settings icon
share icon
Swali

Kuna aina gani za malaika tofauti?

Jibu


Kuna vikundi mbili za malaika: malaika "ambao hawajaanguka" na malaika walioanguka. Malaika wasioanguka ni wale ambao wamebakia watakatifu wakati wa kuwepo kwao na kwa hivyo wanaitwa "malaika watakatifu." Katika Maandiko, kwa kawaida wakati malaika wanatajwa, ni kundi la malaika watakatifu ambao huwa wanazungumziwa. Kwa upande mwingine, malaika walioanguka ni wale ambao hawajaendelea kutunza utakatifu wao.

Malaika watakatifu huwa katika vikundi maalum, na watu fulani huitwa na kutajwa. Mikaeli ambaye ni malaika mkuu anawaongoza malaika wote watakatifu, na jina lake linamaanisha "ambaye ni kama Mungu?" (Danieli 10:21, 12: 1, 1 Wathesalonike 4:16; Yuda 1: 9; Ufunuo 12: 7-10). Gabrieli ni mmoja wa wajumbe wakuu wa Mungu, jina lake linamaanisha "shujaa wa Mungu," na alipewa ujumbe muhimu kama vile ujumbe uliopewa Danieli (Danieli 8:16; 9:21), uliopewa Zekaria (Luka 1: 18- 19), na Maria (Luka 1: 26-38).

Malaika wengi watakatifu hawajatajwa katika Biblia bali huelezwa tu kama "malaika waliochaguliwa" (1 Timotheo 5:21). Maneno "ukuu" na "mamlaka" yanaonekana kutumika kwa malaika wote haijalishi wameanguka au ni watakatifu (Luka 21:26; Warumi 8:38, Waefeso 1:21, 3:10; Wakolosai 1:16; 2:10, 15) ; 1 Petro 3:22). Malaika wengine huteuliwa kama "makerubi," ambao ni viumbe hai ambao hulinda utakatifu wa Mungu kutoka kwa uchafu wowote wa dhambi (Mwanzo 3:24; Kutoka 25:18, 20). "Maserafi" ni kikundi kingine cha malaika, ambacho kimezungumziwa mara moja tu katika Maandiko katika Isaya 6: 2-7, na huelezwa kuwa na jozi tatu za mabawa. Wao wanaonekana kuwa na kazi ya kumsifu Mungu, kuwa wajumbe wa Mungu duniani, na hususan wanahusishwa na utakatifu wa Mungu. Maandiko imerejelea huduma za malaika watakatifu, ambazo ni pana. Malaika watakatifu walikuwapo wakati wa uumbaji, utoaji wa Sheria, kuzaliwa kwa Kristo na ufufuo wake, kupaa mbinguni, na watakuwapo katika kuinyakuliwa kwa Kanisa na kuja kwa pili kwa Kristo.

Tofauti kabisa na kikundi cha malaika watakatifu, malaika walioanguka pia hawana idadi kubwa, ingawa ni wachache kuliko malaika watakatifu, na wanaelezewa kuwa wameanguka kutoka nyadhifa zao za kwanza. Wanaongozwa na Shetani, ambaye hapo awali alikuwa malaika mtakatifu, malaika walioanguka walipinga, waliasi dhidi ya Mungu, na wakawa wenye dhambi katika hali zao na kazi zao. Malaika walioanguka wamegawanywa katika makundi mawili: wale ambao ni huru na wale ambao wamefungwa. Katika malaika walioanguka, Shetani pekee amepata kutajwa katika Biblia. Wakati Shetani alianguka (Yohana 8:44; Luka 10:18), alifuatwa na theluthi moja ya malaika. Kati ya hayo, baadhi yao wamefungwa na minyororo wakingoja hukumu (1 Wakorintho 6: 3, 2 Petro 2: 4; Yuda 1: 6), na waliosalia wako huru na ni pepo, ambao wametajwa katika Agano Jipya (Marko 5: 9, 15, Luka 8:30, 1 Timotheo 4: 1). Wao ni watumishi wa Shetani katika kazi zake zote na watapata adhabu kama yeye(Mathayo 25:41; Ufunuo 20:10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna aina gani za malaika tofauti?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries