Swali
Je, modalizimu/ mfumo wa kifalme wa Mungu ni nini?
Jibu
Modalizimu na mfumo wa kifalme wa Mungu ni maoni mawili ya uongo juu ya asili ya Mungu na ya Yesu Kristo ambayo ilionekana katika karne ya pili na ya tatu AD. Mtazamo wa modalisti ni kwamba anaona Mungu kama Mtu mmoja badala ya Watu watatu na anaamini kwamba Baba, Mwana, na Roho ni Watu tofauti au aina za Mtu huyo mmoja wa Kiungu. Kwa mujibu wa modalizimu, Mungu anaweza kubadilika kati ya maonyesho matatu tofauti. Monakia huamini katika umoja wa kiungu (neno la Kilatini monarchia linamaanisha "utawala mmoja") na inapelekea kuasi hali ya Mungu ya tatu. Modalizimu na Mfumo wa kifalme wa Mungu hushikilia kwa mafundisho ambayo husema kwamba Mungu Baba aliteseka msalabani na (au kama) Mwana. Ni mafundisho ambayo inakaribiana na Sabelianizimu.
Mfumo wa kifalme wa Mungu ilichukua aina mbili za msingi, mojawapo huamini kuwa Kristo alikuwa mtu wa kawaida aliyezaliwa kimiujiza na nyingine ambayo hufundisha ufalme mmoja wa Mungu. Mtazamo hu wa Kristo kama mtu tu ulianza kwa mtazamo usio sahihi wa asili wa Yesu, hasa, kwamba Yeye si Mungu lakini alikuwa, wakati wa ubatizo wake, alipewa nguvu na Mungu kufanya maajabu aliyofanya. Mtazamo wa ufalme mmoja wa Mungu, kwa upande mwingine, ulichukua mtazamo wa kawaida kwamba Yesu alikuwa Mungu, lakini tu kwa sababu ya kwamba Yesu alikuwa mmoja wa "kujidhihirisha" ya Mungu. Kulingana na mtazamo wa ufalme mmoja wa Mungu, utatu wa Mungu hauna tofauti, sio wa kibinafsi mwenyewe. Maneno ya kibiblia Baba, Mwana, na Roho ni majina tofauti tu kwa Mtu mmoja, kulingana na wanaoshikilia mtazamo huo.
Mtazamo wa ufalme wa Mungu Mmoja unafundisha kwamba umoja wa Mungu hauhusiani na tofauti ya Watu ndani ya Uungu. Kwa mujibu wa modalizimu, Mungu amejidhihirisha kwa njia mbalimbali kama Baba (hasa katika Agano la Kale), kama Mwana (hasa kutoka Yesu alipokuwa tumboni mwa mama yake hadi kupaa kwake), na kama Roho Mtakatifu (hasa baada ya Yesu kupaa mbinguni). Mfumo wa ufalme mmoja wa Mungu una mizizi katika mafundisho ya uwongo ya Noetus ya Smirna karibu AD 190. Noetus alijiita Musa na kumwita ndugu yake Haruni, na alifundisha kwamba, ikiwa Yesu alikuwa Mungu, basi lazima awe sawa na Baba. Hippolytus wa Roma alipinga uongo huu katika " Contra Noetum" yake. Aina ya mwanzo ya mzatamo wa ufalme mmoja wa Mungu pia ulifundishwa na kuhani kutoka Asia Ndogo aitwaye Praxeas, ambaye alisafiri Roma na Carthage karibu AD 206. Tertullian alipinga mafundisho ya Praxeas katika "Adventus Praxean" karibu 213. Mtazamo wa ufalme mmoja wa Mungu na dini zake zinazohusiana pia zilikanushwa na Origen, Dionysius wa Alexandria, na Baraza la Nicea mnamo 325.
Aina ya ufalme wa Mungu mmoja bado upo leo katika Pentekoste ya umoja. Katika teolojia ya umoja, ambayo ni hupinga Utatu, hakuna tofauti kati ya Watu wa Uungu. Yesu ni Mungu, lakini pia ni Baba na Roho. Kwa kupotoka kidogo kutoka kwa mfumo wa kale, Wapentekoste wa umoja hufundisha kwamba Mungu anaweza kujidhihirisha Mwenyewe katika "hali" zote tatu wakati huo huo, kama vile katika ubatizo wa Yesu katika Luka 3:22.
Biblia inaonyesha kwamba Mungu ni Mungu mmoja (Kumbukumbu la Torati 6: 4), lakini inazungumzia watu watatu-Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19). Jinsi wanavyounganika haiwezekani kwa akili ya kibinadamu. Tunapojaribu kuelewa hushindwa kuelewa. Lakini Maandiko ni wazi: Mungu yupo katika watu watatu wa milele, ambao ni sawa. Yesu alimwomba Baba yake (Luka 22:42) na sasa ameketi katika mkono wa kulia wa Baba mbinguni (Waebrania 1: 3). Baba na Mwana walituma Roho ulimwenguni (Yohana 14:26; 15:26). Mtazamo wa ufalme mmjoa wa Mungu ni hatari kwa kiroho kwa sababu unashambulia asili ya Mungu. Mafundisho yoyote ambayo haitambui Mungu kama watu watatu tofauti ni kinyume cha Biblia.
English
Je, modalizimu/ mfumo wa kifalme wa Mungu ni nini?