settings icon
share icon
Swali

Je! Majira ya nyakati za mwisho ni gani?

Jibu


Huduma ya Got Questions (Huduma ya Nina Maswali" inachukua mtazamo matezo kabla ya mwisho wa dunia. Kutoka kwa mtazamo huo, hapa kuna orodha ya matukio ya nyakati za mwisho ambayo Biblia inatufunulia:

1. Unyakuzi wa kanisa. Kristo anakuja mawinguni "kunyakua" wale wote wanaomtumaini (1 Wakorintho 15:52). Wakati huo huo, "waliokufa katika Kristo" pia watafufuliwa na kupelekwa mbinguni. Kwa mtazamo wetu hii leo, hili ndilo tukio linalofuata katika ratiba ya nyakati za mwisho. Unyakuzi uu karibu; hakuna unabii mwingine wowote wa kibiblia unaohitaji kutimizwa kabla ya unyakuzi kutokea.

2. Kuinuka kwa Mpinga Kristo. Baada ya kanisa kuondolewa (2 Wathesalonike 2: 7-8), mtu aliye na nguvu za kishetani atapata uwezo wa kuudhibiti wa ulimwengu kwa ahadi za amani (Ufunuo 13: 1; Danieli 9:27). Atasaidiwa na mtu mwingine, anayeitwa nabii wa uwongo, ambaye anaongoza mfumo wa kidini ambao unahitaji kuabudiwa kwa Mpinga Kristo (Ufunuo 19:20).

3. Dhiki. Kipindi cha miaka saba ambayo hukumu ya Mungu itakuwa imemwagwa juu ya wanadamu wenye dhambi (Ufunuo 6-16). Kuinuka hadi mamlakani kwa Mpinga Kristo kunahusishwa na kipindi hiki cha wakati. Wakati wa dhiki duniani, Kanisa litakuwa mbinguni. Inafikiriwa kuwa wakati huu Kiti cha Hukumu cha Kristo na Karamu ya Ndoa ya Mwanakondoo itafanyika mbinguni (2 Wakorintho 5:10; Ufunuo 19: 6-10).

4. Vita vya Gogu na Magogu. Katika sehemu ya kwanza ya dhiki, jeshi kubwa kutoka kaskazini, kwa kushirikiana na nchi zingine nyingi kutoka Mashariki ya Kati na Afrika, zitaifamia Israeli na zitashindwa kwa nguvu za Mungu (Ezekieli 38-39). (Watoa maoni wengine husema kuwa vita hivi vilitokea kabla ya kuanza kwa dhiki.)

5. Chukizo la uharibifu. Katikati mwa dhiki ya miaka saba, Mpinga Kristo anavunja agano lake na Israeli na anaonyesha tabia yake kamili. Wayahudi wanatawanyika, na wengi wao wanamrudia Bwana, wakigundua kwamba Yesu ndiye Mwokozi wao. Mateso makubwa yanazuka dhidi ya wale wote wanaomwamini Kristo (Danieli 12:11; Marko 13:14; Ufunuo 12:17).

6. Vita vya Armagedoni. Mwishoni mwa dhiki, Yesu atarudi na majeshi ya mbinguni (Marko 14:62). Ataokoa Yerusalemu kutokana na maangamizi na kuyashinda majeshi ya mataifa yanayopigana chini ya Mpinga Kristo (Ufunuo 19: 11–21). Mpinga Kristo na nabii wa uwongo watakamatwa na kutupwa wakiwa hai katika ziwa la moto (Ufunuo 19:20).

7. Hukumu kwa mataifa. Kristo atawahukumu manusura wa dhiki, akiwatenga waadilifu na waovu kama "kondoo" na "mbuzi" (Mathayo 25: 31-46). (Inafikiriwa kuwa wakati huu watakatifu wa Agano la Kale watafufuliwa kutoka kwa wafu.) Wenye haki wataingia katika Ufalme wa Milenia; waovu watatupwa kuzimuni.

8. Kufungwa kwa Shetani. Shetani atafungwa na kushikiliwa Jehannam kwa miaka 1,000 ijayo (Ufunuo 20: 1–3).

9. Ufalme wa Milenia. Yesu mwenyewe atatawala ulimwengu, na Yerusalemu ndio utakuwa mji mkuu. Hiki kitakuwa kipindi cha miaka 1,000 cha amani na ustawi duniani (Ufunuo 20; Isaya 60-62). Dhabihu za ukumbusho zitafanywa katika hekalu lililojengwa upya huko Yerusalemu (Ezekieli 40-48).

10. Vita vya mwisho. Mwishoni mwa miaka 1,000, Shetani ataachiliwa kutoka gerezani mwake kwa muda mfupi. Atadanganya mataifa mara nyingine tena, na kutakuwa na uasi dhidi ya Bwana ambao utashindwa kwa haraka (Ufunuo 20: 7-10). Shetani atatupwa ndani ya ziwa la moto, na hataonekana tena.

11. Hukumu kuu ya Kiti kikuu cheupe cha enzi. Wale wote walioko kuzimuni watatolewa, na waovu wote kutoka nyakati zote za historia watafufuliwa ili kusimama mbele za Mungu katika hukumu ya mwisho (Ufunuo 20: 11-15). Hukumu itasomwa, na wanadamu wote wenye dhambi watatupwa katika ziwa la moto.

12. Uumbaji mpya. Mungu ataumba upya mbingu nan chi. Ni waka huu ambapo Mungu atayapanguza machozi na hakutakuwa na uchungu tena, kifo, wala husuni. Yerusalemu Mpya itashuka kutoka mbinguni, na watoto wa Mungu watafurahia milele pamoja Naye (Ufunuo 21–22).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Majira ya nyakati za mwisho ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries