Swali
Majina ya malaika katika Biblia ni yapi?
Jibu
Biblia inasimulia malaika kuwa viumbe wa kiroho wenye nguvu ambao waliumbwa na Mungu kutekeleza kazi maalum mbinguni na duniani. Ingawa Biblia inataja “jeshi” ya malaika, inataja tu wachache.
Gabrieli ndiye malaika anayejulikana sana kwa kutajwa kwake katika Biblia. Kila mara anapotajwa, tunamwona akitenda kama mjumbe wa kutoa hekima au tangazo maalum kutoka kwa Mungu. Katika kitabu cha Danieli, Gabrieli alimtokea nabii Danieli ili kueleza baadhi ya maono ambayo Mungu alimpa Danieli kuhusu nyakati za mwisho (Danieli 8:15–27; 9:20–27). Wakati Danieli alikuwa na tatizo kuyaelewa maono, maelezo ya Gabrieli pamoja na maelezo mengine ya Biblia kuhusu nyakati za mwisho, yameturuhusu kufikia hitimisho fulani kuhusu jinsi nyakati za mwisho zitakavyokuwa.
Gabrieli pia anaonekana katika Agano Jipya. Alimtokea Zakaria hekaluni ili kutangaza Habari kwamba Elisabeti, mkewe Zakaria angemzaa Yohana. Gabrieli pia alimtokea Maria na tangazo ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Baadaye, Yosefu anapata mwongozo katika kutembelewa na wanandoa kutoka kwa Gabrieli. Kwa sababu ya umuhimu mkubwa sana ya matangazo haya ya kihistoria, inaonekaza kwamba Gabrieli ni mmoja wa wajumbe wakuu wa Mungu.
Malaika wa pili ambaye Biblia inamwita kwa jina ni Mikaeli, ambaye jinsi anavyofanya kazi ni tofauti sana na malaika Gabrieli. Mikaeli ni malaika mkuu, cheo hiki kinaonyesha kuwa Mikaeli ana cheo cha juu mbinguni. Ingawa haujulikani kwa hakika kuwa Mikaeli ndiye malaika mkuu pekee, uwezekano upo kulingana na Yuda 1:9, ambapo Mikaeli anarejelewa kwa hususan kuwa “Mikaeli malaika mkuu”. Ikiwa malaika wengine wakuu wapo, kuna uwezekano kuwa Mikaeli ndiye anayewaongoza.
Wakati Mikaeli anapoonekana katika Biblia, mara nyingi huwa ni katika vita vya aina fulani. Anapigana na malaika walioanguka (waliotenda dhambi dhidi ya Mungu na kuwa mapepo) na shetani kwa niaba ya watu Wake. Mikaeli anaonekana mara kadhaa katika kitabu cha Danieli kama shujaa (ona Danieli 10:21 na 12:1). Katika tukio moja, malaika Gabrieli anaelezea Mikaeli kama ambaye anapigana vita dhidi ya “mkuu wa ufalme wa Uajemi,” na kumwezesha Gabrieli kumfikia Danieli na kumwelezea maono hayo (Danieli 10:13).
Mikaeli pia anaonekana katika kitabu cha Ufunuo, wakati anapigana na joka kubwa-shetani-wakati wa nyakati za mwisho (Ufunuo 12:7-9). Ukweli kwamba Mikaeli anaongiza jeshi la malaika dhidi ya Shetani mwenyewe inadhibitisha cheo na mamlaka ya Mikaeli.
Ikiwa malika walioanguka wanajumuishwa katika orodha ya malaika ambao wametajwa katika Biblia, majina mawili zaidi yanapaswa kutajwa: nyota ya asubuhi/Shetani na Apolioni/Abadoni. Nyota ya asubuhi alimwasi Mungu na kutupwa chini kutoka mbinguni pamoja na malaika wengine waliomfuata. Kabla ya ukaidi wake, nyota wa asubuhi alikuwa kuimbe mzuri na mwenye mamlaka; lakini alitamani usawa na Mungu aliye juu zaidi na basi akawa mchafu na aliyelaaniwa (Isaya 14:12–18; Luka 10:18). Sasa anajulikana kama Shetani na adui mkuu wa Mungu ambaye hutazamia kudanganya na kuangamiza wanadamu wote (Yohana 10:10). Apolioni/Abadoni ni malaika mwingine aliyeanguka na anatajwa katika Ufunuo 9:11, na anaongoza jeshi la kishetani la nyakati za mwisho.
English
Majina ya malaika katika Biblia ni yapi?