Swali
Mwenye mawazo huru ni nini?
Jibu
Mwenye mawazo huru ni mtu anayedai kuunda maoni kwa msingi wa mantiki, mbali na mila, mamlaka, au imani zilizowekwa. Kwa kawaida, kufikiria huru kunahusishwa na wale wanaotilia shaka dini. Wawaza huru ni watu wa asili na hawategemei maadili kwenye kiwango kilichowekwa na kiumbe kilicho juu sana.
Mawazo huru yanakataa mifumo ya kijadi ya kijamii au kidini. Chenye huwaunganisha watu wenye fikra huru sana sana sio imani zao, bali ni njia ambayo wanazishikilia. Ikiwa mtu wa mafikra huru ana itikadi kwa sababu mtu mwingine amemfahamisha kuwa ni za kweli wakati alikuwa mtoto au ikiwa anazishikilia kwa sababu ndizo zinazompa tumaini au kumfurahisha, mawazo yake hayazingatiwi kuwa huru. Ikiwa, badala yake, ana imani kwa sababu ya kuliwaza kwa uangalifu, anapata uswa wa ushahidi katika neema ya imani, basi mawazo yake ni huru, bila kujali tamatizo lake linaonekana namna gani.
Watu wengi wa mawazo huru huamini kuwa hakuna Mungu (ingawa baadhi ya waumini wasiokubali ufunuo pia hujiiita wawaza huru). Kwa kuwa wao ni wa kimaumbile, watu wanalio na fikira huru huona ukweli kuwa ni mdogo mno kwa kile kinachotambulika moja kwa moja kupitia hisia za kiasili au kupitia akili. Hawakubali uthibitisho wa kutosha wa kuwepo kwa Mungu katika ulimwengu wetu kuwa sababu ya kutosha ya kumwamini Mungu. Wala hawaikubali Biblia kuwa ufunuo wa Mungu ambao kupitia huowanadamu wanaweza kumjua. Biblia inatuambia, “Mpumbavu anasema moyoni mwake,“Hakuna Mungu” (Zaburi 14:1; 53:1). Wenye mafikirio huru hupuuza amri ya Biblia ya “wala usizitegemee akili zako mwenyewe” (Mithali 3:5) na kupatana na maelezo katika Warumi 1:22: “Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga.”
Watu wa mafikirio huru wanaamini kwamba njia pekee ya kuwa huru kwa kweli ni mtu kujiondoa kwa kweli kutoka kwa kila aina ya ushirikina wowote, maandiko matakatifu, imani, masihi, na “uongo” Wowote. Maana yote kwao hupatikana na kuundwa na nafsi, kwa kuwa maana hutoka katika akili ya mtu. Biblia inatuambia kwamba uhuru unapatikana katika Kristo (Yohana 8:36). Hakuna mtu yeyote anayeweza kujiletea uhuru. Watu wamefungwa na dhambi hadi Yesu awatakase na kuvunja nguvu ambayo dhambi na mauti vinawashikilia (Warumi 6). Mungu humpa kila mtu uhuru wa kuchagua kile watakacho kiamini, lakini hii haimaanishi kuwa kila wazo mtu anafikiri ni la kweli. Ukweli wa kimalengo upo, iwe tutaamua kuamini au kutoamini. Kwa kuamini mawazo ”yasiyo na Mungu,” watu wenye mawazo huru hutumia uhuru ambao Mungu anawapa kuishi wakiwa wamenaswa na uwongo. Wao wamefungwa, hawako huru.
Watu wengi wa fikra huru ni wanapenda utu, wanaoegemeza maadili juu ya mahitaji ya binadamu, si yale wanayoona kuwa ya kudhamiriwa kuwa “ulimwengu kamili.” Mara nyingi, mtazamo wao wa ulimwengu unajumuisha heshima kwa sayari na wanyama, vile vile na kujitolea kwa dhati kwa usawa. Wakati watu wa fikra huru wanajaribu kufanya chenye wanaona ni bora, na huku kinastahili pongezi kuwa mtu mwenye fadhili, kurudia, na kuhifadhi na kudumisha thamani ya maisha, haitafikia kiwango kila wakati. Hakutawai kuwa na sababu ya kutosha ya kuendelea kufanya mambo haya- wala umoja wa kukubaliana juu ya kile ni sahihi na kile si sahihi- ikiwa imani ni tokeo la sababu za kibinafsi. Zaidi ya hayo, hata matendo mema, ya kibinadamu ni kama nguo chafu kwa Mungu bila Roho Wake (Isaya 64:6). Haviwezi kamwe kuongoza kwenye msimamo ufaao pamoja na Mungu. Jaribio lolote la kuleta wema katika ulimwengu bila Mungu linafanywa kwa nia mbaya nay a ubinafsi. “Wema” wa mwanadamu mbali na Kristo hatimaye ni ubatili.
Katika kitabu cha Ethics of Belief (Itikadi za Maadili), mwanahisabi na mwanafalsafa William Kingdon Clifford atoa muhtasari wa imani ya mtu mwenye mawazo huru kwamba “ni makosa sikuzote, kila mahali, na kwa mtu yeyote, kuamini chochote bila uthibitisho wa kutosha.” Ni kweli kwamba kuamini kitu bila ushahidi wa kutosha itakua ni upumbavu. Biblia inatuhimiza tuwe watetezi wa kile tunachokiamini (1 Petro 3:15). Kihistoria, kisayansi, na kiutafiti wa vifusi, Biblia inaweza kupinga tetezi zozote na kutoa ushahidi mwingi wa imani (Luka 1:1-4; Matendo 26:25-26). Biblia inatuahidi kwamba tukitafuta, tutapata (Mathayo 7:7-8). Kunayo zaidi ya Ushahidi wa kutosha wa kuamini kweli za Biblia. Wale wanaoitaftua kweli hiyo kweli itapatikana na watawekwa huru na Mungu ambaye ni Kweli (Yohana 14:6).
English
Mwenye mawazo huru ni nini?