Swali
Ninawezaje kujua kama mapenzi ya moyo wangu yanatoka kwa Mungu?
Jibu
Yesu anajibu swali hili kwa ajili yetu: "Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano" (Mathayo 15:19). Halafu: "Kinachotoka kwa mwanadamu ndicho kinachosababisha kuwa" najisi. "Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, mauaji, uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, uovu, wivu, unyanyasaji, kiburi na upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. "(Marko 7: 20-23).
Katika vifungu hivi, Yesu anafunua chanzo cha matakwa yetu: tamaa zetu za kimwili zinatoka ndani yetu. Dhambi haikuji tu kama matokeo ya mazingira ya nje. Huwa inazaliwa katika siri za mawazo na nia zetu, kutoka kwa tamaa za siri ambayo tu akili na moyo vinaweza kutazama. Msingi ni kwamba, katika hali yetu ya kuanguka, tamaa za mioyo yetu huwa hazitoki kwa Mungu. Yeremia inathibitisha zaidi hali ya moyo wa mwanadamu: "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vote, unazidi tiba. Ni nani awezaye kuuelewa? "(Yeremia 17: 9)
Kwa muda mrefu imekuwa maoni ya wengi kwamba wanadamu wote kimsingi ni wema na wenye heshima na kwamba ni hali ya maisha kama vile umasikini au kulelewa vibaya ambayo inatugeuza kuwa wauaji na wezi. Lakini Biblia inafundisha kwamba watu wote wanakabiliwa na udhaifu wa kawaida-dhambi. Mtume Paulo anitaja kuwa asili yetu ya dhambi. " Kwa maana najua ya kuwa ndani ya mwili wangu, halikai neon jema, kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, sitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni dhambi ikaayo ndani yangu "(Warumi 7: 18-20). Mioyo yetu myovu hutuongoza kutenda dhambi.
Zaidi ya hayo, moyo ni mbaya sana na ina udanganyifu kwamba nia zetu hazijulikani hata kwetu wenyewe. Kama viumbe wenye dhambi tunaunda mambo maovu kwa kiburi na kujitosheleza mioyoni yetu (Methali 16:30, Zaburi 35:20, Mika 2: 1, Warumi 1:30). Ukweli ni kwamba Mungu peke yake ndiye anaweza kuchunguza nia zetu kwa kina na tamaa za ndani, na tu kwa Nguvu Zake tunaweza kumtumaini kuondokana na kutokuwa na uhakika na uchafu ambao umefungwa ndani ya mioyo yetu. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake(Waebrania 4: 11-13).
Kwa bahati nzuri, Mungu hatatuachi katika shida zetu na tamaa mbaya na tamaa za dhambi. Badala yake, anatupa neema na nguvu tunayohitaji kupinga na kuondokana na dhambi wakati inapobisha kwenye mlango wa mioyo yetu. Mtunga-zaburi anatuambia "Nawe utajifurahisha kwa BWANA na atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi Bwana njia yako, pia umtumaii, naye atafanya hivi, ataifanya a haki yako kama nuru, na hukumu yako kama adhuhuri . "(Zaburi 37: 4-6).
Mungu anaweza kufanya mapenzi yake kuwa ndani ya moyo wa mwanadamu, moyo ambao, bila Yeye, inakuwa mbaya na yenye udanfanyifu. Anachukua nafasi ya uovu kwa mema na kuelekeza mioyo yetu kwake. Kuondokana tamaa zetu na kuzibadilisha na zake. Hii hutokea tu tunapokuja kwake kwa kutubu na kukubali zawadi ya wokovu kupitia Bwana Yesu Kristo. Wakati huo, Yeye huondoa mioyo yetu ya jiwe na kuiweka kwa mioyo ya mwili (Ezekieli 11:19). Yeye hutimiza hili kwa kuingizwa kwa Roho Wake katika mioyo yetu. Kisha haja zetu kuwa matamanio Yake, mapenzi yetu yanafaniyika kuwa mapenzi Yake, na uasi wetu unageuka kuwa utii wa furaha.
English
Ninawezaje kujua kama mapenzi ya moyo wangu yanatoka kwa Mungu?