Swali
Je, ni makosa kuwa na sanamu za malaika?
Jibu
Katika na wao wenyewe, hakuna makossa ya kuwa na sanamu za malaika. Jinsi mtu anavyoona mfano wa picha ya malaika ndio itaamua kama ni sahihi. Sababu ya pekee ya malaika wanaweza kuwa wabaya ni ikiwa watachukuliwa kuwa mungu, wanatumika katika maombi, au wanaabudiwa, ambayo Mungu anachukia (1 Samweli 12:21). Hatuabudu malaika au sanamu za malaika. Mungu peke yake anastahili kuabudiwa (Zaburi 99: 5; Luka 4: 8), na tunapaswa kumtegemea Yeye peke yake (Zaburi 9:10). Biblia inakemea sana picha za kidini. Matokeo yake, Wakristo wanapaswa kuwa makini sana kamwe wasiruhusu sanamu, kama malaika miungu, picha ya Yesu, eneo la kuzaliwa, nk, kuwa kama mtego au kifunga macho.
Huku kukiwa hakuna dhambi katika kuwa na mifano inayowakilisha malaika au kiumbe kingine chochote, hatupaswi kuwapatia uwezo wowote wa kawaida au kuwa na ushawishi juu ya maisha yetu. Hakuna mfano unaoweza kutukinga na madhara, kutuletea bahati nzuri, au kutuathiri kwa namna yoyote. Imani hiyo ni usingaombwe tu, ambayo haina nafasi katika maisha ya Mkristo. Kuhusiana na ushirikina ni ibada ya sanamu, na ibada ya sanamu imekatazwa wazi katika Maandiko, na hakuna mtu anayeifanya ataingia katika Ufalme wa Mungu (Ufunuo 21:27).
Pia, ni busara kutambua kwamba hatujui hasa jinzi malaika halisi wanavyoonekana. Mifano ni dhana ya mtu jinzi malaika anaweza kuonekana.
English
Je, ni makosa kuwa na sanamu za malaika?