Swali
Je! Ni nini maana ya mwandamano? Je! Ina maan kushikilia dhana ya mwandamano?
Jibu
Tafadhali kumbuka, kama huduma, GotQuestion.org haikubaliani na miujiza endelefu. Makala ya hapa chini yameandikwa na mtu ambaye anaamini uendelevu wa miujiza. Tulifikiri itakuwa bora zaidi kuwa na Makala ambayo yanakuza dhana ya uendelivu wa miujiza, vile kamwe ni vyema mtazamo wetu kupigwa msasaa, na hii itatutia motisha zaidi kuendelea kuyatafiti Maandiko ili kuhakikisha kuwa itikadi zatu ni za kibiblia.
Dhana ya uendelevu ni itikadi inayosema kuwa karama za kiroho, ikiwa ni Pamoja na uponyaji, ndimi, miujiza bado inaendelea hii leo, jinsi ilivyokuwa siku za kanisa la kwanza. Dhana ya uendelevu wa miujiza inaamini kuwa karama za kiroho zimekuwa "zikiendelea" haijapungua tangu siku ya Pentekote na kuwa kanisa la hii leo linaweza kusifikia karama zoate za kiroho ambazo zimetajwa katika Biblia.
Wakati Roho Mtakatifu alikuja vile Yesu aliahidi (Matendo 1:8; 2:1-4), aliwajaza waumini na kuwapa karama sisizo za kawaida na kuwawezesha kumtumikia Mungu kwa nguvu na uwezo. Karama hizi za kiro zimeorodheshwa katika Warumi 12: 6-8, Waefeso 4:11, na 1 Wakorintho 12:7-11, 28 na kanuni endelevu inasema kwamba karama zote zinaendelea hii leo. Karama hizi huwa tofauti kutoka mtu hadi mwingine vile Roho anaona vyema (1Petro 4:10). 1 Wakorintho 12:4-6 inasema, "Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote." Wafuasi wa kanuni endelevu inashikilia kuwa hakuna ushahidi wa kiroho wa kuwa kati ya hizi karama za roho hazifanyi kazi tena.
Mtazamo ulio tafauti na na kauni endelevu unaitwa kanuni kikomo, ambao unafunza kwamba baadhi ya karama "zilikoma" na hivyo hazitumiki siku hizi. Swali wanakanuni ya kikomo sio kuwa kama ikiwa kuna karama bado zinapeana, lakini ni karama gani inapeanwa. Wenye kanuni kuwa karama zilikoma mara nyingi hutaja aya kama 1 Wakorintho 13:10 na ukweli kwamba karama ya miujiza inaonekana kuwa karibu na huduma ya mitume na udhibitisho wa ufunuo wa Mungu (Matendo 2:22; 14:3; 2 Wakorintho 12:12) kama ushahidi kwamba karama za miujiza za Roho zilikoma.
Vile ilivyo kwa kanuni yoyote, kunayo kupita kadri katika upande wowote. Baadhi ya wanaoshikilia kanuni kuwa karama zote zilikoma wanaamini kuwa zilikoma pamoja na mwisho wa wakati wa mitume. Wanaoshikilia kanuni kuwa karama zilikoma ambao si wenye msimamo mkali wanashikilia kwamba ni "karama za kiroho"-uponyaji, miujiza, na ndimi- zimekoma. Katika upande wale wanaovuka mipaka kwa kaunga kununi kuwa karama bado zinaendelea, miongoni mwao kunao wale wanaofundisha kuwa kuongea katika ndimi kila mara lazima ifuate wokovu au kujazwa kwa Roho Mtakatifu. Kunaweza kuwa na msisitizo potovu katika karama badala ya Utu wa Yesu Kristo. Baadhi hudai kuwa kila muumini anaweza kujazwa na kila karama ya miujiza ikiwa yeye ana Imani ya kutosha. Lakini dhana hii inakataliwa wazi katika 1 Wakorintho 12:11, ambayo inasema kwamba Roho "ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe." Paulo alishughulikia jambo hili katika kanisa la Korintho: "Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza? Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Je, wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha?" (1 Wakorintho 12:29-30). Jibu kwa swali hili la kimajazi ni "la."
