settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu malaika?

Jibu


Malaika ni viumbe vya kiroho ambao wako na hekima, hisia, na nia. Hii ni kweli kwa malaika wazuri na wabaya (mapepo). Malaika wako na hekima (Mathayo 8:29; 2 Wakorintho 11:3; 1 Petero 1:12), inaonyesha hisia (Luka 2:13; Yakobo 2:19; Ufunuo 12:17), na kujaribu kufanya penzi lao (Luka 8:28-31; 2 Timotheo 2:26; Yuda 6). Malaika ni viumbe vya kiroho (Waebrania 1:14) bila na kuwa na mwili. Ingawa hawana mwili, bado wako na hali ya mwili.

Kwa sababu na viumbe, hekima yao ni ndogo. Hii inamaanisha kuwa hawajui mambo yote vile Mungu anajua (Mathayo 24:36). Wanaonekana kuwa na maarifa sana kuliko mwanadamu, ingawa inaweza kuwa kwa sababu ya mambo matatu. Kwanza, malaika waliumbwa mtindo wa viumbe wakiwa juu kuliko mwanadamu. Kwa hivyo tangu kuumbwa wako na hekima. Pili, malaika waisoma Bibilia na ulimwengu sana kuliko mwanadamu na wanapata maarifa kutokana na kusoma kwao (Yakobo 2:19; Ufunuo 12:12). Tatu malaika wapata maarifa kupitia kutazama kwao mwanadamu kwa muda kazi ya mwanadamu. Kinyume na mwanadamu, malaika hawastahili kuyachunguza yaliyopita kwa maana wamekwisha yapitia. Kwa hivyo wanajua vile wengine wametenda na vile wemetoa hisia zao katika hali zinazowakumba na wanaweza kutabiri kwa ukamilifu wa juu sana vile tunaweza kuwa katika hali sawa.

Ingawa wako na hisia, malaika, kama viumbe wengine, wamenyenyekea kwa mapenzi ya Mungu. Malaika wazuri wametumwa na Mungu ili kuwazaidia wakristo (Waebrania 1:14). Hapa baadhi ya kazi ambayo Bibilia inaelezea kuhusu malaika: Wanamsifu Mungu (Zaburi 148:1-2; Isaya 6:3). Wanamwabudu Mungu (Waebrania1:6; Ufunuo 5:8-13). Wanafurahia kwa kile Mungu amefanya (Ayubu 38:6-7). Wanamtumikia Mungu (Zaburi 103:20; Ufunuo 22:9). Wanaleta mbele za Mungu (Ayubu 1:6; 2:1). Wao ni vyombo vya hukumu ya Mungu (Ufunuo 7:1; 8:2). Wanaleta majibu ya maombi (Matendo Ya Mitume 12:5-10). Wanazaidia kuleta watu kwa Kristo (Matendo Ya Mitume 8:26; 10:3). Wanautazama mtindo wa mwanadamu, kazi na matezo (1 Wakorintho 4:9; 11:10; Waefeso 3:10; 1 Petero 1:12). Wanatia moyo wakati wa hatari/hali ngumu (Matendo Ya Mitume 27:23-24). Wanawashughulikia watakatifu wakati wa kifo (Luka 16:22).

Malaika ni wa mtindo tofauti na binadamu. Mwanadamu hawezi kuwa malaika baada ya kufa. Malaika kamwe hawatakuwa mwanadamu. Mungu aliwaumba vile alivyowaumba wanadamu. Hamna mahali Bibilia inasema kwamba malaika wameumbwa kwa mfano wa Mungu, kama wanadamu katika (Mwanzo 1:26). Malaika ni viumbe vya kiroho, hadi kiwango kingine wanachukua umbo la mwili. Mwanadamu ako na umbo la mwili, lakini pia na mwili wa kiroho. Kitu kikubwa tunaweza kukisoma kutoka kwa malaika watakatifu ni utiifu wao usio na kikomo na usio na maswali kwa mtu yeyote.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu malaika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries