settings icon
share icon
Swali

Mkristo ni mtu gani?

Jibu


Kwa tafsiri kutoka kamusi ya Webster mkristo ni “mtu mwenye kukiri imani ndani ya yesu kama kristo au dini yenye msingi wa mafundisho ya yesu.” Ijapokuwa huu ni mwanzo mwema wa kufahamu mkristo ni mtu gani, kama maelezo mengi ya kidunia yalivyo, inapungukiwa na uhalisi wa kibiblia juu ya Maana kamili ya ukristo au mkristo.

Neno mkristo limetumika mara tatu katika agano jipya (Matendo 11:26; Matendo 26:28; Petero WA kwanza 4:16). Wafuasi wa yesu kristo waliitwa kwa mara ya kwanza “wakristo” antiokia (Matendo 11:26) kwa sababu tabia zao, matendo yao na hotuba zao zilikuwa kama za Kristo. Ilitumika kiasili na watu wasiookoka wa Antiokia kama jina la kimajazi kuwadhihaki wakristo hao. Ina maana sawa na “Kuwa mmoja wa kundi la kristo” au “mfuasi wa kristo,” ambayo imefanana na tafsiri ya Neno hili katika kamusi ya Webster.

Kwa bahati mbaya, neno mkristo limepoteza kwa kiwango kikubwa usawa wa matumizi yake na Linatumika mara kwa mara kumaanisha tu mtu mwenye dini au pengine muadilifu kinyume cha Mfuasi halisi wa yesu kristo aliyezaliwa mara ya pili. Watu wengi wasioamini na kuwa na tumaini ndani ya yesu kristo hujichukulia tu kuwa ni wakristo kwa sababu wanahudhuria ibada za kanisa ama wanaishi katika taifa la kikristo. Lakini, kuenda kanisani, kuwahudumia wale wasiobahatika maishani au kuwa mtu mzuri haviwezi kukufanya kuwa mkristo. Kama muinjilisti mmoja alivyosema, “kuenda kanisani hakufanyi mtu kuwa mkristo sawa na mtu kuenda gereji hakumfanyi kuwa gari.” Kuwa mshirika wa kanisa anayehudhuria ibada kila mara na kutoa kwa ajili ya kazi za kanisa hakuwezi kukufanya wewe kuwa mkristo.

Biblia inatufundisha ya kwamba matendo yetu mema tunayoyatenda hayawezi kutufanya tukubalike mbele za Mwenyezi Mungu. Tito 3:5 inatuambia ya kwamba “si kwa matendo ya haki tuliyoyatenda, ila kwa huruma zake alituokoa kwa kutuosha na kutufanya upya kwa roho Mtakatifu.” Kwa hivyo mkristo nimtu aliyezaliwa mara ya pili na Mungu (Yohana 3:3; Yohana 3:7; Petero wa kwanza 1:23) na aliyeweka imani na tumaini lake lote ndani ya yesu kristo. Waefeso 2:8 inatuambia ya kwamba “Kwa neema mmeokolewa kupitia imani wala si kwa ajili yenu wenyewe bali ni kipawa cha Mungu.” Mkristo wa kweli ni mtu aliyetubu dhambi zake na kuweka imani na tumaini lake ndani ya Yesu kristo pekee. Imani yao haimo ndani ya kufuata dini ama kanuni Fulani za uadilifu ama miongozo ya kusema fanya hiki na usifanye kile.

Mkristo wa kweli ni mtu aliyeweka imani na tumaini lake lote ndani ya utu wa Yesu kristo na kukubali ya kwamba alikufa msalabani kwa fidia ya dhambi zetu na akafufuka tena siku ya tatu kupata ushindi dhidi ya kifo ili awape uzima wa milele wote wamwaminio. Yohana 1:12 inatuambia ya kwamba “wote waliomwamini aliwapa uwezo kuwa wana wa mungu, kwa wale waliaminio jina lake.” Mkristo wa kweli ni mwana wa Mungu halisi, sehemu ya jamii halisi ya mungu na aliyepewa maisha mapya ndani ya kristo. Alama ya mkristo wa kweli ni upendo kwa wengine na utiifu kwa neno la Mungu (Yohana wa kwanza 2:4; Yohana wa kwanza 2:10).

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo ni mtu gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries