settings icon
share icon
Swali

Unyakuzi utatokea lini ukiambatana na matezo?

Jibu


Muda wa unyakuzi kuambatana na matezo ni mojawapo ya kitu ambacho ni cha kutatanisha katika kanisa leo. Kuna mitazamo mitatu ya kimsingi nayo ni matezo kabla ya (unyakuzi utatokea kabla ya matezo), wakati wa matezo (unyakuzi utatokea katikati mwa matezo), matezo baada ya unyakuzi (matezo yachayo baada ya unyakuzi). Mtazamo wa nne, ambao wajulikana sana ghadhabu kabla ya matezo, ni rembesho kidogo juu ya wakati wa matezo.

Kwanza ni muimu kutambua lengo la matezo. Kulingana na Danieli 9:27, kuna miaka saba ambayo inakuja. Ufunuo wa Danieli wote wa miaka sabini na saba (Danieli 9:20-27) anasungumzia taifa la Israeli. Ni kipindi cha wakati ambapo Mungu anaangazia taifa la Israeli. Mwaka wa saba, matezo, lazima kuwe ni wakati ambao Mungu analihukumu taifa la Israeli. Ingawa hii haionyeshi kuwa kanisa litakua hapo, inaleta swali kuwa ni kwa nini kanisa litakua ulimwenguni wakati huo.

Kifungo cha Bibilia kinachohusu unyakuzi ni 1 Wathesalonike 4:13-18. Inasema kuwa wote walio hai, pamoja na wateule waliokufa, watakutana na Bwana Yesu mawinguni na watakua naye milele. Unyakuzi ni Mungu kuondoa watu wake katika ulimwengu. Aya zingine baadaye katika 1 Wathesalonike 5:9, Paulo anasema, “Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo .“ kitabu cha Ufunuo Wa Yohana ambacho kwa undani kinasungumzia kipindi cha matezo, pia ni ujumbe wa kinabii jinsi Mungu ataimwaga ghadhabu yake ulimwenguni wakati wa matezo. Kitaonekana kitu kisicho na ukweli kwa Mungu kuahidi wateule kwamba hawatatezeka kwa ghadhabu na awaache ulimwenguni kutezeka ndani ya ghadhabu ya matezo. Hoja kuwa Mungu aliahidi kuwaokoa Wakristo kutoka kwa ghadhabu muda mfupi baada ya kuahidi kuwatoa watu kutoka ulimwenguni yaonekana kujumlisha matukio mawili pamoja.

Ukurasa mwingine wa maana wa wakati wa unyakuzi ni Ufunuo Wa Yohana 3:10 ambapo Kristo anaahidi kuwaokoa wateule kutoka “saa ya matezo” ambayo yatakujia ulimwengu. Hii inaweza maanisha mambo mawili. Kristo atawalinda wateule wakati wa matezo, au atawaokoa wateule kutoka kwa matezo. Yote yana maana inayoweza kuaminika wa neno la Kiyunani (Kigiriki) ambalo limetafsiriwa “kutoka.” Ingawa ni muimu kutambua chenye wateule wameahidiwa watachungwa kutoka. Si majaribio pekee, bali “saa” ya majaribu. Kristo anaahidi kuwaweka wateule kuanzia ile saa ya majaribu, iitwayo matezo. Lengo la matezo, lengo la unyakuzi, maana ya 1 Wathesalonike 5:9, na ufafanuo wa Ufunuo Wa Yohana 3:10 yote yanaunga wazi matezo kabla ya. Ikiwa Bibilia anaweza elezewa juujuu basi matezo kabla ya unyakuzi itakua fafanuo ya kibibilia.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Unyakuzi utatokea lini ukiambatana na matezo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries