settings icon
share icon
Swali

Mchungaji ana mamlaka kiasi gani juu ya kanisa?

Jibu


Kanisa linaitwa "kundi la Mungu" (1 Petro 5: 2), "urithi wa Mungu" (1 Petro 5: 3), na "kanisa la Mungu" (Matendo 20:28). Yesu ni "kichwa cha kanisa" (Waefeso 5:23) na "Mchungaji Mkuu" (1 Petro 5: 4). Kanisa ni haki ya Kristo, na Yeye ndiye mamlaka juu yake (Mathayo 16:18). Hii ni sawa na kanisa la mtaa kama Mwili wa Kristo wa ulimwengu wote.

Mpango wa Mungu wa kulijenga kanisa lake ni pamoja na kutumia watu katika ofisi ya mchungaji. Mchungaji ni mzee wa kwanza, na pamoja na wazee wengine, mchungaji anawajibika kufanya mambo yafuatayo:

1) Kuangalia kanisa (1 Timotheo 3: 1). Maana ya msingi ya neno askofu ni "mwangalizi." Uangalizi mkuu wa huduma na utendaji kazi wa kanisa ni wajibu wa mchungaji na wazee wengine. Hii itajumuisha utunzaji wa fedha ndani ya kanisa (Mdo. 11:30).

2) Utawala juu ya kanisa (1 Timotheo 5:17). Neno lililotafsiriwa "utawala" halisi linamaanisha "kusimama mbele." Wazo ni kuongoza au kushugulikia, kwa msisitizo kuwa mwangalifu wa kujitahidi. Hii itajumuisha wajibu wa kutumikia nidhamu ya kanisa na kuwaadhibu wale wanaopotea kutoka kwenye imani (Mathayo 18: 15-17; 1 Wakorintho 5: 11-13).

3) Kulisha kanisa (1 Petro 5: 2). Kwa kweli, neno askofu lina maana "mchungaji." Mchungaji ana wajibu wa "kulisha kundi" kwa Neno la Mungu na kuwaongoza kwa njia sahihi.

4) Kulinda mafundisho ya kanisa (Tito 1: 9). Mafundisho ya mitume yalikuwa yapewe "watu waaminifu" ambao watafundisha wengine pia (2 Timotheo 2: 2). Kuhifadhi uaminifu wa injili ni mojawapo ya wito wa juu wa mchungaji.

Wachungaji wengine wanaona jina "mwangalizi" kama amri ya kuwa na mkono wao katika kila kitu. Ikiwa ni kusimamia vipasa sauti au kuchagua nyimbo za Jumapili au kukusanya vitambaa, wachungaji wengine huhisi ni wajibu wao kushiriki katika kila uamuzi. Hii haichosi pekee mchungaji ambaye hujikuta katika kila mkutano wa kamati, pia huwazuia wengine kutumia zawadi zao kanisani. Mchungaji anaweza kusimamia na kugawa kwa wakati mmoja. Aidha, mfano wa kibiblia wa wazee wengi, pamoja na madikoni waliochaguliwa kumsaidia mchungaji na wazee, huzuia uchungaji kutoka kudhibitiwa na mtu mmoja.

Amri ya "kutawala" kanisa wakati mwingine huchukuliwa kuwa mbaya pia. Wajibu rasmi wa mchungaji ni kutawala kanisa pamoja na wazee, na lengo lake linapaswa kuwa hasa kiroho, kushugulikia mambo kama vile kuimarisha waumini na kuwawezesha watakatifu kufanya kazi ya huduma (Waefeso 4:12). Tumesikia wachungaji ambao wanaonekana kuwa na ukatili zaidi kuliko mchungaji, wanawataka wale walio chini ya mamlaka yao kutafuta ruhusa yao kabla ya kufanya uwekezaji, kwenda likizo, nk. Wanaume hawa, inaonekana kwetu, wanahitaji kudhibitiwa na hawastahili kutawala kanisa la Mungu (angalia 3 Yohana 9-10).

Waraka wa Kwanza wa Petro 5: 3 ina maelezo mazuri kuhusu huduma ya uchungaji: "Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi." Mamlaka ya mchungaji sio kitu "cha kutawala" kanisa; badala, mchungaji ni mfano wa ukweli, upendo, na utakatifu kwa kundi la Mungu kufuata. (Ona pia 1 Timotheo 4:12.) Mchungaji ni "msimamizi wa Mungu" (Tito 1: 7), na anawajibika kwa Mungu kwa uongozi wake kwa kanisa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mchungaji ana mamlaka kiasi gani juu ya kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries