settings icon
share icon
Swali

Je! Mpinga Kristo ni Kiislamu? Je! Mpinga Kristo atakuwa Mwislamu?

Jibu


Pamoja na mvutano unaoongezeka katika Mashariki ya Kati katika miaka ya hivi karibuni, na hasa taarifa za Waislamu wa Shiite kuhusu wasiwasi juu ya Imamu ya kumi na mbili, watu wengi wameanza kuuliza jinsi hii inahusiana na unabii wa Biblia. Ili kujibu, tunapaswa kwanza kujua nani Imam wa kumi na mbili na anatarajiwa kufanya nini kwa Uislam. Pili, tunapaswa kuchunguza maelekezo ya Waislamu wa Shiite kuhusiana na matumaini hayo, na ya tatu, tunahitaji kuangalia Biblia ili kutoa nuru juu ya suala zima.

Ndani ya tawi la Uislam la Shiite, kumekuwa na imam kumi na mbili, au viongozi wa kiroho waliochaguliwa na Allah. Hii ilianza na Imam Ali, binamu kwa Muhammad, ambaye alidai urithi wa kinabii baada ya kifo cha Muhammad. Karibu A.D. 868, Imamu wa kumi na mbili, Abu al-Qasim Muhammad (au Muhammad al-Mahdi), alizaliwa kwa Imam wa kumi na moja. Kwa sababu baba yake alikuwa chini ya mateso makubwa, Mahdi alitumwa mafichoni kwa ajili ya ulinzi wake. Akiwa na umri wa karibu miaka 6, kwa muda mfupi alitoka mafichoni wakati baba yake aliuawa, lakini kisha akarudi mafichoni. Inasemekana kwamba amekuwa mafichoni katika mapango tangu wakati huo na atakuja kurudi kimwujiza kabla ya siku ya hukumu ili kuondoa udhalimu na ukandamizaji wote, kuleta umoja na amani duniani. Yeye ndiye mkombozi wa ulimwengu katika teolojia ya Shiite. Kwa mujibu wa mwandishi mmoja, Mahdi itaunganisha heshima ya Musa, neema ya Yesu, na uvumilivu wa Ayubu katika mtu mmoja mkamilifu.

Utabiri juu ya Imam wa kumi na mbili unafanana na unabii wa Biblia wa nyakati za mwisho. Kwa mujibu wa unabii wa Kiislam, kurudi kwa Mahdi kutatanguliwa na matukio kadhaa wakati wa miaka mitatu ya machafuko ya dunia yenye kutisha, na atatawala juu ya Waarabu na dunia kwa miaka saba. Muonekano wake utafuatana na ufufuo mbili, moja ya waovu na moja ya wenye haki. Kwa mujibu wa mafundisho ya Shiite, uongozi wa Mahdi utakubaliwa na Yesu, na matawi mawili makubwa ya familia ya Ibrahimu yataungana tena milele.

Je! Habari za Waislamu wa Shiite, kama vile Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, inahusishwa na hili? Ahmadinejad ni Shiite ambaye amejitia kwa kina na anadai kwamba atatayarisha kibinafsi ulimwengu kwa kuja kwa Mahdi. Ili dunia iokolewe, lazima iwe katika hali ya machafuko na kutumikisha, na Ahmadinejad anahisi aliongozwa na Allah kuandaa njia kwa hilo. Ahmadinejad mara kwa mara ametoa habari kuhusu kuharibu maadui wa Uislam. Rais wa Iran na Baraza la Mawaziri wake wanadaiwa kutia sahihi mkataba ambao wanaahidi wenyewe kwa kazi yake. Wakati aliulizwa moja kwa moja na mwanahabari wa ABC Ann Curry mnamo Septemba 2009 kuhusu habari yake ya kutabiri hali ya maafa makubwa, Ahmadinejad alisema, "Imam…atakuja na mantiki, na utamaduni, na sayansi. Atakuja hili kusiwe na vita tena. Hakuna uadui Zaidi, chuki. Hakuna mgogoro Zaidi. Ataita kila mmoja kuingia katika upendo wa undugu. Bila shaka, atarudi na Yesu Kristo. Hawa wawili watarudi pamoja. Na kufanya kazi pamoja, watajaza dunia na upendo.

Je! Haya yote yanahusianaje na Mpinga Kristo? Kulingana na 2 Wathesalonike 2: 3-4, kutakuwa na "mtu wa dhambi" aliyefunuliwa katika siku za mwisho ambaye atapinga na kujinpadisha mwenyewe juu ya kile kinachoitwa Mungu. Katika Danieli 7 tunasoma kuhusu maono ya Danieli ya wanyama wanne ambao huwakilisha ufalme ambao hufanya majukumu makubwa katika mpango wa kinabii wa Mungu. Mnyama wa nne ameelezewa (mstari wa 7-8) kuwa ni ya kuogopesha, ya kutisha, yenye nguvu sana, na tofauti na wale waliomtangulia. Pia inaelezewa kuwa na "pembe ndogo" ambayo inangoa pembe zingine. Pembe hii ndogo mara nyingi hujulikana kama Mpinga Kristo. Katika mstari wa 25 inaelezewa akizungumza "Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sharia; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati"(miaka 3 ½). Katika Danieli 8, maono ya kondoo dume na mbuzi hutambua mfalme atakayekuja katika siku za mwisho (mstari wa 23-25), kuharibu watu wengi, na kusimama dhidi ya Kristo, lakini mfalme huyu atavunjika. Katika Danieli 9:27 inatabiriwa kuwa "mwana mfalme atakayekuja" atafanya agano la miaka 7 na watu wengi na kisha kuleta uharibifu mkubwa. Mpinga Kristo huyu atakuwa nani? Hakuna mtu anayejua kwa hakika, lakini nadharia nyingi zimepewa, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kwamba atakuwa Mwaarabu.

Bila kujali nadharia mbalimbali, kuna uwiano machache kati ya Biblia na teolojia ya Shiite ambayo tunapaswa kutambua. Kwanza, Biblia inasema kuwa Ufalme wa Mpinga Kristo atatawala ulimwengu kwa miaka saba, na Uislamu unadai kwamba Imamu wa kumi na mbili atatawala ulimwengu kwa miaka saba. Pili, Waislamu wanatarajia miaka mitatu ya machafuko kabla ya kufunuliwa kwa Imam wa kumi na mbili, na Biblia inazungumzia miaka 3 ½ ya dhiki kabla ya Mpinga Kristo kujidhihirisha mwenyewe kwa kuharibu hekalu la Kiyahudi. Tatu, Mpinga Kristo anaelezewa kuwa ni mdanganyifu ambaye anadai kuleta amani, lakini kwa kweli huleta vita vilivyoenea; tumaini la Imam wa kumi na mbili ni kwamba ataleta amani kwa njia ya vita kubwa na ulimwengu wote.

Je! Mpinga Kristo atakuwa Mwislamu? Mungu pekee anajua. Je! Kuna uhusiano kati ya eskatologia ya Kiislamu na eskatologia ya Kikristo? Hakika kunaonekana kuwa na uhusiano wa moja kwa moja, ingawa ni kama kusoma maelezo ya vita kubwa, kwanza kutoka kwa mtazamo wa mshindwa, akijaribu kuokoa uso, na kisha kutokana na mtazamo wa mshindi. Mpaka tuone utimilifu wa mambo haya, tunahitaji kuzingatia maneno ya 1 Yohana 4: 1-4, "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndio roho ya mpinga Kristo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuweko duniani. Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mpinga Kristo ni Kiislamu? Je! Mpinga Kristo atakuwa Mwislamu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries