settings icon
share icon
Swali

Je! Mihuri saba katika ufunuo ni gani?

Jibu


Mihuri saba ni mojawapo wa msururo wa hukumu za nyakati za mwisho kutoka kwa Mungu. Mihuri hiyo imeelezewa katika Ufunuo 6: 1-17 na 8: 1-5. Katika maono ya Yohana, mihuri hiyo saba inashika hati iliyofungu mbinguni, na, kila muhuri unapovunjwa, hukumu mpya inaachiliwa duniani. Kunachofuata hukumu za muhuri ni hukumu za parapanda na hukumu za bakuli.

Utangulizi wa kufunguliwa kwa mihuri saba katika maono ya Yohana ni utafutaji wa mtu anayestahili kukifungua kitabu cha mbinguni katika Ufunuo 5. Yohana anaandika, "Kisha nikaona katika mkono wake wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nje, kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba" (Ufunuo 5: 1). Kitabu hiki kina hukumu za Mungu; ukweli kwamba kimeandikwa pande zote mbili inaonyesha hali ya kina ya hukumu inayosubiri. Malaika hodari anapaza sauti, "Ni nani anayestahili kuzivunja hizo lakiri na kukifungua kitabu?" (Ufunuo 5: 2). Hakuna mtu aliyepatikana anastahili kuvunja mihuri na kufungua kitabu, jambo linalosababisha Yohana kuomboleza (Ufunuo 5: 3-4). Ikiwa hati haingeweza kufunguliwa, basi uovu haungehukumiwa na uovu ungeendelea kuathiri dunia.

Yohana anapolia juu hati ambayo haijafunguliwa na muhuri wake kuvunjwa, anapokea habari njema: "Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba" (Ufunuo 5:5). "Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa… Huyo Mwana-Kondoo akaja na kukitwaa kile kitabu kutoka kwenye mkono wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi" (Ufunuo 5:6-7). Hii ni taswira ya Yesu Kristo, Kondoo ambayo ilichinjwa ambaye pia ni Simba wa hukumu. Yesu ndiye pekee anastahili kuhukumu ulimwengu (linganisha Yohana 5:22). Anapochukua hati hiyo ili kufungua mihuri na kutangaza hukumu juu ya ulimwengu usio amini, viumbe mbinguni wanamtukuza Yeye kwa wimbo mpya:

"Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa…Anastahili Mwana-Kondoo, yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!" (Ufunuo 5:9,12).

Katikati ya ibada inayostahili Yeye, Mwanakondoo anaanza kufungua mihuri (Ufunuo 6: 1). Kila muhuri ukifunguliwa, gombo linaweza kufunuliwa kidogo zaidi, likifunua hatua kwa hatua hukumu ambazo Mungu ameweka kwa ajili ya kipindi cha dhiki. Mihuri minne ya kwanza kati ya ile saba inaachilia kile kinachojulikana kama Wapanda farasi Wanne wa Ufunuo, kwa sababu hukumu inaonekana kuwa ishara kama farasi na mpanda farasi akileta uharibifu katika kuamka kwake.

Muhuri wa kwanza. Muhuri wa kwanza unamtambulisha Mpinga Kristo (Ufunuo 6: 1-2). Kutoka kwa maelezo ya kibiblia, tunakusanya maelezo kadhaa: yeye hupanda farasi mweupe, ambaye anazungumza juu ya amani; mwanzoni mwa dhiki, Mpinga Kristo atakuja chini ya uwongo wa kuleta amani ulimwenguni (taz. Danieli 9:27). Amepewa taji, ambayo inaonyesha kwamba Mpinga Kristo atakuwa na mamlaka makubwa (rej. Danieli 7: 24-25). Anashika upinde, ambao unaonyesha nia yake ya kweli, na anavyozidi kuwa "mshindi aelekeaye katika kushinda" (Ufunuo 6: 2).

Muhuri wa pili. Wakati Mwanakondoo anafungua muhuri wa pili, vita vikuu vinatokea duniani (Ufunuo 6:3-4). Hii inaonesha ishara kuwa mpanda farasi na upanga juu ya farasi mwekundu.

Muhuri wa tatu. Kuvunjwa kwa muhuri wa tatu kati ya ile saba unasababisha njaa (Ufunuo 6:5-6). Mpanda farasi ambaye Yohana anamwona anaendesha farasi mweusi na "mizani mkononi mwake." Alafu Yohana anasikia tangazo kuu kwamba watu watafanya kazi mchana kutwa ndio wapate angalau chakula kidogo.

Muhuri wa nne. Lakiri la nne linafunguliwa, na Yohana anaona farasi wa kijivujivu. "Mauti, naye Kuzimu alikuwa akimfuata nyuma yake kwa karibu" (Ufunuo 6:7-8). Matokeo ya muhuri huu wa nne ni kwamba theluthi moja ya idadi ya watu duniani wanauawa "kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia."

Muhuri wa sita. Muhuri wa tano wa kitabu hicho unaonyesha wale ambao watauawa kwa imani yao katika Kristo wakati wa dhiki (Ufunuo 6: 9-11; taz. Mathayo 24: 9). Nafsi za wale waliouawa zinataswiriwa kuwa kudumu katika madhabahu mbinguni. Mungu anasikia kilio chao cha haki, na kumpa kila mmoja wao joho jeupe. Mashahidi hao wanaambiwa wasubiri "mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia." Mungu anaahidi kulipiza kisasi, lakini wakati haukuwa imetimia bado (ona Warumi 12:19).

Lakiri la sita. Wakati Mwanakondoo wa Mungu anafungua lakiri la sita, mtetemeko mkuu unatokkea, na kusababisha uharibifu mkubwa na machafuko mamabya -pamoja na matukio ya kawaida ya angani: jua linageuka kuwa nyeusi, na mwezi unakuwa mwekundu kama damu, na "Anga ikatoweka kama vile karatasi isokotwavyo, na kila mlima na kila kisiwa kikaondolewa mahali pake" (Ufunuo 6: 12–14). Manusura wa muhuri wa sita, bila kujali msimamo wao kijamii, wanakimbilia mapangoni na kulilia milima na miamba, "Wakaiita milima na miamba wakisema, "Tuangukieni, mkatufiche na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi, na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo! Kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imewadia. Je, ni nani awezaye kustahimili?" (Ufunuo 6: 16-17).

Baada ya kufungua muhuri wa sita kati ya ile saba kuna pumziko katika kitabu cha Ufunuo. Yohana anawaelezea Wayahudi 144,000 ambao watakingwa wakati wa dhiki (Ufunuo 7:1-8). Baadaye, anaona mbinguni "na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo" (Ufunuo 7:14). Watu hawa wamefaa nguo nyeupe, wakiwa wameshika matawi ya mitende na wakipasa sauti:

"Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo" (Ufunuo 7:10). Yohana anaambiwa umati huu wenye nguo nyeupe ni: "Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa" (Ufunuo 7:14). Wamepewa ahadi kuwa "'Kamwe hawataona njaa wala kiu tena. Jua halitawapiga wala joto lolote liunguzalo...Naye Mungu atafuta kila chozi kutoka macho yao" (Ufunuo 7:16-17; linganisha na Isaya 25:8; 49:10).

Muhuri wa saba. Wakati Mwanakondoo anafungua muhuri wa saba, "pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa" (Ufunuo 8:1). Hukumu ambayo inaelekeza katika kukamilika kwa dhiki sasa zinaonekana katika hati ya kuviringisha na ni kali mno kiwango kwamba kimya kitatanda mbinguni kwote. Lakiri ya saba kwa wazi inafungulia msururo wa hukumu, maana Yohana anaona papo hapo malaika saba ambao wamepewe tarumbeta saba wakiwa karibu kuzipuliza (Ufunuo 8:2). Malaika wa nane anachukua chetezo na kuchoma "uvumba mwingi" na ndani yake ilikuwa inawakilisha maombi ya watu wa Mungu (Ufunuo 8:3-4). Malaika bado anachukua chetezo kile kile, "akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la ardhi" (Ufunuo 8:5).

Pindi tu hukumu saba za muhuri zitakapomalizika, sehemu inayofuata ya dhiki, inaonyesha hukumu saba za tarumbeta, iko tayari kuanza.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mihuri saba katika ufunuo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries