Swali
Ni mfumo upi sahihi wa ubatizo?
Jibu
Jibu rahisi sana kwa Swahili linapatika katika maana ya neno “kubatiza." Linatoka kwa neon la kiyunani linalomaanisha “kuzama katika maji." Kwa hivyo, ubatizo wa kunyunyiza au wa kumwagia sio wa halali, jambo ambalo linajipinga binafsi. Ubatizo kwa kunyunyiza waweza maanishaa " kuzamisha mtu katika maji kwa kunyunyizia maji juu yao." Ubatizo, kwa ufafanuzi wke wa asili, ni lazima uwe ni kitendo cha kuzamishwa kwenye maji.
Ubatizo unaeleza kijitambulisha kwa waumini na kifo cha Kristo, kuzikwa, na kufufuka kwake. "Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatzwa katika Kristo Yesu tulibatzwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusidi kama Krisot alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima" (Warumi 6:3-4). Hatua ya kuzamishwa katika maji ni taswira ya kufa na kuzikwa na Kristo. Hatua ya kuja nje ya maji unaeleza ufufuo wa Kristo. Matokeo yake, ubatizo kwa kuzamisha ni njia pekee ya ubatizo ambayo unaeleza kuzikwa pamoja na Kristo na kufufuka pamoja naye. Ubatizo kwa kunyunyiza / au kwa kumwagia unafanyika kwa sababu ya mazoea yasio ya kibiblia ya Ubatizo wa watoto wachanga.
Ubatizo kwa kuzamisha, huku ukuwa ndio mfumo wa Biblia mfumo wa kujitambulisha na Kristo, si (kama baadhi ya wengine huamini) sharti kwa wokovu. Na badala ni tendo la utii, matangazo ya imani katika Kristo na kitambulisho pamoja naye. Ubatizo ni picha ya kuacha maisha yetu ya zamani na kuwa kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17). Ubatizo kwa kuzamisha ndio mfumo pekee ambao kikamilifu unaeleza haya mabadiliko makubwa.
English
Ni mfumo upi sahihi wa ubatizo?