settings icon
share icon
Swali

Tutakuwa na miili ya kimwili Mbinguni?

Jibu


Ijapokuwa Biblia inatuambia machache juu ya jinsi itakavyokuwa mbinguni, inaonekana kwamba tutaweza kuwa na mwili wa kimwili, ingawa si kwa maana sawa ya "mwili" tuliyo nayo sasa. Wakorintho wa kwanza 15:52 inasema kwamba "wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu," na kwamba wale walio hai wakati wa kurudi kwa Kristo kwa ajili ya watakatifu Wake "watabadilishwa." Yesu Kristo ni "mzaliwa wa kwanza" wa wale waliokufa (1 Wakorintho 15:20, 23). Hii ina maana kwamba Yeye ameweka mfano na anaongoza njia. Wakorintho wa Kwanza 15:42 inasema kwamba miili yetu "Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika." Katika mtangulizi wa ufufuo wa waumini, wengine walifufuliwa wakati wa ufufuo wa Kristo katika Mathayo 27:52 ambapo inasema kwamba "miili yao" ilifufuliwa. " Thomas, katika Yohana 20:27, alialikwa kuugusa mwili wa Kristo baada ya ufufuo wake, kwa hiyo Yeye alikuwa na mwili ulio imara.

Tunaweza kutarajia kuwa miili yote ya ufufuo wa waumini itakuwa kama ule wa Kristo. Ni ukweli wa ajabu ulioje! Biblia haisingatii hili hasa, lakini inaonekana kwamba tutaweza kula. Yohana, katika Ufunuo 22: 2, anaandika juu ya maono yake ya hali ya milele ambapo aliona kuwa "katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi..." Hii inaonekana kuwa ni mabadiliko ya adhabu ya Mwanzo 3 ya Adamu na Hawa, na hivyo wanadamu wote, walizuiliwa kula kutoka kwa mti huu. Kwa sababu ya njaa, inaonekana kuwa hakutakuwa na yoyote. Isaya 49:10 inasema kuwa hakutakuwa na njaa au kiu katika ufalme wa milenia. Hii inazungumzia wanadamu wakati wa kipindi hicho, sio watakatitifu waliobadilishwa, bali kwa ugani unaweza kusema kwamba ikiwa wanadamu duniani wakati wa Ufalme wa Kristo hawatahisi njaa, hakika hakutakuwa na njaa mbinguni (angalia pia Ufunuo 7:14 -16).

Hatimaye, Ayubu aliandika kwamba alijua kwa hakika kwamba hata baada ya kufa na ngozi yake imekwisha kupita, kwamba "katika MWILI wangu nitamwona Mungu" (Ayubu 19:26 – herufi kubwa zote ziliongezwa kwa msisitizo). Kwa hiyo hiyo inamaanisha miili yetu itakuwa na aina fulani ya mwili wa utukufu. Kila aina tuliyo nayo, tunajua kuwa itakuwa kamilifu, isiyo na dhambi, na isiyo na maana.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutakuwa na miili ya kimwili Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries