Swali
Je, kwa nini Mungu huuliza mwaswali ikiwa Yeye anajua kila kitu?
Jibu
Mungu anajua kila kitu. Tunaona pia katika maandiko Mungu akiuliza maswali. Katika Bustani ya Edeni, Mungu anamwuliza Adamu mahali yupo na kile alichokifanya (Mwanzo 3:9, 11). Akiwa mbinguni anamwuliza shetani mahali ambapo amekuwa (Ayubu 1:7). Jangwani, Mungu anamwuliza Musa nini anachoshika mkononi mwake (kutoka 4:20). Yesu alipokuwa katika umati wa watu akielekea nyumbani kwake Yairo, aliuliza ni nani amabaye alimguza (Marko 5:30). Mungu anajua yote, na alikuwa tayari anajua majibu ya maswali haya. "Maana ndiye azijuaye siri za moyo" (Zaburi 44:21). Kwa nini basi anauliza?
Maswali ambayo Mungu huuliza huwa na kusudi. Yeye huwa haulizi ili kupata habari, kwa sababu ana maarifa yote. Maswali yake huwa na kusudi tofauti, na kusudi hilo hutofautiana kulingana na muktadha wa mahitaji ya yule ambaye ameulizwa swali.
Baada ya Adamu na Awa kula tunda lililokatazwa na kijificha kutoka kwa Mungu, Mungu aliitana, "Uko wapi?" (Mwanzo 3:9). Kwa kweli, Mungu alijua mahali Adamu alipokuwa; hiyo haikuwa hoja ya swali hiyo. Swali hilo lililenga kumtoa Adamu mafichoni. Mungu angejongea viumbe wake wahalifu kwa hasira, maneno makali ya kulaani na hukumu, lakini hakufanya hivyo. Badala yake, alimwendea Adamu kwa swali na kuonyesha neema yake, upole na hamu ya maridhiano.
Wakati wakufunza mwanafunzi hesabu, mwalimu anaweza kuuliza, "2+2 itakuwa ngapi ?" Mwalimu haulizi kwa sababu hajui jibu lake lakini ni kwa sababu anataka mwanafunzu kufikiria kuhusu suluhisho la hesabu hilo. Wakati Mungu alipouliza Adamu, "Uko wapi?" kusudi la swali hilo lilikuwa kumfanya Adamu kulenga tatizo lililokumkumba pamoja na mke wake.
Maswali mengine ya Mungu katika maandiko yanaweza kuwa na madhumuni mengine. Katika Ayubu 38-41, Mungu anamwuliza Ayubu kuhusu mahali alipokuwa wakati Mungu alipokuwa anaiweka misingi ya dunia (Ayubu 38:4) pia anauliza Ayubu kuhusu kukosa uwezo wa kumvua mamba kwa ndoana (Ayubu 41:1). Hapa, ni dhahiri kwamba Mungu anatumia maswali zana ya kufundisha na kusistiza nguvu zake na ukuu wake.
Mungu alirudia kumwuliza Yona, "Je, unatenda vyema kukasirika?" (Yona 4:4,9) swali ambalo lililenga kumfanya Yona kujichunguza. Swali lake Mungu kwa Eliya, "Unafanya nini hapa?" ( 1 Wafalme 19:9) lilionyesha jinsi Eliya alikuwa anaepuka kusudi la Mungu kwakwe. Swali la Mungu mbele ya Isaya, "Nimtume nani? Nani atakayekwenda kwa ajili yetu?" (Isaya 6:8) lilikusudia kumfanya nabii ajitolee.
Wakati wa huduma ya Yesu hapa duniani, mara nyingi aliuliza maswali. Mwalimu mwema hutumia maswali yakimkakati ili kuwezesha mchakato wa mafunzo, na Yesu alikuwa Mwalimu Mkuu. Wakati mwingine Yesu aliuliza maswali ili kuweka fursa ya kujifunza: "Watu wanasema mimi ni nani?"(Marko 8:27). Au pia kuwafanya wasikilizaji wake kuwa na umakini juu ya jambo muhimu: "Imeandikwa nini katika sheria?...Unaelewaje?" (Luka 10:26). Au pia kuchochea kujiangalia nafsi. "Je, unataka kupona?" (Yohana 5:6) Au pia, kuchochea fikra zaidi: "Maana yake ni nini basi neno hili lililoandikwa, jiwe walilokataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni?" (Luka 20:17). Au kuelezea imani: "Ni nani aliyenigusa?" (Luka 8:45). Au kufanya ufunuo mkubwa: "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" (Yohana 20:15).
Mungu ni Baba anayetumia lugha kufunza katika muktadha wa uhusiano. Yeye ni mwalimu ambaye anatumia maswali kuwashirikisha wanafunzi wake, kuwalazimisha kufikiria, au kuwaelekeza kwa ukweli. Wakati anapouliza swali, sio kwa sababu Yeye hajui jibu lake lakini ni kwa sababu anataka sisi tujue.
English
Je, kwa nini Mungu huuliza mwaswali ikiwa Yeye anajua kila kitu?