Wanaoashikilia kuendelea kwa karama wanaamini kuwa maagizo ya kibiblia kuhusu karama za kiroho ni muhimu hii leo jinsi na namna ilivyokuwa wakati Biblia iliandikwa. Wanashikilia kuwa hakuna sababu ya kibiblia ya kuamini kinyume na kwamba gharama ya kudhibitisha iko kwa wanaoamini kuwa karama zilikoma. Waaumin wa pande zote za jambo hili wanaweza kukubaliana au wasikubaliane, lakini mitazamo yote miwili lazima iwe na ombi la Yesu katika Yohana 17:22-23: "Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja; 23mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi." Iwe ni wale wanaoshikilia kuwa karama zinaendelea au wale mtazamo kuwa zilikoma, wote ni waumini ambao wamezaliwa mara ya pili ni sehemu ya mwili Kristo (1 Wakorintho 12:27). Wakati tunaruhusu suala lolote lisilo la msingi kusababisha mgawanyiko na fitina, hatutilii maanani jambo ambalo ni la muhimu kwa Bwana wetu.
Ongezeko la ubishi la wanaoamini kuwa karama zilikoma na jibu la wanaoamini kuwa karama zinaendlea
Wakristo wanaoshikilia msimamo kuwa hakuna msingi wa kibiblia usemao kuwa kukoma kwa karama wakati mwingine unaitwa "kuendelea kwa karama." Waumini hawa huchukulia kues msimamo wao umeambatana na biblia na hivyo kanuni ya kuwa karama zilikoma haina msingi wowote wa kiroho. Yafuatayo ni baadhi ya mabishano ya kanuni kuwa karama zilikoma na majibi ya wanakununi kuwa karama bado zinaendelea:
1. Maandiko
Wanakanuni kuwa karama zilikoma mara nyingi hutaja 1 Wakorintho 13:8-10 ili kuunga mkono hoja kwamba baadhi ya karama zilikoma wakati "ukamilifu" ulikuja. Baadhi ya wanaamini kuwa "ukamilifu" inamaanisha kukamilika kwa Biblia. Msimamo huu unashikilia kwamba pindi tu Biblia ilifikia kukamilika kwake, hakukuwa na haja tena Roho Mtakatifu kufanya miujiza kupitia kwa waumini. Ijapokuwa, aya ya 12 inafafanua zaidi utambulisho wa "ukamilifu" huo: "Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana." Jinsi hatuwezi kuona Biblia ana kwa ana, au Biblia yenyewe "kututambua", wanakununi endelevu huchukulia haya kumaanisha ujio wa Yesu mara ya pili. Katika wakati huo hakutakuwa na haja ya karama ya Roho Mtakatifu, ikiwa ni Pamoja na kipaji cha maarifa (aya ya 8), kwa kuwa sisi tutakuwa mbele za Yesu Mwenyewe.
Aya nyingine ambayo mara nyingi hutajwa ni 2 Wakorintho 12:12. Wanakanuni kukoma kwa karama wanashikilia kwamba karama za miujiza kama vile, ndimi, uponyaji, unabii, na miujiza zilikuwa hifadhi kwa mitume tu pekee kwa kudhibitisha mamlaka yao. Ingawa, Biblia inajumlisha samulizi za wale hawakuwa mitume katika kanisa la kwanza lakini ile hali walitenda miujiza na uponyaji kama vile Stefano (Matendo 6:8) na Filipo (Matendo 8:6-7). Karama za ndimi na unabii vilikuwa vimeenea sana karibu kwa kila mtu ambaye alikuwa amejazwa na Roho Mtakatifu (Matendo 10:46; 19:6; 1 Wakorintho 14:5, 39; Wagalatia 3:5). Paulo anajumlisha karama hizi za miujiza wakati alikuwa anazungumza na kanisa la Korintho (1 Wakorintho 12:4-11, 28). Wanakanuni ya uendelevu wa karama hubishi kuwa ikiwa, ndimi, uponyaji, na miujiza ilihusika na mitume, karama hizi hazingeweza jumulisha katika maagizo ya Paulo kwa kanisa mianga mingi baada ya Pentekote. Paula alikauli, "Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu" (1 Wakorintho 14:5). Kutokana na ayah ii, tunaweza kusema kuwa Paulo hakuchukulia karama kukoma na mitume. Nguvu sisizo za kawaida zenye mitume walionyesha (Matendo 15:12) huenda zilikuwa ni kwa sababu ya Yesu Mwenyewe kuwapa wale kumi na wawili hizi nguvu kama wajumbe wake maalum (Luka 9:1). Uwezo wao wa kufanya miujiza haukuwa na uhusiano hasa wakfu wa karama za roho ambazo zilitumika na waumini wote waliojazwa na Roho.
2. Neno
Neno karama ishara mara nyingi inatumika kuonyesha kwamba Mungu alipeana uwezo Fulani kwa mitume kama "ishara" ya kudhibitisha utume wao. Baadhi ya wanatheolojia wamelipinga suala hilo, wakikauli kuwa Biblia inaongelelea juu ya ishara za mtume wa kweli haionyeshi kuwa baadhi ya karama za kiroho ni ishara ambayo inashiria utume. Wanaoendeleza kanuni ya kuendelea kwa karama wanaamini kuwa Agano Jipya inarejelea "ishara" ikimaanisha kuwa uwezo usio wa kawaida unapeanwa na Mungu kwa yeyote anachagua ili kutimiza kusudi lake (Kutoka 7:3; Warumi 15:18-19; Waebrania 2:4; 1Wakorintho 12:11). Neno karama ishara halitumiki kwa aina yake kuhusiana na Roho Mtakatifu.
Unabii ni neno lingine ambalo limeibua mtafaruku. Wanakanuni ya kuendelea kwa karama hutaja baadhi ya mifano ya wale wanaoamini kanuni hii na wameishi kadri na mjibu wa Maandiko. Ingawa, wengi wa wanakanuni ya uendelevu wa karama hukubaliana na wanakununi wa karama kukoa kuwa hamna ufunuo wanadamu wamepewa ambao utawai kuwa karibu na Biblia iliyokamilika. Walakini, waendelezaji wa karama hawaoni chochote katika maandiko ambacho kinaonyesha kuwa Mungu wa uhusiano alitupa Maandiko kwamba haneni na watu wake. Karama ya unabii inaweza kuhuzisha kuongea ukweli wa Neno la Mungu, lakini inaweza kuwa ni Pamoja na ufunuo usio wa kawaida ambao Mungu huwapa watumishi wake ili kuwashawishi wengine katika njia mwafaka. Mtume Paulo alihimiza kanisa "Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu" (1 Wakorintho 14:1).
3. Ndimi
Mada ya kuongea katika ndimi imekuwa chanzo cha kutoelewana kwa Wakristo wengi. Umiaji wake mbaya katika baadhi ya makundi umezidisha Imani kwa wanaoamini kuwa karama zilikoma na kwamba hizi karama haziko katika maisha yetu na sio muhimu. Baadhi hukisia tabia hii kuwa kazi ya mapepo au mhemko wa hisia. Vile vile wanashikilia kuwa, ikiwa ndimi zilikuwa karama halisi, kila mjumbe angepewa karama hii ili aepuke miaka ya kusomea lugha.
Kwa kujibu, waendelezaji kanuni ya karama wanakubali kwamba baadhi ya yale ambayo yanakisiwa kuanzishwa na Roho sio kitu kingine zaidi ya hisia za mhemko. Shetani na binadamu wale ambao wameanguka mara nyingi wakiiga kazi ya miujiza ya Mungu na bado wanaendelea (Kutoka 7:10-11; Matendo 8:9, 11; Ufunuo 13:14). Walakini, kuwepo kwa muigizo hautoi ukweli wa kile kilicho halisi. Katika Matendo 16:16, Paulo na Sila waliudhiwa na yule mwanamke aliyepagagwa na pepo ya unabii. Ukweli kuwa uwezo wake usio wa kawaida ulitoka kwa Shetani na sio Mungu haukumfanya Paulo kutamatisha kuwa karama zote za unabii ni za kishetani (1 Wakorintho 14:1). Katika Mathayo 7:21-23, Yesu alibashiri kuwa wengi watasema wanamjua kwa sababu walifanya miujiza kwa jina lake. Ukweli kwamba kulikuwa na walaghai haikumaanisha kuwa kila mtu aliyetenda ishara ilikuwa bandia.
Wanakanuni ya karama endelevu wanapendekeza kuwa baadhi ya switofahamu kwa suala hili ni kuwa huenda kukawa na aina mbili ya "ndimi" zilizosungumziwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume na barua kwa Wakorintho. Kipaji kilichoshuka siku ya Pentekote kiliwawezesha mitume kunene katika lugha za wale waliokuwemo. Hii iliwezesha injili kuenea kwa kasi sana katika eneo hilo (Matendo 2:6-8). walakini, katika 1 Wakorintho 14, Paulo anaonekana kuongelelea juu ya kusudi tofauti la ndimi. Katika mlango wote wa kumi na nne ni maagizo kwa kanisa kuhusu kusudi na matumizi ya vipaji, mojawapo inaweza kuwa ni kwa kuabudu (1 Wakorintho 14:2, 14-16, 28).
Uungwaji wa Kibiblia wa msimamo huu unapatikana Matendo 10:45-46 wakati Konelio alipokea Roho Mtakatifu. Alianza kumsifu Mungu katika ndimi, hata kama hakukuwa na mtu yeyote aliyehitaji kusikia injili kwa lugha nyingine. Mfano mwingine uko katika Matendo 19:6-7. Wanaume kumi na wawili kutoka Efeso walipokea Roho Mtakatifu na wakaanza kuongea katika ndimi, hata kama hakukuwa na mtu yoyote aliyehitaji kusikia injili. Kanisa la Korintho mara kwa mara lilihusisha ndimi katika ibada yao, bila dalili yoyote ya kuwa kulikuwa na watu miongoni mwao waliohitaji kuusikia ujumbe katika lugha nyingine.
Katika 1 Wakorintho 14:28, Paulo anaendelea na maagizo juu ya utumizi wa ndimi katika ibada ya Pamoja: "Lakini kama hakuna awezaye kufafanua, basi, mwenye kusema lugha ngeni anyamaze mkutanoni, aseme na nafsi yake mwenyewe na Mungu." Hii inaonekana kumaanisha kuwa ndimi zinaweza kuwa njia mojawapo ya kuomba "katika roho," ambayo inatupa mtazamo mwingine kwa vifungu kama 1 Wakorintho 14:14-15 na 28, Warumi 8:26, Waefeso 6:18, na Yuda 1:20. Paulo hakuwai waadhibu Wakorintho kwa kutumia kipaji hiki (1 Wakorintho 14:39) bali pale walipokitumia vibaya kwa kuzua mchafuko (aya ya 23 na 39). Mlango wa kumi na nne unatamatisha Paulo akiwaagiza kuwa "lakini msimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni. Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwa utaratibu" (1 Wakorintho 14:39-40).
4. Historia ya Kanisa
Wanakanuni ya kukoma kwa karama wanadai uungwaji wa kihistoria, huku wakikauli kuwa hakuna ishara kuwa ishara za miujiza iliendelea baada ya mitume kufa. Walakini, wanakanuni wa karama endelevu wanashikilia kwamba rekodi ya kanisa haikubaliani. Wao hutaja mifano ifuatayo:
Justin Martyr (AD 100-165), mwanahistoria wa kanisa wa kwanza, alisema kuwa "karama za unabii imabaki nasi hadi wakiti huu. Sasa kuna uwezekano kuona miongoni mwetu wamawake na wanaume ambao wanamiliki karama za Roho wa Mungu."
Irenaeus (AD 125-200) alisema, "Pia twawasikia wependwa wengi katika kanisa ambao wana kipaji cha unabii na kupitia kwa Roho wanazungumza lugha zoteā¦Hata wafu wamefufuliwa, na kuishi pamoja nasi kwa miaka mingi."
Novatian (AD 210-280) alisema, "Huyu ndiye (Roho Mtakatifu) yule awawekaye manabii katika kanisa, akiwafunza waalimu, kuongoza ndimi, kupeana nguvu na uponyaji, na anafanya kazi nzuri ya ajabu."
Augustine (AD 354-430) pia ananukuliwa kama baba wa kanisa la kwanza ambaye alikataa wazo la kuendelea kwa karama. Hii ilikuwa kweli hapo mapema. Walakini, baadaye katika maisha, alishawishika na uponyaji na miujiza ambayo aliishuhudia na kuiandika katiak Mji wa Mungu (The City of God), "Ninashawishika na ahadi ya kuimaliza kazi hii na kuwa sitaweza kurekodi ishara zote ninazozijua."
Wasomi wengi wa hivi majuzi wa Biblia kama vile John Wesley, A. W. Tozer, R. A. Torrey, na J.p. Moreland pia waliamini kuwa karama zote za Kiroho bado zinafanya kazi ulimwenguni hii leo, na kwa kweli walifanya chini ya karama hizo.
5. Majadiliano/mabishano kutoka kwa Silence
Wanakanuni wa karama kukoma wanasema kwamba barua za mapema za Paulo zilikuwa na marejeleo ya ishara za karama. Baadaye barua kama Waefeso hazikuzitaja. Hitimisho lao ni kuwa karama hizi lazima "zilikufa" baada ya kanisa lilikua limekua dhabiti. Walakini, wanakanuni wa karama endelevu wanasema kuwa huu ni ubishi kutoka kwa Silence, ambao ni ni uwongo. Ukosefu wa rejeleo kwa suala kwa vyovyote vile haimanishi kuwa maagizo yah apo awali yalikuwa yamebadilika. Inaweza kumaanisha kuwa karama za miujiza hazikusababisha rabsha katika Efeso jinsi zilivyofanya Korintho, na mambo mengine yalikuwa ya muhimu na kustahili Paulo kuyashughulikia. Orodha ya vipaji inayopatika katika Warumi 12:6-9, 1 Wakorintho 12:4-11, na 1 Petro 4:10-11 hazifanani na labda hazikukusudiwa kuelezewa kwa undani.
Wengi wa wasomi wa Biblia huwa pande zote mbili za suala hili. Wanakanuni ya karama kukoma wanashikilia kuwa Neno lilo na pumzi ya Mungu ndilo tunalohitaji pekee kuishi jinsi Kristo anavyotukusudia kuishi. Wanakanuni wa karama endelevu wanasema kuwa Roho Mtakatifu amabye alimiminwa katika Matendo 2 bado anaendeleza kazi yake, pamoja na karama zote sisizo za kawaida ambazo zimetajwa katika Maandiko. Daudi Martyn Lloyd-Jones, mwanatheolojia wa karne ya 19 ambaye mara nyingi ananukuliwa kuwa muunga mkono wa karama kukoma anasema haya: "Kila Mkristo lazima kila wakati atafute kile kilicho bora na kikuu. Kamwe tusiridhike na chochote havifu kuliko kile kilichoelezewa kuwa na uwezekano Mkristo kukipata katika Agano Jipya." Kwa hilo, pande zote zitasema, "Amina."
English
Je! Ni nini maana ya mwandamano? Je! Ina maan kushikilia dhana ya mwandamano?