settings icon
share icon
Swali

Je! Maombi ya pamoja ni muimu? Maombi ya pamoja ni ya nguvu kuliko ya mtu mmoja?

Jibu


Maombi ya pamoja ni sehemu muimu katika maisha ya kaninsa, pamoja na ibada, na kanuni nzuri, kuumega mkate, na ushirika. Kanisa la kwanza lilikutana kila wakati ili wajifunze kanuni ya mitume, kuumega mkate na kuomba pamoja (Matendo Ya Mitume 2:42). Wakati tunaomba pamoja na Wakristo wengine madhara yatakua ya muimu. Maombi ya pamoja hujenga na kuleta umoja tunaposhiriki imani moja. Roho huyo huyo Mtakatifu ambaye anakaa pamoja na kila Mkristo anazifanya nyoyo zetu kuwa na furaha tunaposikia sifa kwa Bwana wetu mwokozi, zikitushikanisha pamoja kwa ushirika ambao haupatikani mahali popote katika maisha.

Kwa wale wanaweza kuwa peke yao na kungángána na taabu za maisha, wakisikia wengine wanawainua mbele ya kiti cha neema itakuwa jambo kubwa la kutia moyo. Pia inajenga ndani yetu upendo wa kuwajali wengine wakati tunawaombea. Kwa wakati huo huo, maombi ya pamoja yatukua dhihirisho la moyo wa mtu binafsi anayeshiriki. Tunastahili kuja kwa Mungu kwa unyenyekevu (Yakobo 4:10), ukweli (Zaburi 145:18), kutii (1 Yohana 3: 21-22), na shukrani (Wafilipi 4:6), na ujaziri (Waebrania 4:6). Cha kushangaza ni kuwa, maombi ya pamoja yanaweza kuwa jukwaa kwa wale maneno yao yanaelekea kwa wasikilizaji, lakini si kwa Mungu. Yesu alionya kuhusu tabia kama hizo katika Mathayo 6:5-8 mahali ambapo anatufunza tusiwe wa kuchukuliwa na upepo kama huo au unafiki katika maombi yetu, bali tuombe kisiri katika nyumba zetu ili tuepuke majaribu ya kutumia maombi kiunafiki.

Hakuna kitu katika maandiko cha kupendekeza kuwa maombi ya pamoja “yako na nguvu” kuliko ya mtu mmoja katika hali kuwa yanautembesha mkono wa Mungu. Kwa umbali sana, Wakristo wanazawazisha maombi na “kupata vitu kutoka kwa Mungu” na maombi yanakuwa mahali pa kukalili idadi ya haja zetu. Maombi ya kibibilia, huwa na sura tofauti, yakijumlisha haja zote na kuingia katika ufahamu na uhusiano wa ndani na Mtakatifu wetu, mkamilifu na Mungu mwenye haki. Kwamba Mungu kama huyo atakunja sikio lake kwa viumbe wake ambao wanaweka sifa na ibada kwa wingi (Zaburi 27:4; 63:1-8), na kuzaa moyo wa toba na kukiri (Zaburi 51; Luka 18:9-14), waanzisha moyo wenye nia na shukrani (Wafilipi 4:6; Wakolosai 1:12), na kuunda hali ya kuwamboe wengine kwa niapa yao (2 Wathesalonike 1:11; 2:16).

Maombi kwa hivyo kushirikiana na Mungu ili alete mpango wake, sio kujaribu kumkunja aingie kwa mapenzi yetu. Tunapoacha haja zetu kwa kujitoa kwa Yeye ajuaye hali zetu sana kutuliko na Yeye “chenye unahitaji kabla uulize” (Mathayo 6:8), maombi yetu yanafikia upeo wake. Maombi yametolewa kwa unyenyekevu kwa mapenzi yake, kwa hivyo kila wakati yanajibiwa , hata kama yametolewa na mtu mmoja au watu elfu.

Dhana kuwa maomba ya pamoja yanaweza mzawishi Mungu yatokana na kufasiri vipaya Mathayo 18:19-20, “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo kakati yao.” Aya hizi zinatoka katika ufahamu mkubwa ambao wazungumzia mpangilio utakaofuatwa katika kesi ya kumwadhibu mshirika wa kanisa. Kuzifasiri kama kuahidi Wakristo cheki tupu kwa kitu chochote watakacho kubaliana kumwomba Mungu, haijalishi kama ni cha dhambi au upumbavu, sio eti hakiingiliani na masingara ya adhabu ya kanisa, bali yakataa maandiko mengine yote hasa ukuu wa Mungu.

Kwa kuongezea, kuamini kuwa wakati “wawili watatu wamekusanyika” kuomba, nguvu zingine za kiuchawi zinatumika papo hapo katika maombi yetu sio uungaji wa kibibiilia, hata kama huyo mtu ametenganishwa na wengine kwa umbali wa maili elfu moja. Maombi ya pamoja ni muimu kwa sababu yajenga umoja (Yohana 17:22-23), na ni sehemu kuu kwa Wakristo kutiana moyo wao kwa wao (1 Wathesalonike 5:11) na kuwaelekeza kwa upendo na matendo mema (Waebrania 10:24).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Maombi ya pamoja ni muimu? Maombi ya pamoja ni ya nguvu kuliko ya mtu mmoja?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries