Swali
Ina maana gani kwamba Yesu atarudi kama mwizi usiku?
Jibu
Kurudi kwa Yesu Kristo kunalinganishwa na kuja kwa mwizi usiku. Vifungu viwili vinavyotumia neno "mwizi usiku": Mathayo 24:43, "Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye numba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe," na 1 Wathesalonike 5: 2, "Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku."
Katika Mathayo 24, Yesu anasungumzia ujio wake wa pili baada ya mwisho wa dhiki. Paulo anaiita "siku ya Bwana" katika 1 Wathesalonike 5. Hii ni siku ya adhabu ya kiungu itakua na mlipuko wa kuogofya na "ishara ya Mwana wa Adamu" itaonekana mbinguni (Mathayo 24: 29-30). Yesu anasema itatokea "baada ya dhiki ya siku hizo" (mstari 29), maelezo ambayo yanafafanua tukio hili kutoka kwenye kunyakuliwa, ambayo yatatokea kabla ya dhiki.
Je! Ujio wa pili utakuwa kama mwizi ajeye usiku? Kipengele muhimu cha kulinganisha ujio wa Yesu ni kwamba hakuna mtu atakayejua wakati atarudi. Kama vile mwizi anavyompata mwenye nyumbakwa mshangao, Yesu ataishtukia dunia isiyoamini wakati atakaporudi na hukumu. Watu "watakula na kunywa, kuooa na kuoza katika ndoa" (mstari wa 38), kana kwambwa walikuwa na wakati wote duniani. Na, kabla wagundue, Siku ya Hukumu itakuwa juu yao (mistari 40-41). Paulo anasema hivi: "Watu watakapokuwa wanasema: 'Kila kitu ni shwari na salama', ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo" (1 Wathesalonike 5: 3).
Muumini haogopi hukumu hii ya haraka na ya ghafla; "mwizi wa usiku" hatatupata kwa mshangao. Wakristo wako katika kitengo tofauti: "Lakini ninyi, ndugu na dada, hamko katika gizani, na siku hiyo hapaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi" (1 Wathesalonike 5: 4). Ni wale tu walio katika giza ambao watakujiwa kwa mshangao, na sisi "tunaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi is watu wa usiku, wala wa giza" (mstari wa 5). Msifuni Bwana, "Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (mstari wa 9).
Wale hajaokolewa wanapaswa kuzingatia onyo la Yesu: "Kwa hiyi, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia" (Mathayo 24:44). Unawezaje kuwa tayari? Mungu amekupa njia ya kuepuka hukumu. Njia hiyo ni Yesu Kristo (Yohana 14: 6). Kwa kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wako, umepewa msamaha wa dhambi, huruma, na wokovu na ahadi ya uzima wa milele (Yohana 3:16, Waefeso 2: 8-9). "Mwizi" anakuja, lakini unaweza kuwa mtoto wa mwanga. Usiuzime; huu ni "mwaka wa neema wa Bwana" (Luka 4:19).
English
Ina maana gani kwamba Yesu atarudi kama mwizi usiku?