Swali
Mtume ni nani?
Jibu
Neno mtume linamaanisha "mtu ambaye ametumwa." Katika Agano Jipya, kuna matumizi aina mbili ya kimsingi ya neno mtume. Matumizi ya kwanza ni katika kutaja mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo. Matumizi ya pili kwa ujumla inahusu watu wengine ambao wametumwa kuwa wajumbe / mabalozi wa Yesu Kristo.
Mitume kumi na wawili walikuwa na cheo cha kipekee. Katika kurejelea Yerusalemu Mpya, Ufunuo 21:14 inasema, "Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo." Mitume kumi na wawili pia wametajwa katika Mathayo 10: 2 ; Marko 3:14; 4:10; 6: 7; 9:35; 14:10, 17, 20; Luka 6:13; 9: 1; 22:14; Yohana 6:71; Matendo 6: 2; na 1 Wakorintho 15: 5. Ilikuwa ni mitume hawa kumi na wawili ambao walikuwa wajumbe wa kwanza wa injili baada ya kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. Ilikuwa ni mitume hawa kumi na wawili ambao ndio walikuwa msingi wa kanisa-huku Yesu akiwa jiwe jiwe kuu la pembeni (Waefeso 2:20).
Mitume wa aina hii hawako katika kanisa hii leo. Sifa za mtume wa aina hii ni: (1) lazima awe alimwona Kristo aliyefufuka (1 Wakorintho 9: 1), (2) lazima awe alichaguliwa wazi na Roho Mtakatifu (Matendo 9:15), na (3) lazima awe na uwezo wa kufanya ishara na miujiza (Matendo 2:43; 2 Wakorintho 12:12). Jukumu la mitume kumi na wawili la kuweka msingi wa kanisa, pia inaweza kunena upekee wa Mitume. Miaka elfu mbili baadaye bado hatufanyi kazi ili kuweka msingi.
Zaidi ya mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo, pia kulikuwa na mitume wengine kwa ujumla. Barnaba anaitwa "mtume" katika Matendo 13: 2 na 14: 4. Andronicus na Junias huenda wanajulikana kama mitume katika Warumi 16: 7. Neno la Kigiriki lile lililotafsiriwa "mtume" linatumiwa kumtaja Tito katika 2 Wakorintho 8:23 na Epafrodito katika Wafilipi 2:25. Kwa hivyo, inaonekana dhahiri kuwa neno 'mtume' inaweza kutumika kuelezea mtu mwingine badala ya mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo. Mtu yeyote ambaye "alitumwa" anaweza kuitwa mtume.
Kuna jukumu gani hasa la mtume kando ya ile la mitume kumi na wawili? Swala hili haliko wazi hasa. Kutoka kwa ufafanuzi wa neno, mjumbe wa karibu sana hii leo na mtume katika njia ya jumla ni mmishonari. Mmishonari ni mfuasi wa Kristo ambaye ametumwa na ujumbe maalum wa kuitangaza Injili. Mmishonari ni balozi wa Kristo kwa watu ambao hawajapata kusikia habari njema. Ijapokuwa ndio tuzui tashwishi hii, basi itakuwa bora sana kutotumia neno mtume kwa kurejelea nafasi yoyote katika kanisa hii leo. Wingi wa matukio ya neno mtume au mitume katika Agano Jipya hutaja mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo.
Kuna baadhi ya watu hii leo ambao wanatafuta kurejesha nafasi ya mtume. Hili ni vuguvugu hatari. Mara kwa mara, wale wanaodai kuwa mtume wanatafuta mamlaka sawa, au upinzani kwa mamlaka ya awali ya mitume kumi na wawili. Hakuna ushahidi wa kibiblia hasa wa kuunga mkono ufahamu huo wa jukumu la mtume hii leo. Hii itaingiana vizuri sana na onyo la Agano Jipya dhidi ya mitume wa uwongo (2 Wakorintho 11:13).
Kwa kadri, wafuasi wote wa Yesu Kristo wameitwa kuwa mitume. Sisi sote tumekuwa mabalozi Wake (Mathayo 28: 18-20; 2 Wakorintho 5: 18-20). Sisi sote tunapaswa kuwa "wale waliotumwa" (Matendo 1: 8). Sisi sote tunapaswa kuwa wahubiri wa habari njema (Warumi 10:15).
English
Mtume ni nani?