Swali
Kwa nini Mungu aliamuru uharibifu / mauaji ya Wakanaani, wakiwemo wanawake na watoto?
Jibu
Katika 1 Samweli 15: 2-3, Mungu aliamuru Sauli na Waisraeli, "Bwana MUNGU asema hivi: Nitawaadhibu Waamaleki kwa sababu waliwapiga walipokuwa wanatoka Misri. Sasa nenda, ukawashambulie na kuangamiza vitu vyotewalivyo navyo. Usiwaacha hai ila uwauwe wote; wanaume kwa wanawake, watot wachanga na wanyonyao, kondoo, ngamia na punda. " Mungu aliamuru mambo kama hayo wakati Waisraeli walipokuwa wakiingia nchi iliyoahidiwa (Kumbukumbu la Torati 2:34, 3: 6, 20: 16-18). Kwa nini Mungu aiwaamuru Waisraeli kuangamiza kundi lote la watu, wanawake na watoto?
Hili ni suala ngumu. Hatuelewi kwa nini Mungu angeamuru kitu hicho, lakini tunamwamini Mungu kwamba Yeye ni wa haki — na tunatambua kwamba hatuwezi kuelewa kikamilifu Mungu mwenye nguvu, Mungu wa milele. Tunapoangalia masuala magumu kama haya, tunapaswa kukumbuka kwamba njia za Mungu ni za juu kuliko njia zetu na mawazo yake ni ya juu kuliko mawazo yetu (Isaya 55: 9; Warumi 11: 33-36). Tunapaswa kuwa na nia ya kumwamini Mungu na kuwa na imani ndani yake hata wakati hatuelewi njia zake.
Tofauti na sisi, Mungu anajua yajao, mambo yatakayotendeka. Mungu alijua matokeo yatakavyokuwa kama Israeli hakuwaangamiza kabisa Waamaleki. Ikiwa Waisraeli hawakufanya amri za Mungu, Waamaleki wangerudi kuwasumbua Waisraeli katika siku zijazo. Sauli alidai kuwa ameuawa kila mtu ila tu mfalme Waamaleki Agagi (1 Samweli 15:20). Kwa wazi, Sauli alidanganya. Miaka michache baadaye, kulikuwa na Waamaleki wa kutosha kuchukua Daudi na familia za wanaume wake mateka (1 Samweli 30: 1-2). Baada ya Daudi na watu wake kushambulia Waamaleki na kuokoa familia zao, Waamaleki 400 walikimbia. Ikiwa Sauli alikuwa ametimiza yale aliyoamuru Mungu, haya hayangetokea. Miaka mia kadhaa baadaye, mjukuu wa Agagi, Hamani, alijaribu kuwaangamiza watu wote wa Kiyahudi (tazama kitabu cha Esta). Hivyo, utii usio kamili wa Sauli ulikuwa umesababisha uharibifu wa Israeli. Mungu alijua hili litatokea, kwa hiyo aliamuru uangamizaji wa Waamaleki kabla ya wakati.
Kwa upande wa Wakanaani, Mungu aliamuru, "Katika miji ya ya nchi ambayo Mwenyezi Mungu , Mungu wenu, anawapeni, msisalimishe chochote. Mtawaangamiza watu wote: Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi – kama Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyoamuru. Wasije wakawafundisha desturi zao za kuchukiza ambazo waliifanyia Muingu yao, nanyi mkatenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. "(Kumbukumbu la Torati 20: 16-18). Waisraeli walishindwa katika utume huu pia, na kile ambacho Mungu alisema kitatokea (Waamuzi 2: 1-3, 1 Wafalme 11: 5, 14:24; 2 Wafalme 16: 3-4). Mungu hakuagiza ungamizaji wa watu hawa kwa ukatili, lakini kuzuia uovu hata mkubwa zaidi kutokea katika siku zijazo.
Pengine sehemu ngumu zaidi ya amri hizi kutoka kwa Mungu ni kwamba Mungu aliamuru kifo cha watoto na watoto wachanga pia. Kwa nini Mungu aliagiza kifo cha watoto wasio na hatia? (1) Watoto wanahatia (Zaburi 51: 5; 58: 3). (2) Watoto hawa wangeweza kukua kama wafuasi wa dini mbaya na mazoea ya wazazi wao. (3) Kwa kumaliza maisha yao kama watoto, Mungu aliwawezesha kuingia mbinguni. Tunaamini kabisa kwamba watoto wote wanaokufa wanakubalika mbinguni kwa neema na huruma ya Mungu (2 Samweli 12: 22-23; Marko 10: 14-15; Mathayo 18: 2-4).
Jibu hili halisuluishi kabisa na masuala yote. Lengo letu linapaswa kuwa kumwamini Mungu hata wakati hatuelewi njia zake. Pia tunapaswa kukumbuka kwamba Mungu anaangalia mambo kutoka kwa mtazamo wa milele na kwamba njia zake ni za juu kuliko njia zetu. Mungu ni mwenye haki, mtakatifu, mwenye upendo, mwenye huruma, na mwenye neema. Jinsi yeye hufanya kazi pamoja inaweza kuwa kama siri kwetu sisi lakini yeye haimaanishi kwamba Yeye sio ambaye Biblia inamtangaza kuwa.
English
Kwa nini Mungu aliamuru uharibifu / mauaji ya Wakanaani, wakiwemo wanawake na watoto?