). Lakini, kwa msaada wa Mungu, majaribu ya ngono yanaweza kushindwa. Hii ni kweli kwa wanaume na wanawake.
English
Kwa nini majaribu ya ngono ni tatizo kubwa kwa wanaume kuliko kwa wanawake?