settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kuwa mke wa kiungu?

Jibu


Ili kufafanua mke wa kiungu, lazima kwanza tuchunguze maana ya neno la kiungu. Katika 1 Timotheo 2: 2, Paulo analitumia neno hilo sawia na kuwa "wa amani," "mtulivu," na "mwenye heshima." Biblia inasema Roho, ambaye yuko ndani ya kila muumini, hutoa matendo inayoonekana na yasiyoonekana ya utakatifu, "upendo furaha, amani, uvumilivu, wema, wema, uaminifu, upole, udhibiti" (Wagalatia 5: 22-23). Ufafanuzi halisi wa utakatifu utakuwa "Ukristo." Uungu unahusisha jitahida za kweli za kumuiga Kristo, kuwa kama Yeye katika mawazo na matendo kama mtume Paulo anavyojitahidi kuwa (1 Wakorintho 11: 1). Hizi nyenzo za tabia ya kiungu zinahusu kila muumini, iwe ni wa kiume au kike. Kwa bahati nzuri, Biblia inatoa sifa maalum zaidi juu ya kile mwanamke mwenye kumcha Mungu-hasa, mke wa kiungu-anapaswa kuonekana.

Katika kitabu cha Mithali, kuna neno la picha nzuri la mke wa kiungu. Uzuri wa mke wa Mungu haujabadilika, hata zaidi ya maelfu ya miaka. Mke wa kiungu ni mtu ambaye ana imani kamili kwa mumewe. Hana haja ya kuwa na wasiwasi kwamba atakuwa akijaribiwa na malengo ya mtu mwingine, kulipia kadi za mkopo, au kutumia kila siku kuangalia vipindi vya video. Anajua yeye ni wa heshima, hekima, na kujitolea (Methali 31:11, 12, 25, 26). Anaamini msaada wake na upendo wa dhati kwa sababu hawezi mhukumu au kumdadisi. Mumewe ana sifa nzuri katika jamii, na mkewe hazungumzii mabaya kumhusu, kamwe humsengenyi. Badala yake, yeye daima humwinua na kumpa sifa. Anaweka familia kabisa na anajiheshimiwa mwenyewe (Mithali 31:12, 21, 23).

Mke wa kiungu hutumia muda mfupi mbele ya kioo kuliko vile anavyoshiriki mali zake na masikini na walio na mahitaji kwa sababu yeye hajipendi na mwenye huruma (Mithali 31:20, 30). Lakini yeye hajitekelezi mwenyewe; anaweka mwili wake na roho imara na kwa afya njema. Ingawa yeye hufanya kazi kwa bidii na anaendelea masaa mingi, yeye hajoshwi; anajali mambo mazuri ya kujiendeleza mwenyewe na familia yake (Mithali 31:17, 21, 22).

Kinyume na kile ambacho watu wengi wanaamini picha ya kibiblia ya mke wa kiungu, Mithali 31 inaonyesha yeye ni mwenye kuvutia na mwenye bidii. Mke wa Mithali 31 ni mmiliki wa biashara ndogo-anafanya na kuuza nguo. Anafanya maamuzi yake ya biashara kwa kujitegemea, na yeye peke yake anaamua ni nini cha kufanya na mapato yake (Methali 31:16, 24). Angalia, hata hivyo, mapato yake hayaishii kwa kunua viatu au mifuko, lakini kununua shamba ambako anaweza kupanda mizabibu-kitu ambacho kitafaidi familia nzima.

Kupitia jitihada zake zote, huduma, na kazi ngumu, mke wa Mungu anadumisha furaha. Anaweza kutambua yote anayofanya ni faida, ambayo inamfanya atoe furaha (Mithali 31:18). Mke wa kimungu hawi na wasiwasi juu ya ile kesho inaweza kuleta. Anatapasamia wakati ujao kwa sababu anajua Bwana wake ana udhibiti wa kila kitu (Mithali 31:25, 30). Mstari wa 30 ni ufunguo wa kifungu nzima kwa sababu mwanamke hawezi kuwa mke wa kiungu bila kumcha Bwana kwanza. Ni katika kumfuata Yesu amboko mke wa kiungu anaweza kuishi ndani yake na aweze kuzaa matunda ya utakatifu kwa udhihirisho katika maisha yake (angalia Yohana 15: 4).

Mwisho, mke wa kiungu lazima awe chini ya mume wake (Waefeso 5:22). Mke mwenye utiivu anaonekanaje? Sio kile unaweza kufikiri. Biblia inafundisha kwamba Yesu anajiwasilisha kwa Baba yake (Yohana 5:19). Lakini Yesu ni sawa na Baba (Yohana 10:30). Kwa hiyo, mke mwenye utiivu sio wa dhamani ndogo kama mwanadamu; jukumu lake sio la dhamani ndogo — lakini ni tofauti. Wakristo wanajua kwamba Kristo kwa kila kitu ni Mungu kama Baba (na Roho Mtakatifu), lakini kila mmoja ana jukumu tofauti katika ukombozi. Kwa njia hiyo hiyo, wanaume na wanawake kila mmoja huwa na sehemu tofauti katika ndoa. Kwa hivyo, kwa mke kuwa chini ya mume wake kama vile Kristo amejisalimisha kwa Baba ina maana kuwa yeye huruhusu mumewe kuongoza. Yesu alienda msalabani kwa hiari, ingawa bila dhiki (Mathayo 26:39). Kristo alijua njia ya Baba ilikuwa bora. Mke wa kiungu anaweza kupata kuwa njia ya utiivu wakati mwingine ni ya uchungu, lakini kumfuata Mungu kutakuwa na thawabu za kiroho ambazo hudumu milele (1 Timotheo 4: 7-8).

Biblia inalinganisha utiivu wa mume wa mtu na utiivu kwa Mungu (Waefeso 5:22). Kwa maneno mengine, ikiwa mke hawezi kujisalimisha kwa mumewe, inaweza kuwa ni mfano wa mapambano yake ya kunyenyekea kwa Kristo. Uwasilishaji hauashirii udhaifu; mke mwenye mtiivu haimaniishi yeye si "busara" au "hauna si wa maana." Uwasilishaji unahitaji nguvu, heshima, na kujitolea, kama vile tunavyojifunza kutoka kwa mwanamke wa Mithali 31.

Methali 31 inatoa taswira kamili. Mwanamke anaweza kuwa mke wa kiungu bila kuwa mkamilifu (tunajua hakuna kitu kama ukamilifu wa kibinadamu). Lakini kama mke anakua karibu sana katika uhusiano wake na Kristo, atakua zaidi kiungu katika ndoa yake. Uungu mara nyingi ni kinyume na kile jamii ya kidunia inasema mwanamke anapaswa kutamani kuwa. Hata hivyo, kama wanawake wa Mungu haja yetu ya kwanza lazima daima iwe kile kinachopendeza Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kuwa mke wa kiungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries