settings icon
share icon
Swali

Je, ni mtazamo wa Biblia juu ya migogoro ya kinyumbani ni upi?

Jibu


Vurugu za kijamii zimeelezewa kwa kifupi kama tendo au vitendo la tishio la ukatili kwa mtu ambaye mhalifu huyo amekuwa na uhusiano wa karibu kimapenzi naye. Mara nyingi unyanyasaji wa kijamii huleta mawazo ya "mke aliyepigwa" au labda wanandoa kujibisana kwa maneno katika ndoa kunamalizia mapigano. Vurugu za za jamii pia huhusishwa na unyanyasaji wa watoto. Hata kama watoto hawajeruhiwi, kuona au kusikia mzazi akijeruhiwa inaweza kuwa na madhara makubwa ya kisaikolojia.

Vurugu za kijamii huwa juu ya kutaka kuwa na nguvu na udhibiti. Ijapokuwa vurugu ya neno ina maelezo ya kimwili, unyanyasaji wa nyumbani au unyanyasaji unaweza kutokea kwa njia zisizo za kimwili. Kwa mfano, waathiri wanaweza kukandamiza waathiriwa kwa njia ya kihisia au kiuchumi. Unyanyasaji wa maneno na unyanyasaji wa kijinsia ni aina nyingine. Mtu wa umri wowote, jinsia, darasa la kijamii na kiuchumi, ngazi ya elimu, au dini anaweza kuathiriwa na unyanyasaji wa kijamii.

Dhuluma za kijamii zinaweza kutazamwa kwa mujibu wa "mzunguko wa vurugu." Mvutano hujibuka; mhasiri akijaribu kumfanya mhadhiriwa ateseke; lakini, hatimaye, tukio linatokea. Mtuhumiwa anaomba msamaha na anajaribu kumwahidi mwathiriwa, labda kwa kuahidi kuwa haitatokea tena au kwa kumtunukia yule aliyeathiriwa na zawadi. Kisha inakuja kipindi cha utulivu kabla ya mvutano kuanza tena. Hatua za mzunguko huu zinaweza kuchukua dakika moja au inaweza kukua zaidi ya miaka. Bila kuingilia upatanisho wowote muda wa "maridhiano" na "utulivu" mara nyingi hutoweka.

Mizozo ya kijamii ni kinyume kabisa na mpango wa Mungu kwa familia. Mwanzo 1 na 2 zinaonyesha ndoa kama mwili mmoja, uhusiano wa kusaidiana. Waefeso 5:21 inazungumzia juu ya kunyenyekea wao kwa wao. Waefeso 5: 22-24 inaelezea utii wa mke kwa mumewe, huku mistari ya 25-33 inazungumzia upendo wa kujitolea wa mume kwa ajili ya mkewe. Waraka Wa Kwanza Wa Petro 3: 1-7 inatoa maelekezo sawa. Wakorintho Wa Kwanza 7: 4 inasema, "Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe" Wao wawili ni wa kila mmoja na wameunganiswa kupendana kama vile Kristo alivyotupenda. Ndoa ni mfano wa Kristo na Kanisa. Mzozo wa kijamii sio kitu kilicho karibu na tabia ya Yesu.

Mzozo wa familia unaowahusisha watoto pia unakashifiiwa na Mungu. Zaburi 127: 3 inasema, "Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu." Mungu anawapa wazazi watoto, na wazazi hao wanastahili kuwalea kwa upendo na kuwafundisha. Waefeso 6: 4 inasema, "Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana" (angalia Wakolosai 3:21). Watoto wanapaswa kuwatii wazazi wao (Waefeso 6: 1-3), na nidhamu ni muhimu. Lakini nidhamu ni tofauti kabisa na vurugu na unyanyasaji.

Kumfuata Mungu kunahusisha kuwatumikia wengine, si kuwaongoza kimabafu na kuwadhibiti. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" (Mathayo 20: 26-28). Amri yake kwetu ni "kupendana" (Yohana 13:34). Waefeso 5: 1-2 inasema, "Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato." Wakristo wameitwa ili kuwapenda wengine kwa kujitolea, hasa wale wa familia zao.

Wale ambao kwa sasa wako katika hali ya mizozo ya nyumbani wanapaswa kufanya kila kitu iwezekanavyo ili wapate kutoka kwa ndoa kwa usalama. Mara nyingi, wakati hatari zaidi kwa mhasiriwa wa unyanyasaji wa ndoa ni wakati yeye anaamua kutoka. Kuwasiliana na polisi kunaweza kusiwe na usaidizi, au kunaweza kuwa na usaidizi mwingine hapo karibu naye. Nchini Marekani, nambari ya Taifa ya Vurugu ya Ukatili inaweza kusaidia kwa habari na rasilimali. Nambari yao ni 1-800-799-7233. Wanaweza pia kupatikana mtandaoni kwenye http://www.thehotline.org/ (KUMBUKA: matumizi ya tarakilishi yanaweza kufuatiliwa, kwa hiyo tembelea tovuti hizi tu ikiwa mkosaji hana njia ya kufuatilia shughuli zako mtandaoni). Wakati unyanyasaji wa jamii unaendelea, usalama ni hatua ya kwanza.

Hata baada ya waathiriwa wana usalama wa kimwili na maumivu ya kimwili yamepona, makovu ya kihisia na ya kisaikolojia hubaki. Vurugu za jamii zinaweza kuwa na madhara makubwa ya kiroho pia. Waathiriwa wanaweza kosa kumwamini Mungu. Kwa nini ataruhusu jambo kama hilo lifanyike? Je, anaaminika? Je, ananipenda? Alikuwa wapi wakati nilipokuwa nateswa? Kutembea kwa njia ya mchakato wa uponyaji inachukua muda. Tabia ya kihisia ya hali hiyo inakuja. Ni sahihi kueleza hasira juu ya unyanyasaji. Ikiwa hatuitikii ukali wa hali hiyo-hasira, kuchanganyikiwa, madhara, aibu, nk — hatuwezi kuponya kutoka kwao. Mara nyingi, waathiriwa wamepangwa mapema kwa msamaha. Hatimaye, msamaha ni jambo ambalo litaweka mwathiriwa huru. Lakini msamaha wa kweli hauwezi kupanuliwa ikiwa makovu ya unyanyasaji haukubaliwa kwanza na kushughulikiwa. Waathiriwa wa unyanyasaji wa ndani watahitaji msaada wa mshauri mzuri wa Kikristo wa kutembea nao katika mchakato wa uponyaji.

Hatupaswi kudhani kwamba wakamaizaji hawana mahitaji mengine kuliko kuacha kudhumu wengine. Kuna uwezekano wa masuala ambayo hayajafumbuliwa ambayo yamewasababisha kuwa wakatili. Ikiwa mwanyanyasaji anakubali kkuitikia makosa yake na matamanio yake, kuna matumaini. Tena, ushauri wa Kikristo unaweza kuwa wa thamani sana.

Hadithi ya kila unyanyasaji wa jamii ni tofauti. Hali na watu ni tofauti sana kwamba hakuna kitu kimoja kinaweza kushughulikia suala hilo kwa kutosha. Hata hivyo, kwa ujumla, ushauri wa ndoa sio suluhisho sahihi-angalau hata wakati wote unyanyasaji umekoma, wote wawili wamepata ushauri wa kibinafsi, na pande zote mbili hutaka upatanisho. Vilevile ni kweli kwa tiba ya familia. Watoto hawapaswi kamwe kuingizwa katika hali mbaya au wanatarajia kubaki wakati kwa mmoja huku mkosaji anajifunza uzazi wa kiungu.

Mzozo wa kijamii huumiza moyo wa Mungu. Yeye hasawishiki na waathiriwa wake, wala Yeye amewaacha. Mpango wake wa mahusiano ya kibinadamu-hasa wale kati ya familia-ni mfano mzuri unaonyesha Yeye ni nani. Familia inapaswa kuangaza upendo wa Mungu. Ni huzuni wakati ndoa inakuwa mahali pa maumivu. Tamanio la Mungu kwa wale wanaohusika na unyanyasaji wa kijamii-wote waasiri na waathiriwa-ni uponyaji na utele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni mtazamo wa Biblia juu ya migogoro ya kinyumbani ni upi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries