settings icon
share icon
Swali

Ni kwani watu katika Mwanzo waliishi maisha marefu?

Jibu


Wakati mwingine ni maajabu kwa nini watu katika fifungu vya kwanza kwanza katika Mwanzo waliishi maisha marefu. Kuna maelezo mengi yamewekwa mbele na wadadisi wa bibilia. Kizazi katika Mwanzo 5 unanakili uzao wa Mungu wa Adamu- uzao ambao utamzaa mkombozi. Hii ikiwa elezo liwezekanalo, hakuna mahali bibilia inapunguza miaka ya kuishi kwa watu ambao wametajwa katika Mwanzo 5. Zaidi mbali na Enoshi Mwanzo 5 haimtambui mtu yeyote kuwa mcha Mungu. Kuna uwezekano kuwa kila mtu wakati huo umetolewa aliishi mamia ya miaka. Hali mbalimbali zilichangia.

Mwanzo 1:6-7 inataja maji kuwa juu ya nchi, kivuli cha maji ambacho kilizunguka ardhi. Kivuli kama hicho cha maji kingetengeneza uvuli ambao ungezuia joto na kwa hivyo kuelekea ongezeko la joto. Hii ingetokea katika sehemu zinazokaliwa na watu. Mwanzo 7:11 yaonyesha kwamba, katika wakati wa gharika, kivuli cha maji kilimwagwa juu ya nchi, na kuatarisha maisha. Linganisha kipindi cha maisha kabla ya gharika (Mwanzo 5:1-32) na yale maisha baada ya gharika (Mwanzo 11:10-32). Pale tu baada ya gharika miaka ya kuishi ilipungua.

Hali nyingine ni kuwa vizazi vichache baada ya uumbaji, chembe chembe za damu ya mwanadamu ikawa na madhara. Adamu na Hawa waliumbwa wakamilifu. Kwa kweli walikuwa na kinga ya mwili ya juu sana. Vizazi vyao wangeridhi uzuri huu ingawa kwa kiwango cha chini. Baada ya muda kwa sababu ya dhambi chembe chembe za mwanadamu iliendelea kuaribiwa, na mwanadamu akaadhirika na kifo na magojwa. Hii nayo ingepelekea kupungau kwa kipindi cha miaka ya kuishi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwani watu katika Mwanzo waliishi maisha marefu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries