settings icon
share icon
Swali

Mkristo anapaswa kuwa na mtazamo gani kwa mantiki?

Jibu


Mantiki ni sayansi ya kupata ukweli kupitia uchambuzi wa ukweli ama moja kwa moja au njia isiyo moja kwa moja. Mantiki huchukua vidokezo fulani, inachambua mahusiano, inayafananisha na mambo mengine yanayotambulika, na hufika kwenye hitimisho ambalo inabainisha ukweli uliojulikana hapo awali. Mantiki ni hisebati na mawazo badala ya herufi. Ni njia ya kutambua uhusiano kati ya mawazo.

Mantiki inaonekana kuwa ni moja ya sheria za asili ambazo Mungu aliweka wakati wa uumbaji wa ulimwengu. Kisha, Mungu aliumba watu wenye akili na uwezo wa kufikiria. Ikiwa uumbaji wa Mungu, mantiki ni jambo jema ambalo, linapotumiwa vizuri, linaweza kutuelekeza kwa Mungu. Kwa bahati mbaya, ni rahisi kutumia mantiki kwa njia isiyo sahihi.

Sayansi ya mantiki inahusika na fomu za mahusiano ya mawazo. Kama idadi katika hesabu, mawazo yanaweza kufungiwa kwa fomu zinazoonyesha uhusiano wao na mawazo mengine. Ni manufaa kuelewa misingi ya kanuni hizi. Mazungumzo ya kisasa mara nyingi yamejawa na hisia, ambazo zinaweza kuandika mazungumzo na kuzuia azimio muhimu. Juhudi inaweza kuzuia njia ya kweli. Mara nyingi, ukweli umefichwa na kile kinachojulikana kama hoja ya udanganyifu kulingana na mantiki ya uongo na mawazo mabaya. Uongo ni mbinu ya unyanyasaji, na hailekezi kwa majadiliano ya faida.

Mantiki kwa maana halisi inajumuisha njia zote na ukweli. Aina hizi hutoa mahusiano, lakini kuna lazima kuwe na mawazo ya msingi yanayotokana na fomu ya kuchambua. Ingawa ukadri unapisha njia hata kwa mawazo ya msingi, watu wengi bado wanategemea ushahidi-mahususi- habari wao wanakusanya kwa njia ya akili zao. Watu wengi wana ujasiri wa kutoa kauli kama vile "Mimi nipo" na "meza ipo." Mantiki inachukua kauli kama hiyo na hupata ukweli zaidi. "Kitu chochote kilicho na mwanzo kinapaswa kufanywa na kitu kingine" ni kauli iliyoelezewa kwa umantiki. Uchunguzi zaidi unaongoza kwa kweli tatanishi zaidi, kama vile "Mungu yupo."

Kwa bahati mbaya, wajadili wengi hujipata kwa udanganyifu kwa sababu hawaanzi toka mwanzoni. Hiyo ni kusema, wao huruhusu wazo la awali, halijathibitishwa kusimamia ukweli. Wavumbuzi wanaanza na mageuzi ya asili kama msingi wa hoja zao kwa sababu hawakubali uwezekano wa miujiza. Dini nyingi zinakataa kwamba Yesu ndiye Mungu-kwa sababu wanaanza na Uaginostiki (kimwili ni mbaya, kiroho ni nzuri). Wasioamini dini ambao wanasisitiza kwamba dini ni hisia ya kawaida ya akili kwa kuhofia kifo dhana inayoanza kwamba Mungu hayupo.

Ukweli ni kwamba, watu wengi hawatashawishika kiwango kikubwa na mantiki ili waamini kitu kilicho kinyume na imani zao. Kawaida, hisia hupita mantiki. Na, ingawa Yesu wala mitume hawakuwa wageni wa mantiki, haikuwa chombo chao cha msingi. Wakati Petro anasema kuwa "... tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu" (1 Petro 3:15), hakumaanisha uanza na hoja ya kuwepo kwa Mungu. Alimaanisha kuwa tuwe tayari kwa habari za uhusiano wetu na Mungu na matumaini ambayo yamekuja kutoka kwake. Mtu anayetumia imani yake juu ya hisia hawezi kufuatilia mazungumzo ya kimantiki. Mantiki mikononi mwa mtetezi aliyefunzwa ni chombo chenye nguvu. Lakini kinachoshawishi sawia ni "ushahidi wa kimwili" wa maisha ya Kikristo. Sisi ni "nuru ya ulimwengu" (Mathayo 5:14); giza haliwezi kupenda mwanga, lakini haliwezi kukana kuwepo kwake. Kama Paulo alivyowaagiza Tito, "... katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,

8 na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu" (Tito 2: 7-8).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo anapaswa kuwa na mtazamo gani kwa mantiki?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries