Swali
Ni nini maana ya mtazamo wa Kikristo?
Jibu
“Mtazamo” wamaanisha njia mtu anaiona dunia kutoka mahali moja. “Mtazamo wa kikristo,” kwa hivyo wamaanisha jinsi mtu anaiona dunua kiukristo. Mtazamo wa mtu binafsi ni “picha yake kubwa” kuweka pamoja imani zake zote kuhusu dunia. Ni njia yake ya kuelewa ukweli. Mtazamo wa mtu ni msingi wa kufanya maamuzi ya kila siku na kwa hivyo ni muimu sana.
Chungwa lilowekelewa juu ya mesa linaonekana na watu wengi. Mtalaamu wa mimea anayeliangalia analiweka katika kikundi. Mchoraji anakiona chuma na kukichora. Mkusa maua anaona kitega uchumi na kuanzisha. Mtoto anakiona chakula cha mchana na kukila. Vile tunavyoiangalia hali imeshawishiwa na vile tunavyoiona dunia. Kila mtazamo wa Kikristo au usiwe wa kikristo washughulikia mambo haya matatu:
1) Je! Tulitoka wapi? (na ni kwa nini tuko hapa?)
2) Kuna shida gani na ulimwengu?
3) Tunawezaje kuitatua hii shida?
Mtazamo unaokubaliwa wa dunia ni ule wa kimazingira, ambao unajibu maswali matatu kama hivi: 1) Sisi ni uzao wa mazingira na hatuna lengo kamili. 2) Hatuheshimu mazingira vile tunavyostahili. 3) Tunaweza kulinda ulimwengu kupitia utunzaji wa mazingira. Mtu wa mtazamo wa kimazingira anaanzisha maswali mengi ya udadisi kama vile kuwa na imani kuwa tabia na ukweli hubadilika kulingana na tamaduni fulani au taifa, imani kuwa mwanadamu hujiundia tabia zake mwenyewe na wamewajibika kwa matukio yoyote, na ile dhana kuwa kila kitu katika kijiji ni kikamilifu.
Mtazamo wa Kikristo, kwa upande mwingine yajibu maswali hayo matatu kibibilia: 1) Sisi ni viumbe wa Mungu, tulipangiwa tuwe na mamlaka duniani na tuwe na ushirika na Mungu (Mwanzo 1:27-28; 2:15). 2) Tulitenda dhambi kinyume na Mungu na kupelekea ulimwengu wote kuwa chini ya laana (Mwanzo 3). Mungu mwenyewe amekomboa ulimwengu kupitia kwa mwanawe Yesu Kristo kama dhabihu (Mwanzo 3:15; Luka 19:10), na siku moja atarejesha viumbe wote katika hali yao ukamilifu ya zamani (Isaya 65:17-25). Mtazamo wa Kikristo unatuelekeza kuamini, miujiza, utu, na uwezekano wa kukombolewa.
Ni muimu kukumba kwamba mtazamo ni kitu kinachoendelea. Unaadhiri kila sehemu ya maisha kuanzia pesa hadi tabia, kutoka siasa hadi uchoraji. Ukristo wa kweli ni zaidi ya hoja zilizowekwa pamoja kutumika kanisani. Ukristo vilevile umefunzwa katika bibilia wenyewe ni mtazamo. Bibilia kamwe haitofautishi kati ya “dini” na maisha ya kawaida; maisha ya Kikristo ndio pekee yako. Yesu alijitangaza Yeye mwenyewe kuwa “ndimi njia na ukweli, na uzima” (Yohana 14:6) na kwa kufanya hivyo ukawa mtazamo wetu.
English
Ni nini maana ya mtazamo wa Kikristo?